Risk Assessment and Management: CHADEMA nayo Imuondoe Dr. W. Slaa!

Risk Assessment and Management: CHADEMA nayo Imuondoe Dr. W. Slaa!

hapana ndugu yangu unajipinga tu; kama Dr. Slaa inapaswa aondolewe kwa sababu ya dini yake ili kuwaridhisha watu wa dini nyingine basi kuna udini maana mtu anahukumiwa kwa msingi wa dini yake. Na wewe mwenyewe ulilikoroga mwanzoni uliposema bila ku-qualify kuwa "Waislam hawamtaki" na hapo ukaingiza Dini wewe mwenyewe. Sasa pendekezo lake halihusiani na uwezo wa Dr. Slaa, makosa yake, kushindwa kwake kama kiongozi wala nini; pendekezo lako linasema Dr. Slaa alikuwa padre =>jambo hilo linawatisha Waislamu => Waislamu hawaikubali Chadema = Dr. Slaa aondoke ili Waislamu waikubali Chadema!

Nisahihishe kama huo sio mlolongo wa hoja yako. Maana naweza kuwa nimekuwa too harsh kwa kumiss kitu fulani hapa.
 
Tunasahau hizi tuhuma zimezushwa na kundi la mafisadi ambao wanaamini kuwa CDM ndio imekuwa kikwazo. Tunajua kuwa kundi hili limeshutumiwa bila kupinga tuhuma za kupanga mauaji ya viongozi wa siasa wanaoonekana mwiba(rejea shutuma za Dr Mwakyembe) likaajiri watu ndani ya yombo vya dola na kutoka somali eti kupambana na wanaoushambulia uislam.!!!
Mbinu zao ziliposhindwa wakahamia kwenye agenda yao ya mwanzo ya udini na ni hawa ndio wanaofadhili shughuli nzima ya propaganda.

Kama kiongozi kuwa ni padre ni makosa, basi hatutakuwa na viongozi asilani kwani akiwepo Alhaji wakristo watasema huyo ni Alhaji CDM wamuondee. Wakiweka pagan, wakristo na waislam watasema huyo ni mshirikina muondoeni. Wakiweka Atheist watasema huyo hamjui mungu yoyote muondoeni. Tunabaki na swali moja, je kiongozi wa kisiasa anatakiwa aweje kiimani ili kuwafurahisha watu wote?

Kufanya mambo kwa hofu au shinikizo la kikundi ni hatari sana, CUF waliandika rasimu ya katiba yao na Mtatiro licha ya usomi wake akaandamana kwa kishinikizo la kikundi cha CUF na kupeleka rasimu kusikojulikana na bila kujua utaratibu wa kuandika katiba yenye maana. Leo ukimuuliza Mtatiro je walitaka nini na kwa utaratibu gani, hana jibu. Ameadhirika sana kisa tu kufuata mashinikizo ya mitaani.
CDM wakifanya mambo kama CUF sijui kama watasalimika.

CDM walipofanya maandamano kanda ya ziwa waliungwa mkono na wananchi wengi, si kwasababu ya Slaa au Halima Mdee ni kwa ujumbe'message' iliyogusa maisha ya wananchi, umeme, kupanda gharama za maisha, Katiba na Dowans. Wananchi hawakuona tofauti zao zaidi ya shida zao za pamoja. Hiki ndicho CDM wanapaswa kuendelea nacho sehemu zote nchini ikiwa ni pamoja na sehemu ambazo hawafiki(pwani na kusini). Mwisho wa siku wananchi watajua ni nani yupo nao na ni akina nani wanawadangaya.

Hatuwezi kuwa na viongozi kwa kuangalia imani zao kwani kufanya hivyo kutawafunga na kutunyima watu wenye thamani katika taifa letu.Jiulize Rais au waziri ambaye ni wa imani yako amebadilishaje maisha yako? Na je ukitaka kugombea nafasi za uongozi basi hupaswi kwenda Roma au Mecca ili usijeudhi baadhi ya watu!!

