Teko Modise
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 1,914
- 6,033
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 kuliwahi kuandaliwa shindano la wenye sura mbaya Tanzania kwa upande wa wanaume. Wanawake walikataa hivyo likaandaliwa la wanaume tu.
Washiriki walikuwa wengi lakini waliofanikiwa kufika top 3 walikuwa ni Mzee Jangala, Remmy Ongala na Masoud Sura Mbaya.
Baada ya mchuano mkali, majaji wakatoa matokeo yao. Mshindi wa kwanza akawa Masoud, wa pili Remmy na wa tatu ni Mzee Jangala.
Basi kama ilivyoada, Masoud akapewa kitita chake kama zawadi, wakati Masoud akikabidhiwa check yake, marehemu Remmy Ongala akaanzisha mzozo wa kutomtambua mshindi huku akijinadi yeye ndio alipaswa kuwa mshindi kwani sura yake ni mbaya na hakuna wa kumkaribia.
Majaji wakamshauri akate rufaa, kweli Remmy akakata rufaa lakini akashindwa na Masoud akapewa mzigo wake wa ushindi.
Ni shindano ambalo halikuwahi kujirudia tena, japo wengi walitamani linhejirudia miaka ya mbeleni. Hiyo ni miaka ya 2000 kabla ya vurugu zenu za Insta, Facebook wala TikTok.
My take:
Hivi hili shindano lingeletwa zama hizi kuna wanaume wangekubali kushiriki kweli? Hawa wanaoedit picha zao photo shoot ili zing’ae huko mitandaoni ili wajizolee “likes” za kutosha!