Ridhiwani Kikwete: Serikali kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuibua miradi ya tasaf itakayoondoa changamoto zilizopo

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Serikali imesema miradi yote inayotekelezwa na TASAF (Mpango wa kunusuru kaya maskini) huibuliwa na jamii kwa kutumia utaratibu shirikishi unaohusisha na jamii yote na kwamba serikali itaendelea kutoa elimu kwa jamii nzima nchini kuhakikisha inaibua miradi inayotatua changamoto zao katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete wakati akijibu swali la Mbunge wa Newala Vijijini, Maimuna Mtanda aliyetaka kujua kwanini miradi iliyokubaliwa na jamii kupitia TASAF hukataliwa na kukubaliwa miradi ambayo haikukubaliwa na jamii.

"Miradi yote inayotekelezwa kupitia TASAF huibuliwa na jamii kwa kutumia utaratibu shirikishi unaokutanisha jamii yote katika kijiji, mtaa au shehia katika mkutano wa kuchagua miradi inayoondoa kero za wananchi inayokubaliwa na jamii na inayokidhi vigezo vya kisekta. Endapo jamii itaibua mradi ambao haukukidhi vigezo vya sekta na kuangalia manufaa ya miradi kwa kuangalia miradi ya kipaumbele cha kwanza katika jamii basi mradi wa pili katika orodha ya vipaumbele vya jamii hutekelezwa. Alisema Kikwete.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge Mtanda (aliyeuliziwa swali na Mbunge Tecla Ungele kwa niaba yake) aliyetaka kujua kwakua elimu ya uibuaji miradi yenye tija kwa jamii bado haijaeleweka vizuri, mkakati wa serikali ni upi kupeleka elimu kwa jamii na elimu hiyo iwe endelevu.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Kikwete amesema "Kuhusu elimu ya uibuaji miradi yenye tija ambayo haijaenea vizuri, katika utaratibu wa mikutano mikuu ya vijiji, kata au shehia ya kwenda kuibua miradi hatua ya kwanza wanayofanya wataalamu wetu ni kuendelea kuelimisha wananchi kabla hawajaibua miradi yao. Shida kubwa inatokea ni kwamba wananchi wanakua na vipaumbele vyao dhidi ya ile mipango ambayo serikali inaileta na hapo ndipo hutokea tatizo na mgongano lakini nataka nimhakikishie Mbunge aliyeuliza swali kwamba serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili wafike sehemu wanaibua miradi ambayo inaendana moja kwa moja na changamoto ambazo ziko maeneo yao kwa ajili ya utekelezaji." Alimalizia Kikwete.

IMG-20240209-WA0032.jpg
 
Back
Top Bottom