Thamani ya kitu ipo machoni na mioyoni mwa watu, CDM wasimamie thamani hizo na kuzibainisha kwa mifano kama ilivyokuwa Halamashauri ya Karatu ambayo kila mtu aliisifu na kuipenda chini ya Slaa. Hakuna sababu ya kwenda na upepo kwani hawa watu wanaoeneza udini ni wafanyakazi, walikuwepo CCM wakati wa Mkapa, wakahamia CUF na sasa hatujui wamerudi CCM au wameajiriwa na mafisadi. Nawahakikishieni wapo waislam wanaochukizwa sana na hili kundi na ni wengi bahati mbaya hawana vipaza sauti.Ni makosa kufikiri kikundi cha watu wachache au wa mtaa fulani ni jamii nzima.

Na mwisho, ninyi wanJF ambao wengi ni wapenzi wa CDM mnapoleta thread za uchambuzi wa uteuzi wa viongozi kwa imani zao na kejeli za dini mnaisadiaje CDM kukabiliana na uongo?
 
2011-2015 is four years battle ambapo only brave fighters can last. Nadhani ni wazi kwamba Dr slaa anaweza kufanya makongamano kadhaa na waislam. Mfano, Dr.Slaa anaweza kukutana na Young educated Muslim ambao wako na views toward Tanzania development less than muslim development. Hapa akawaambia kwamba majority of Tanzania have the same problem as you, they don't have sustainable energy, they can't afford three meals a day. This is our battle and not Roman battle neither Saudi Battle, This is Tanzanian battle. I believe this young mind will pass the idea to another. Remember you don't build a tower top bottom, you build bottom up.

Nimependa, haya mapendekezo tuliyatoa sisi wengine kwa Chadema wakati ule lakini nani alikuwa na muda wa kusikiliza wakati wote walikuwa wanagombea? Nakuhakikishia kama kweli Chadema wangekuwa wanataka kufanya vizuri mwaka jana kwa makundi mbalimbali wangeweza kwani hakuna jambo ambalo linapendekezwa leo halikupendekezwa wakati ule, na believe me, sidhani kama bado wanamawazo ya kubadilika - angalau CCM wamejionesha wanataka kuvua gamba. Kinachonitisha kuhusu Chadema ni kuwa when push comes to shovel, wataangushwa tena kwa sababu hawaambiliki na hata ukiwawekea idea nzuri kiasi gani mapajani mwao wengine wanafikiri unafanya hivyo kwa sababu una some ulterior motives.

Binafsi, kusema ukweli nimetambua kuwa ni kupoteza muda sana kujaribu kutoa mawazo ya kuisaidia Chadema. Wengi hapa wamekuwa wakitoa mawazo kwa miaka mitano, mawazo ambayo sote tunajua kama yangefanyiwa kazi kabla ya uchaguzi Chadema ingekuwa mbali zaidi kuliko hivi ilivyo sasa. Lakini tatizo ni kuwa bado utaambiwa "tupatieni mawazo tutayafanyia kazi!".

Hivyo, hata wenye kutoa mawazo yanayotokana na mapenzi kwa Chadema wanakaa pembeni na kuangalia drama inavyochezwa. Wafanye nini kingine isipokuwa kushika tama na kusikitika?
 
Nasikia harufu ya chama kipya tanzania in like....10yrs
 
Mkandara said:
Kuhusiana na MoU, waislaam wanataka uhalali na usawa ktk huduma zinazopatikana, kwani makubaliano baina ya serikali na kanisa ilikuwa ni swala la Kikatiba....kuhakikisha mali za watu wote zilizokuwa zimetaifishwa zinarudishwa kwa wenyewe na sio kikundi kimoja cha kanisa au viongozi kuchukua mali za Umma na kuzifanya zao..Huu ni uhuni ambao Chadema wanatakiwa kuupiga vita hata kama inawahusu ktk imani zao za dini..

Mkandara,

..MOU ilisainiwa 1992 wakati Alhaji Mwinyi akiwa Raisi.

..pia Bakwata walikuwa wanashiriki kama observers wakati wa mchakato wa MOU.

..ninachojiuliza mimi ni kwanini Waislamu hawajiungi pamoja na kuandika MOU baina yao na serikali ili nao wapate kurudishiwa mali zao zilizochukuliwa na serikali?

