Katibu Mkuu Yakubu asisitiza watendaji sekta ya sanaa kuwa wabunifu katika utendaji kazi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amewasisitiza watendaji na watumishi wa taasisi chini ya wizara hiyo kuwahudumia wadau wa sekta ya Utamaduni na Sanaa kwa wakati ili kuleta tija katika utendaji kazi.

Katibu Mkuu Bw. Yakubu amesema hayo Juni 20, 2023 jijini Dar es Slaaam alipofanya ziara ya kikazi katika taasisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania pamoja na Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania.

"Tuongeze ubunifu zaidi na kurasimisha wafanyabiashara wa kazi za Utamaduni na Sanaa na wasanii ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika utoaji wa huduma kwa wadau wa sekta zetu hizi" amesema Bw. Yakubu.

Ameongeza kuwa taasisi zote za Wizara zina wajibu kutekeleza vipaumbele vya Serikali ikiwemo kuongeza wigo wa wasanii kwenda kufanya kazi za Sanaa nje ya nchi na kutangaza Utamaduni na Sanaa ya Tanzania na kuongeza ubunifu katika utendaji kazi wao.

IMG-20230620-WA0025.jpg
 
Back
Top Bottom