Ridhiwani Kikwete: Serikali kutowafumbia macho wanaofuja fedha za TASAF

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
305
519
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete amewaonya watumishi na waratibu wa mradi wa kuondoa umaskini (TASAF) kuhusu matumizi mabaya ya pesa za mradi na kutofuata maelekezo yaliyotolewa kusimamia mradi huo; alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Lulindi Ndg. Ali Mchungahela alipotaka kufahamu hatma ya wananchi wake katika mradi huu.

alikuwa akijibu swali la Mheshimiwa Issa Ally mchungahela Mbunge wa Lulindi aliyetaka kujua Serikali inafanya nini kuhakikisha Miradi ya TASAF inakuwa yenye tija kwa Wanufaika.
 
Hizo ni siasa, sasaiv kila mmoja anakula kulingana na urefu wa kamba yake hakuna chochote kinachofanyika, tena sasaivi hakuna uoga kabisaaaaa!! Ukishindwa kujenga kipindi cha huyu mama basi wewe hutajenga tena!! Waliotajwa kwenye ripot ya CAG si wanaendelea kula bata! Ni hatua gani zilichukuliwa??? Waache kutudanganya tunataka katiba mpya
 
Kwenye jimbo lake kuna wazee hawalipwi hadi wafanye kazi. Kila mwezi wazee hao wanachama wa TASAF wametengewa siku 10 za kufanya kazi asubuhi hadi saa6 mchana.
Kwenye hizo siku 10 kila siku sh.3000.
 
Zifujwe mara ngapi
Hela za tasaf zinaliwa
Na wapigaji tu

Ova
 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete amewaonya watumishi na waratibu wa mradi wa kuondoa umaskini (TASAF) kuhusu matumizi mabaya ya pesa za mradi na kutofuata maelekezo yaliyotolewa kusimamia mradi huo; alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Lulindi Ndg. Ali Mchungahela alipotaka kufahamu hatma ya wananchi wake katika mradi huu.

alikuwa akijibu swali la Mheshimiwa Issa Ally mchungahela Mbunge wa Lulindi aliyetaka kujua Serikali inafanya nini kuhakikisha Miradi ya TASAF inakuwa yenye tija kwa Wanufaika.
View attachment 2904636
Haya maneno ni kama sala ya Bikira Maria kwa wakatoliki
 
Back
Top Bottom