..maadamu umesema unafahamu baadhi ya wanaharakati naomba uwaulize hili swali linalotutatiza baadhi yetu, kwamba Waislamu wanaishia kulalamika[since 1992] kwenye mihadhara bila ya wao kuandaa MOU baina yao na serikali.
 
hapana ndugu yangu unajipinga tu; kama Dr. Slaa inapaswa aondolewe kwa sababu ya dini yake ili kuwaridhisha watu wa dini nyingine basi kuna udini maana mtu anahukumiwa kwa msingi wa dini yake. Na wewe mwenyewe ulilikoroga mwanzoni uliposema bila ku-qualify kuwa "Waislam hawamtaki" na hapo ukaingiza Dini wewe mwenyewe. Sasa pendekezo lake halihusiani na uwezo wa Dr. Slaa, makosa yake, kushindwa kwake kama kiongozi wala nini; pendekezo lako linasema Dr. Slaa alikuwa padre =>jambo hilo linawatisha Waislamu => Waislamu hawaikubali Chadema = Dr. Slaa aondoke ili Waislamu waikubali Chadema!

Nisahihishe kama huo sio mlolongo wa hoja yako. Maana naweza kuwa nimekuwa too harsh kwa kumiss kitu fulani hapa.

ulianza kwa hasira kaka, nimesema swala la risk assessment, sio lazma atoke mkuu kama chama kitakuwa hakina risk
 
Mkuu wangu unafikiria kisomi sana, jaribu kufikiria kama Mtanzania aliyekosa tumaini la kupona isipokuwa kwa kwenda Loliondo, na imani hiyo imekubalika hadi viongozi wasomi wenye ma Phd..

Waislaam wengi hawana imani na Dr.Slaa kwa sababu wanaamini system nzima ya Utawala wa Tanzania inatawaliwa na kanisa...Sasa ni bora kwao kuwa na Muislaam ndani ya hilo kanisa kuliko kuwa na Mkristu tena Padre, hivyo ni jukumu la Dr.Slaa kuwahakikishia hakuna kitu kama hicho na kama kipo yeye atakikomesha..hapo tena wakiendelea kutomuamini basi wana lao jambo.. elewa tu kwamba asilimia 80 ya Watanzania ni kabuntas na shule zetu za kata tunazojisifia nazo dhidi ya madrasa..
Mkuu solution yako inaonekana ni sawa na kuweka barafu kwenye jipu lilioko kichwani,tatizo ni kwamba jipu halitakwisha bali utalihamishia sehemu nyingine ya mwili tu pengine,tena penye madhara zaidi ya hapo kichwani.
 
Mkuu maneno yako ni sawa kabisa lakini lazima ukumbuke kwamba hata sisi Chadema hatuwezi kumkubali mtu ambaye tunafikiria ni Fisadi hata kama sii fisadi na hana sababu ya yeye kujiaminisha kwetu..

Lowassa anakubalika sana huko nyanda za juu na wapo watu wengi sana wanamkubali na hawaamini kuwa ni fisadi ila tajiri kwa uwezo wake mwenyewe lakini haina maana Tanzania nzima watamkubali hivyo hata Zitto na watu wengine ndani ya Chadema kuwa Waislaam bado zipo tuhuma dhidi yao kama vile tunavyokituhumu chama kizima cha CCM pamoja na kwamba sii viongozi wote ni Mafisadi..Wapo wanaojulikana na ukaribu wa baadhi ya mafisadi kumewaweka hata wao ktk nafasi za kuogopwa.

Kibaya zaidi mkubwa wangu fikirieni kama asilimia 80 ya Watanzania waliosoma shule za kata na madrasa ambao ndio kesho wapiga kura na ndio wenye wasiwasi sana kwani hawana tumaini jipya...

Mkuu Mkandara,

Nilibahatika kukaa na watu wengi wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2010, baadhi yao walikuwa ni waislamu kwa kweli niliyoyaona na kuyasikia toka kwa watu hawa ni kwamba wapo Waislamu wengi tu ambao hawaamini kabisa kama CDM ni chama cha kidini na wanaamini hizo ni propaganda chafu toka kwa CCM.

Kama ulivyosema wapo pia wale wanaomini kwamba CDM ni chama cha kidini na hata siku moja hawawezi kumpigia kura mgombea yeyote yule ambaye ni wa CDM. Mkuu Mkandara mimi naamini kabisa kwamba CDM kama itafanya mikakati ya nguvu nchi nzima hasa katika ile mikoa ambayo ina Waislamu wengi ili kuondoa hii dhana potofu kwamba CDM ni chama cha kidini basi wanaweza kabisa kufanikiwa na hatimaye kujiongezea idadi ya wapiga kura ambao ni Waislamu.
 
