TANZIA Rest in peace Valentina (JF Member)

Nakumbuka uncle amefariki sikufuta namba, sasa baada ya miezi minne auntie akanipigia kwa namba ya uncle alafu nilikuwa nishalala nilishtuka sana na sikupokea hadi alipotuma msg ingawa nikamtafuta kesho yake nikimdanganya kuwa nilikuwa nimelala.
Huwa ni vigumu kufuta kumbukumbu za Kifo cha mpendwa wako


Na iwapo utasalia na namba yake, ndiyo inaweza kuzidisha huzuni zaidi
 
Valentina alikua mtu aliyependa kutengeneza marafiki. Mwaka 2017 tulikutana hapa JF baadaye akaniunga kwa WhatsApp group lake ila siku interested tukabakia kuwa marafiki kwa muda wote!

Mara nyingi alikua akinialika endapo nikiwa Arusha tubadilishane mawazo ila ratiba zikawa ngumu hata niendapo Arusha

Leo ndio nimeona taarifa za msiba kutoka kwa ndugu yake. Nimejiskia vibaya sana. Nimeambiwa alifariki aliwa anajifungua ila mtoto amenusurika. Mungu awape uvumilivu familia yake,wanaJF na marafiki wote wa Valentina hapa jamvini
 
Weka picha hata ya ovatar yake sasa wasiomjua waitambue hata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…