Ripoti ya CAG 2021/2022. ATCL, NHIF, Deni la Taifa, Vyura wa Kihansi, risiti za kielektroniki, Biswalo. Vyazua Mjadala

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Leo April 06, 2023 mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali, Charles Kichere ameongea na waandishi wa habari kuhusu ripoti ya ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Miongoni mwa mambo muhimu
CAG amewashukuru waandishi wa habari, wenyeviti na makamu wenyeviti wa kamati za Bunge kwa kujimuika katika uwasilishaji wa taarifa hiyo. CAG amesema aliwasilisha ripoti ya ukaguzi kwa Rais kwa mujibu wa katiba na leo zimewasilishwa Bungeni hivyo kuzifanya kuwa nyaraka zinazoweza kusambazwa kwa umma. Leo anatoa taarifa ya yaliyomo kwa ufupi.

Ripoti 22
CAG amesema aliwasilisha kwa Rais jumla ya ripoti 22 zikijumuisha mambo mambo mbalimbali kwa taasisi zilizokaguliwa na CAG miongoni zikiwemo ripoti ya Serikali kuu, TAMISEMI, mashirika ya umma, miradi ya maendeleo na nyinginezo.

Hati 1010 kati ya 1045 zinaridhisha(96.6%)
CAG ametoa jumla ya hati 1045 kwa mwaka wa fedha 2021/22. Katika hizo, hati zinazoridhisha ni hati 1010 sawa na asilimia 96.6, hati zenye shaka ni 29(2.78%) na hati mbaya ni 3(0.29%) na hati tatu zilizoshindikana kutoa maoni.

Malipo ya Bilioni 25.95 hayana risiti za kielektroniki
CAG ameona malipo bila kuomba risiti za kielekroniki ya Bilioni 25.95 kwenye maeneo mbalimbali ndani ya Serikali, CAG amesema inadhohofisha juhudi za Serikali katika kukusanya kodi, wafanyabiashara wanaweza kutumia mwanya huu kukwepa kodi.

CAG amerejea ushauri wa awali wa maafisa masuuli wanapaswa kufanya shughuli na wafanyabiashara ambao wana mashine za risiti na kudai risiti za kielektroniki kwa mujibu wa sheria za kodi.

Ucheleweshaji malipo umesababisha riba ya bilioni 418.77
CAG amesema alibaini ucheleweshaji wa malipo na kuzaa riba ya bilioni 418.77 katika taasisi mbalimbali za Serikali. CAG amesema haya ni malipo yasiyo na tija na kuiingiza Serikali hasara. Sababu za ucheleweshaji inajumuisha mchakato wa malipo kuchukua muda mrefu bila kuzingatia mkataba.

Dawa za bilioni 3.5 muda wa matumizi ulikwisha bila kutumika
CAG alibaini baada ya kukagua rejesta katika hospitali dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya bilioni 3.5, hatari yake kuangukia kwa watu wasio waaminifu.

Pia bohari kuu ya dawa ina dawa zenye thamani ya milioni 235.84 zilizokwisha muda wake kabla ya kusambazwa.

Magari yenye thamani ya bilioni 35.29 hayajapokelewa
Magari yenye thamani ya bilioni 35.29 yaliyonunuliwa kupitia wakala wa huduma wa ununuzi Serikalini yalikuwa hayajapokelewa mpaka mwezi wa 12 wakati wanamalizia ukaguzi.

Mfuko wa wanawake, vijana na wenye ulemavu - Bilioni 88. 4 hazijakusanywa
Mfuko wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, mamlaka 180 za Serikali za mitaa zimeshindwa kukusanya bilioni 88.42 za mikopo iliyotolewa kutokana na kukosekana ujuzi, udhaifu kwenye upembuzi, udhaifu katika ufuatiliaji wa mikopo.

Mifumo ya usalama na utambuzi wa moto haifanyi kazi Uwanja wa Mkapa
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (#CAG), Charles Kichere amesema “Nimebaini mapungufu kadhaa kuhusiana na utendaji wa Uwanja wa Mkapa, ambayo yanahitaji usimamizi makini.”

Ameongeza “Nimebaini miundombinu na vifaa duni, viti vimevunjika na havijarekebishwa, hali isiyoridhisha kuhusu miundombinu ya choo, hii inaweza kuleta athari za kiafya kwa watumiaji na kuathiri mapato."

Amesema “Viyoyozi hazifanyi kazi vizuri, usambazaji wa maji na mfumo wa usafi haufanyi kazi kwa njia inayoridhisha, mifumo ya usalama haifanyikazi kama wa utambuzi wa moto na wa tahadhari haifanyi kazi.”



 

Attachments

  • Ripoti_Kuu_ya_Ukaguzi_ya_Serikali_Kuu_(MDA)_Mwaka_2021-22.pdf
    32.7 MB · Views: 6
  • Ripoti_Kuu_ya_Ukaguzi_wa_Miradi_ya_Maendeleo_Mwaka_2021-22.pdf
    30.2 MB · Views: 7
Mbona arudia tena kusoma ripoti ileile?

Alipaswa kujiandaa kuja kujibu masuali mbalimbali ya waandishi na wapashaji habari.

Waandishi na wapashaji habari walipaswa kuja na masuali ambayo yametokana na kuchambua ripoti hiyo.

Hii nchi ngumu hii.
 
Ok, kazi yake alishaifanya na kuimaliza, tatizo linabaki ngazi za juu..
 
Mbona arudia tena kusoma ripoti ileile?

Alipaswa kujiandaa kuja kujibu masuali mbalimbali ya waandishi na wapashaji habari.

Waandishi na wapashaji habari walipaswa kuja na masuali ambayo yametokana na kuchambua ripoti hiyo.

Hii nchi ngumu hii.
Hao waandishi na wahariri mandazi wamenunuliwa na msoga gang
 
Hatimae kichaka cha hayati Magufuli kimeisha sasa wizi wao ,ufisadi wao ,uongo wao ,unafiki wao upo hadharani sasa.
Huyu jiwe kachafuka mpk kaburini anakoipata sulubu ya moto wa milele. CAG endelea kuigalalagaza legacy
 
Hao waandishi na wahariri mandazi wamenunuliwa na msoga gang
Nchi yetu ina waandishi mahiri wa habari wachache sana, yaani top class na Jenerali Uliomwengu aongoza kundi hili.

Pia nchi yetu ina waandishi wa habari ambao ni mchanganyiko wa umahiri na uhuni na ndo hao unowasema wamenunuliwa na ndo huitwa "chequebook journalists" hawa wapowapo tu mara hapa mara pale.

Kisha kuna wale wapashaji habari ambao ndo wengi wao wana vibuyu vya asali.
 
Kila sehemu ni wizi tu.

Hata polisi yule inspector wa polisi kakimbia na milioni 700 hadi leo hajapatikana.

Yaani wakimbia yatangazwa umekimbia kisha usiku warudi kisha zile 700m zagawiwa na kesi closed.
Kodi za Watanzania zinaibiwa sana na zinazobakia zinatumiwa vibaya.
 
Mbona arudia tena kusoma ripoti ileile?

Alipaswa kujiandaa kuja kujibu masuali mbalimbali ya waandishi na wapashaji habari.

Waandishi na wapashaji habari walipaswa kuja na masuali ambayo yametokana na kuchambua ripoti hiyo.

Hii nchi ngumu hii.
Waandishi wapi? Nchi hii ina waandishi wa maana kwa sasa? Angalia hapo yamekaa tu yanapiga story na kusubiri bahasha za kaki baas!
 
Back
Top Bottom