Nimependa, haya mapendekezo tuliyatoa sisi wengine kwa Chadema wakati ule lakini nani alikuwa na muda wa kusikiliza wakati wote walikuwa wanagombea? Nakuhakikishia kama kweli Chadema wangekuwa wanataka kufanya vizuri mwaka jana kwa makundi mbalimbali wangeweza kwani hakuna jambo ambalo linapendekezwa leo halikupendekezwa wakati ule, na believe me, sidhani kama bado wanamawazo ya kubadilika - angalau CCM wamejionesha wanataka kuvua gamba. Kinachonitisha kuhusu Chadema ni kuwa when push comes to shovel, wataangushwa tena kwa sababu hawaambiliki na hata ukiwawekea idea nzuri kiasi gani mapajani mwao wengine wanafikiri unafanya hivyo kwa sababu una some ulterior motives.

Binafsi, kusema ukweli nimetambua kuwa ni kupoteza muda sana kujaribu kutoa mawazo ya kuisaidia Chadema. Wengi hapa wamekuwa wakitoa mawazo kwa miaka mitano, mawazo ambayo sote tunajua kama yangefanyiwa kazi kabla ya uchaguzi Chadema ingekuwa mbali zaidi kuliko hivi ilivyo sasa. Lakini tatizo ni kuwa bado utaambiwa "tupatieni mawazo tutayafanyia kazi!".

Hivyo, hata wenye kutoa mawazo yanayotokana na mapenzi kwa Chadema wanakaa pembeni na kuangalia drama inavyochezwa. Wafanye nini kingine isipokuwa kushika tama na kusikitika?

Wafanye hivi hivi wanachofanya -- wala wasifanye kitu kingine. Mimi nadhani kufanya midahalo na Waisilamu kwa ajili ya kupata wafuasi si kitu muafaka -- kwani kuna watakaosema kuwa wanawafuata Waisilamu kwa nguvu. nafikiri Waisilamu kama wataipenda CDM waipende hivyo hivyo ilivyo na u-Padre wa Dr Slaa -- kama vile Waisilamu wengi walivyoingia CDM na kumpigia kura Dr Slaa. Hawa walivutiwa na sera za CDM, na siyo masuala ya udini.

CDM wakifanikiwa kuchota wafuasi wengi hivi hivi ilivyo, basi itakuwa imebomoa hisia moja kubwa ya udini dhidi yake. Upadre wa Dr Slaa unatakiwa usiwe issue kabisa kwa mtu kuipenda CDM -- na ikiruhusiwa kuwa issue -- basi huo ni udini.



 
SIJASEMA SEHEMU CDM INA GAMBA!! CDM haina tatizo lolote ila lisiasa kuna wakati huwa haueleweki unavyotaka ueleweke! nimetoa mifani ya salim na zuma, still you guys purposely mna -digress hoja!!

nwaonea huruma sijaona hoja , waislamu hawawatki BADALA YA KUWAAMBIA VIONGOZI WENU WAPIGANE NA HIYO HALI, MNABAKI KUTUMATUMA VIPOST VYA KISHABIKI..UJINGA HUO

HOJA ni kuwa CDM ifanye nini kujikwamua na hali hii kama mnaona is ok tuendelee!
Wabe weewe ni Mjinga mwili Mzima na umeshidwa kuwakilisha Hoja yako, ni vizuri ukasema nini kinachofanya Dr. Slaa aonekane Kuwa ni Mdini, amefanya nini kinacho sukuma watu au Watanzaniania waichukie kwa sababu ya Udini, mfano waweza sema ilani yake ya Uchaguzi, au hapakuwa na viongozi waislamu waliogombea ubunge na udiwani waislamu nk.
Halafu wewe ni nani has tukizingatia kuwa wewe ni CCM ambaye hupendi kuona CDM ikifa ilininyi Mwaka 2015 mshinde kwa ulaini. Ninachotaka kukuambia kama HAtua za CCM kujivua Gamba kama zitaenelea hadi serikalini basi itakuwa ni changamoto kubwa kwa CDM kwenye uchaguzi wa 2015 ingawa haimaanishi kuwa CDm haitashinda kama KAtiba ikitengenzwa vema.

