Ripoti ya Mtandao wa Sekta Bunifu Tanzania (CINT) imeonesha COSOTA waliipa JKT kazi ya kukusanya Mirabaha ya kazi za Sanaa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,810
11,979
Taasisi ya CINT inayofanya kazi ya Utetezi, Uzengezi na Uwezeshaji, Kuwaunganisha Wasanii na Taasisi zao na Kuzungumza kwa niaba ya Sekta ya Ubunifu Tanzania katika maeneo ya Sera, Fedha, Sheria, Elimu, Miundombinu na Teknolojia imezindua Ripoti ya Wadau wa Sekta ya Sanaa Tanzania ambapo katika mwaka 2022 Ripoti imeonesha ongezeko la Ukuaji na Uzalishaji wa kazi za Sanaa kwa 19.4% licha ya Sekta hii kutotambulika Rasmi kama mchangiaji muhimu wa Pato la Taifa.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Ripoti, Mkurugenzi Mtendaji wa CINT, Robert Mwampembwa amesema kutokana na Kutotambuliwa kwa Sekta ya Sanaa, uchangiaji wake kwenye Pato la Taifa (GDP) bado unaonekana kuwa mdogo kwa kaisi cha 1%, kwa mujibu wa Bajeti za Fedha za Miaka 10 iliyopita.

Tafiti zilizofanywa mwaka 2007 - 2010 ulionesha kuwa kama Serikali itaitambua Rasmi Sekta ya Sanaa nchini, Uchagiaji wake kwenye pato la Taifa unafikia hadi 4.7 ya GDP iwapo marekebisho yatafanywa.

Mapungufu yalipopo kwenye Mpango wa 2 na 3 wa Serikali wa Miaka 5 (FYDP 2/FYDP 3) yanasababisha utekelezaji wa mipango ya Serikali Kibajeti kwenye eneo la Ubunifu hasa Wizara husika kujikita katika Ujenzi wa Miundombinu Mkubwa ikiwemo Viwanja vya Mpira ambayo haisaidii Sanaa ya Ubunifu ikiwemo Muziki, Uchoraji na Filamu katika maeneo ya Uzalishaji wa Sanaa, Utafiti, Mazingira Mazuri ya Biashara, Fedha, Sera, Sheria na Mabadiliko ya Teknolijia katika Sanaa.

ATHARI ZA UVIKO-19 KWENYE SEKTA YA SANAA

Ripoti ya CINT imeonesha Mwaka 2018 Waziri wa Fedha na Mipango alisema kuwa Sekta ya Sanaa na Ubunifu iliongoza kwa Ukuaji nchini na kufikia 13.7% lakini iliporomoka hadi 11.2% kuanzia mwaka 2019 kutokana na kusimamishwa kwa Shughuli zote za Sanaa na Burudani ili kudhibiti maambukizi ya Ugonjwa huo.

CINT wamesema katika Bajeti mbalimbali zilizofuat, Serikali ilitoa Ruzuku ya ya kunusuru kutetereka ikiwemo Sekta za Utalii, Usafiri wa Anga lakini Sekta ya Ubunifu iliachwa.

UKUSANYAJI NA UGAWAJI WA MIRABAHA

Kuanzia Januari 28, 2022, Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kiligawa Mirabaha yenye thamani ya Tsh. 312,290,259 kwa Wasanii 1,123 kwa ajili ya Matumizi ya Kazi 5,924 za Sanaa ya Muziki zilizokusanywa kuanzia Julai hadi Novemba 2021.

Kwa mujibu wa COOTA (Iliyokuwa COSOTA) Mirabaha hiyo ililipwa na Vituo 7 vya Redio, hata hivyo ugawaji wake ulikiuka utashi wa matakwa ya Sheria kwenye maeneo muhimu. COSOTA iliahidi kuwa kutakuwa na mgao wmingine kwa Wasanii katika mwaka 2022 lakni hakufanya malipo yoyote.

Kwa zaidi ya miaka 10 taasisi ya COSOTA imekuwa haiweki hadharani taarifa zake zaFedha kwa wadau kama Sheria inavyotaka.

Mwaka 2022 COSOTA iliwapa kazi Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kukusanya Mirabaha, taasisi ambayo haina haina uzoefu wowote, hauna uelewa wa masuala ya sanaa, teknolojia wala rasilimali za kufanya kazi husika. Matokeo yake Ukusanyaji na Ugawaji wa Mirabaha ya kazi za Sanaa umekuwa hauweleweki.

Akitolea mfano ukusanyaji wa Mapato ya Mirabaha ya Kazi za Sanaa kwa mwaka 2020/21 kwa Nchi ya Malawi yenye watu milioni 20, amesema takwimu zinaonesha nchi hiyo ilikusanya zaidi ya Tsh. Bilioni 25 kwenye sanaa lakini kwa Tanzania ambayo ina idadi ya wasanii wanaofikia Milioni 9 COSOTA ilikusanya Tsh. Milioni 312 pekee.

Tangu mwaka 2015, Makusanyo ya Mirabaha kwa Tanzania ni Tsh. Milioni 489 ambazo ziligawiwa kwa miaka ya 2019 (Tsh. Milioni 183) na Mwaka 2022 Tsh. Milioni 306 kwa wasanii wa Muziki pekee huku sanaa nyinginezo zikiwa hazina mapato yoyote ikiwemo sanaa ya Filamu.

KODI YA VIBEBEO NA VIHIFADHI KAZI ZA UBUNIFU (BLANK TAPE LEVY)

Licha ya Serikali kusikia kilio cha miaka mingi cha wadau wa sanaa kutaka ipitishwe kodi (Levy) kwenye Vifaa vinavyonasa na kusambaza kazi za sanaa ili kuwafidia wabunifu bado kanuni pendekezwa zina changamoto ambayo ingeweza kuepukika. Kifungu 6(10)(d) kinapendekeza kugawiwa kwa fedha zinazopatikana baada ya ya kutoa makato ya serikali, mfuko wa COOTA na kwamba fedha zigawiwe kwa kiasi sawa kwa collective managemnet organisations zote.
 
JKT na mambo ya fedha wapi na wapi jameni?

Wausika waende jela hata miezi mitatu tu inatosha kuziwasha data zao walizojizima.
 
Back
Top Bottom