Ridhiwan Kikwete: Serikali kutowafumbia macho wanaofuja fedha za TASAF

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete amewaonya watumishi na waratibu wa mradi wa kuondoa umaskini (TASAF) kuhusu matumizi mabaya ya pesa za mradi na kutofuata maelekezo yaliyotolewa kusimamia mradi huo.

Serikali imeeleza haya Bungeni wakati wakijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Lulindi Ndg. Ali Mchungahela alipotaka kufahamu hatma ya wananchi wake katika mradi huu. Naibu Waziri ameelezea jinsi walivyopeleka fedha kwa ajili ya kusimamia mradi wa TASAF nchini na kwamba maelekezo yanataka wanufaika kulipwa ndani ya Muda na semina kwa ajili ya ufahamu katika ubunifu wa miradi na uwajibikaji zikifanyika ndani ya Muda, hivyo kwa serikali ni jambo la kushangaza kuwa maelekezo hayafanyiwi kazi.

Naibu Waziri Kikwete, ameeleza hayo pamoja na hatua zitakazochukuliwa kwa watumishi au waratibu wanaosimamia mradi huo kwa kuwa fedha zimekwisha pelekwa na zinapelekwa katika kila robo ya malipo ili kuelimisha na kuwezesha walengwa.

#KaziInaendelea #Bungeni
 
Mheshimiwa Ridhiwani ni bonge la kiongozi kiukweli utendaji kazi wake unaonekana,tunamshukuru Mungu kwa ajili yake kwa kweli,Kazi iendelee.Tunaona mabadiliko ya wazi kabisa.
 
Back
Top Bottom