PipoooS!!!!!!!
 
it was not a good idea kumsimamisha kugombea urais slaa?? ni watu wachache sana Tanzania hii unaweza kuwauliza swali kama hilo
wakakujibu YES. Binafisi ninasema kusimashwa kwa slaa it was the BEST IDEA EVER toka kuanzishwa kwa chama hiki na sababu ni hizi hapa
1.kutoka kura 700,000 za urais mpaka kura 2.5 million that is a success.
2.kutoka wabunge watano mpaka wabunge 47 that is a success.
3.kwa upande wa madiwani sina hakika na idadi labda wachambuzi wengine wanaweza kunisaidia ktk hili lakini i beleive wanaweza kuwa wameongezeka mara kumi ya kuliko waliokuwa nao hapo awali.
4. halmashauri kutoka moja mpaka halmashauri kumi nchi nzima that is a BIG success.
5.wanachama kutoka mamia mpaka milioni plus.
6. ruzuku kutoka milioni 40 mpaka milioni 200 kwa mwezi that is called success. ili uweze kujiimarisha.

bado tu unafikiria kuwa kumsimamisha slaa was a mistake ingawaje ktk maelezo yako umeibuwa issue ya dini lakini umeshindwa kutoa
hoja za kusupport point yako kama kawaida yenu empty skeleton we used to call them.

Thanx once again Mr. Politiki!
Umeongea vema kuhusiana na hii thread ya Waberoya. Huyu jamaa ukisoma thread yake ni pro-Chama Cha Mafisadi kwa 100 pc.
Hakuna hata sentensi moja yenye mashiko kwenye thread yake. Generally ameongea pumba na utumbo mtupu.

Madai kwamba CDM walifanya makosa ya kumsimamisha Dr. W.Slaa kugombea nafasi ya Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2010 ni ujinga na ushabiki wa CCM wa kujifanya kuwa HUONI na kumbe unaona kila kitu tena LIVE! Let me say this to Waberoya: Kwamba kama CCM wasingetumia usalama wa Taifa(UWT) WAKISAIDIANA NA Tume ya Taifa(NEC) chini ya Uwenyekiti wa kitapeli wa Lewis Makame na Mkurugenzi wake KIRAVU, sasa hivi DR. WILBROAD PETER SLAA angelikuwa Ikulu kama RAIS WA JMT.



Hilo liko wazi hata JK anajua hilo. Kukuhakikishia kuwa JK anajua hilo angalia mtiririko wa matukio ya CCM katika kutapatapata,hofu na kubabaika kwa JK kama M/Kiti wa CCM. Matukio yafuatayo yanadhihirisha:
  1. JK kurukia hoja ya KATIBA MPYA na kuifanya kama vile ni ajenda ya CCM wakti ni wazi kwamba iliibuliwa na CDM.
  2. JK kuingiza na kung'ang'ania hoja ya UDINI kuwa imesababishwa na CDM wakti JK anajua ni uongo wa mchana kweupe.
  3. JK kutangaza kuwa CCM LAZIMA WAJIVUE GAMBA ili kuendana na vishindo vya CHADEMA. Beiieve me or Not swala la kujivua gamba kwa CCM limekuja baada ya kuona joto la kisiasa linalosababishwa na CDM linawazidi CCM. Kama wanavosema wenyewe CCM kuwa haijatokea katika historia ya Chama chao kwa hawa jamaa KUJIUZULU KWA SEKRETARIETI NZIMA YA CHAMA. Imebidi wafanye hivyo katika kujaribu KUKABILIANA NA NGUVU KUBWA YA CHADEMA.
  4. CCM kuchakachua matokeo ya Umeya Jiji la Arusha ni moja ya dalili za CCM kuzidiwa na CDM.
  5. Ziara ya Viongozi wa CDM Kanda ya Ziwa kuwafanya CCM wababaike na wenyewe kwenda maeneo hayo tena kujaribu kufuta nyayo za CDM bila mafanikio. Tumesikia Pinda akilazimisha sukari IUZWE kwa Tshs.1700/=badala ya Tshs.2000/= waliyoikuta CDM kule Bukoba na maeneo mengine. Mpaka sasa hakuna mabadiliko ya Bei hiyo hata baada ya Pinda kutoa maagizo yasiyo na nguvu ya hoja baali ubabaishaji mtupu.
Yako mengi sana yanayo dhihirisha kuwa kwa sasa CCM maji ya yamezidi unga. Napenda kumthibitishia Waberoya kuwa kujivua GAMBA KWA CCM wala hakutawasaidia asilan. Tunajua wamebadilisha safu ya uongozi kama kiini macho tu lakini wao watabakia ni CCM hao hao wachovu ambao wameshapoteza mvuto kwa Watanzania walio wengi.

