TANZIA: Aliyekuwa mpinzani mkuu wa Dkt. Remmy Ongala katika Shindano la Sura Mbaya enzi hizo, 'Masuod Surambaya' afariki

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,620
20,951
Amefariki leo siku ya Jumamosi, na kwa kwa mujibu wa ndugu wa marehemu atazikwa kesho katika makaburi ya Ilala Kota Mchikichini.

INNALILAHI WA .....
APUMZIKE KWA AMANI.
FB_IMG_1576387160346.jpg

Hapo kwenye picha ni Remmy Ongala(katikati) Masudy sura mbaya(kushoto) na Mzee Jangala(kulia).
IMG_1839.JPG

Kulikuwa na shindano la mtu mwenye sura mbaya kuliko wengine Tanzania na hawa ndio vinara watatu bora ambapo: -

1. Alichukua Masudy Sura Mbaya

2. Akachukua Remmy Ongala

3. Ikakamatwa na Mzee Jangala

Kilicho staajabisha watu zaidi ni pale Remmy Ongala alipolalamika saaaana kuwa ameonewa kwamba alikuwa anastahiri kuibuka mshindi wa kwanza yeye na sio Masudy. Akasema "jamani Masudy hanishindi kwa ubaya majaji mmembeba"


Masoud Sura Mbaya kama anavyojulikana sasa ni msanii ambaye alivuma miaka ya 90 baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya mwanamume mwenye sura mbaya.

Kwa mara ya kwanza alishiriki katika mashindano ya wanaume wenye sura mbaya yaliyofanyika Buguruni Dar es Salaam na kuibuka mshindi wa kwanza ambapo alipata zawadi ya redio.

Mashindano hayo ya kusisimua yalifanyika kwa mara ya pili katika Wilaya ya Kinondoni ambapo, Masoud aliwashinda wasanii wengine maarufu wakiwamo mwanamuziki wa siku nyingi Remmy Ongala na msanii maarufu wa vichekesho Khalid John, maarufu kama Mzee Jangala.

Masoud anasema anaamini kuwa hakuna mwanamume mwenye uwezo wa kumnyanganya nafasi hiyo nchini Tanzania kwa kuwa ana uwezo wa kubadilisha sura yake kwa kutumia hisia mbalimbali. Mimi ni sura mbaya nambari wani Tanzaniawa kunishinda hajapatikana.

Wapo waliojaribu kukata rufaa kupinga ushindi wangu lakini niliwashinda hata kwenye rufaanajivunia ushindi wangu na kila ninapojiangalia kwenye kioo naona wazi kuwa nina haki ya kushinda, anasema Masoud.
Zaidi soma;

 
Pumzika Masoud, sura yako ndio ulikuwa utambulishi wako! Haijalishi ulifanya mengi mabaya kama sura yako ama yalikuwa amali kwako..wewe na uliyokuwa umepitia ndio mnaojua! Pumzika kwa Amani maana sisi pia tunafuata. Naamin tuna majanga makubwa huko kuliko wewe
 
Pumzika Masoud, sura yako ndio ulikuwa utambulishi wako! Haijalishi ulifanya mengi mabaya kama sura yako ama yalikuwa amali kwako..wewe na uliyokuwa umepitia ndio mnaojua! Pumzika kwa Amani maana sisi pia tunafuata. Naamin tuna majanga makubwa huko kuliko wewe
Aisee
 
Of cause aliibuka kidedea katika shindano hilo akim'bwaga mpinzani wake Remi lakini MZEE ongala alikata rufani ya kwamba yeye ndiye alistahili kuwa Mr sura mbaya Tanzania . Siamini kama alikuwa anatetea usura mbaya ama kuikosa zawadi,,,,,,sikumbuki mshindi alituzwa nini!! Natamani mashindano haya yarudi ili tuongeze burudani zaidi .Japo nina shaka kama washiriki wenye sifa wapo.,,,,,,,,,,,Pamoja na hayo tuendeleza kuomboleza msiba wa mpendwa wetu MASOUD. Amini!!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom