BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 310
- 403
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amesema katika mwaka huu wa fedha 2023/24, Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza Jumla ya Bilioni 51 kwa ajili ya kwenda kunufaisha Watanzania waishio katika mazingira magumu kupitia Mpango wa kuokoa Kaya Maskini wa TASAF kote nchini.
Kikwete ameyasema hayo alipotembelea wanufaika wa TASAF katika manispaa ya Singida na kujionea maendeleo makubwa ya miradi ya TASAF wakati akiwa kwenye ziara yake mkoani humo.
"Niwaombe sana Waratibu wote katika manispaa na wilaya zote za Tanzania msiende kufanya vituko katika fedha hizi maana kituko chako kitakufanya urudi kwenu ili tumtafute mtu mwingine wa kuja kuhudumia Watanzania." Alisema Kikwete.
Naibu Waziri Kikwete amesema Rais Samia ameelekeza fedha nyingi zaidi za TASAF ziende kwa wananchi ili kuboresha maisha yao na kwamba wao kama wasaidizi wake watahakikisha maelekezo aliyotoa Rais Samia kwenye matumizi ya fedha kwa kuhakikisha fedha hizi zote zinawafikia walengwa.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kikwete amesema Serikali itaendelea kuwapa nafasi wanufaika wa TASAF huku akiwahimiza kuendelea kuibua miradi ya maendeleo katika maeneo yao.
"Serikali ya Rais Samia itaendelea kuwapa nafasi, lakini kubwa nyinyi wananchi katika maeneo yenu ni muhimu kubuni miradi yenu ya maendeleo ya kutengeneza rasilimali ili adhima ya Mpango wa TASAF kuondoa umaskini uendelee kuwa wa mafanikio makubwa." Alisema
Mpango wa TASAF wa kunusuru Kaya Maskini nchini umeendelea kuzaa matunda makubwa ikiwemo kuokoa hali duni ya maisha kwa Kaya nyingi za walengwa, kuanzisha miradi ya maendeleo ya kujikwamua kiuchumi, kujenga nyumba na kuboresha makazi, kusaidia elimu kwa watoto na mengine mengi.