Ukiangalia hii safu yao hakuna mabadiliko ya kutisha. Sura mpya au ngeni hasa kwa maaana ya VIJANA ni mbili tu;ni Nnape na Januari tu. The rest of them ni walewale VIJIBABU VILIVOCHOKA AMBAVYO KAMWE HAVITAWEZA KUHIMILI VISHINDO VYA CHADEMA na mgogoro wa NDANI KWA NDANI k.m.UVCCM against vigogo kama kina Sumaye,Lowassa,Rostam,Chenge,n.k! What do you expect from Mukama,Chiligati,Vuai Ali Vuai n.k.

Moto unaochemka ndani na nje ya CCM hautazimwa kwa mbwembwe za KUJIUZULU SEKRETARIATI NZIMA. It won't help. Mimi naona hawa jamaa ni kama wameongeza PETROLI kwenye moto ambao tayari unawaka ndani ya Chama.



 
Wafanye hivi hivi wanachofanya -- wala wasifanye kitu kingine. Mimi nadhani kufanya midahalo na Waisilamu kwa ajili ya kupata wafuasi si kitu muafaka -- kwani kuna watakaosema kuwa wanawafuata Waisilamu kwa nguvu. nafikiri Waisilamu kama wataipenda CDM waipende hivyo hivyo ilivyo na u-Padre wa Dr Slaa -- kama vile Waisilamu wengi walivyoingia CDM na kumpigia kura Dr Slaa. Hawa walivutiwa na sera za CDM, na siyo masuala ya udini.

CDM wakifanikiwa kuchota wafuasi wengi hivi hivi ilivyo, basi itakuwa imebomoa hisia moja kubwa ya udini dhidi yake. Upadre wa Dr Slaa unatakiwa usiwe issue kabisa kwa mtu kuipenda CDM -- na ikiruhusiwa kuwa issue -- basi huo ni udini.





Penye red:

Hapo nakuunga mkono 100%. Hizi fikra za kuogopa kuungwa mkono kwa sababu uko dini fulani na hivyo wale wenye dini nyingine hawatakuunga mkono ni jambo la kipuuzi sana. kama ni hivyo -- basi wote tungekuwa dini moja. Nashangaa kwa nini thread hii imeddxumu muda mrefu bila kuondolewa na Mods -- inachochea udini.

Hata hivyo nimefurahishwa na kipondo alichokipata mwanzishaji wa thread kutoka kwa wachangiaji wengi.
 
always a chameleon .....

take a new non thanks ... groan from me


  • The Following User Groaned At Waberoya For This Awful Post:

    LAT (Today)​


 
Mimi ni Muisilamu lakini siyumbishwi kabisa na masuala ya dini katika siasa. Nilimpigia kura Dr Slaa kwa sababu ya msimamo wake kuhusu masuala mengi -- hususan ufisadi. Nampenda pamoja na upadre wake -- na bila shaka kuna wengi wapo kama mimi.

Nakumbuka wakati wa kampeni ya CDM kule Nzega niliona baraghashia nyingi sana among the crowds. Nilifurahishwa sana.
 
Najiuliza maswali mengi kuhusu huyu mtu maana post anazoanzisha hapa JF ni za kitoto, mfano anaposifia eti CCM sasa imejivua magamba nashindwa kuelewa ana maana gani,

Kwa kawaida Nyoka watu wanamwogopa kwa sababu ya Sumu na wala si magamba, kwanza wengi wetu humu hatufahamu kama nyoka huwa anavua magamba na ni wakati gani, kinachoshangaza zaidi ni kuamini eti Makamba senior akitoka na kuingia makamba junior eti CCM imefanya mabadiliko yatakayowafanya watanzania waiamini si kweli hata kidogo labda kina Waberoya ambao hatuwaelewi wako chama gani.

Nashangaa kuona Waberoya, TBC, Clause FM na baadhi ya magazeti ya mafisadi kuanza kushabikia, oh CCM imevua magamba sasa ni muda wananchi kurudisha imani, kumbe ni nyoka yule yule ambayewauma wengi na anaendelea kuuma wengi.

Kinachoshangaza ni baadhi ya Vyombo vya habari kuanza propaganda za kuwahadaa wananchi eti CCM imeweka sura mpya ni zipi? hii ya kina makamba junior huu ni usanii kwa waTZ.

Cha kushangaza zaidi ni kuona mtu anayeitwa Waberoya anasahau mwaka jana wakati wa kampeni Dk, Slaa ndiye aliyesema CCM ichukue hatua kwa kumfukuza Makamba. Leo miezi mitano baadaye anaondolewa anakuja na kusema CDM nayo imwondoe Dr. Slaa kwa sababu gani, Ukweli ni kwamba hakuna mtanzania wa kawaida mwenye tatizo na Dr. Slaa wawe waislamu, wakristo au wapagani ila Mafisadi wa nchi hii ndio wana chuki binafsi na huyu mzalendo na mchukia ufisadi.

Mimi nafikiri umefika muda wa akina Waberoya kuacha kushabikia mambo yenye maslahi ya mafisadi na kusimama kwa dhati na kuwatetea wananchi.

Ahsnteni.

Peoples Power
 
Mkandara,

..MOU ilisainiwa 1992 wakati Alhaji Mwinyi akiwa Raisi.

..pia Bakwata walikuwa wanashiriki kama observers wakati wa mchakato wa MOU.

..ninachojiuliza mimi ni kwanini Waislamu hawajiungi pamoja na kuandika MOU baina yao na serikali ili nao wapate kurudishiwa mali zao zilizochukuliwa na serikali?

..maadamu umesema unafahamu baadhi ya wanaharakati naomba uwaulize hili swali linalotutatiza baadhi yetu, kwamba Waislamu wanaishia kulalamika[since 1992] kwenye mihadhara bila ya wao kuandaa MOU baina yao na serikali.


Mkuu thats what we are saying here.

Harafu kwa nini waislamu wajione special na victims wa system katika nchi hii wakati wao ndo wameshika mpini? Kuna wanaosema hiyo MoU alisaini mwinyi...kwani Mwinyi ni Msabato? Au maaskofu walimshika at gun point?

My point is, ndugu zangu waislamu waache kujifanya wao ni victim wa circumstances wakati watanzania wote tunaumia na ufisadi wa CCM. Umeme ukikosekana ni kwetu sote, hizi foleni za kila siku humu...kuna wakristu wanapita barabara special?? umasikini huu unaowakimbiza watanzania unaangalia dini ya mtu?? ..kwa nini leo watake special treatment? Kwamba eti leo waislamu wanaonewa wakati Mkuu wa nchi na makamu wake na viongozi wengine wakubwa ni waislamu. It doesnt wash! Mimi narudia kusema hivi....... Wanaotaka kupigania taifa letu tuungane tupiganie hili taifa litoe fursa sawa kwa wote. Kwa wale ambao hamtaki mpaka mpewe affirmative action. Basi kaeni kimya sisi tutahangaike. Tukifanikiwa tutakula wote matunda. Tukishindwa basi wengine wataendeleza. Maana sasa imekuwa tabu watu tunashindwa kujadili issue za muhimu humu Tanzania na kujenga picha as if Masanja is better off kuliko Mohamed! Which is not true.

watu wanakuwa bigots tuu. Baadhi ya viongozi wa kiislam wanamchukia Slaa simply because ni mkristo na aliwahi kuwa Padri. Na naamini kabisa hii sumu inamwaga na watu wachache wenye maslahi yao. Majority ya waislamu wanahangaika kujitafutia mkate wa kila siku na namna ya kusaidia familia zao just like any other Tanzanian.

Kama kuna Muislamu alishawahi kuomba admission shule ya kanisa akanyimwa kwa sababu ya dini yake ajitokeze. Nitamchangia tupeleke kesi mahakamani. I dare any! Hii tabia ya ulalamishi ni ya watu waliofilisika kimawazo. Tuchape kazi tulijenge taifa tuache hizi longo longo la kujiona victims wa system. Hela wanayoiba mafisadi ingesaidia watanzania wote kupata huduma. Na usidanganyike.........usipohangaika..usitegemee kwamba Kikwete atakosa usingizi kwa sababu waislamu/wasabato au walutheri wanataka msaada wake. Never! The best he can think is his family and how to get more for himself.
 
Stein
unamjua Tambalizeni?
Anapanda jukwaani anaghani beti za mashairi ya mipasho then akishuka anasaini petty cash yake...some sort of
 
Back
Top Bottom