Reincarnation...nazidi kupata uhakika binadamu hatufi

Sio tu haufi, au sio tu kwamba utazaliwa tena na tena, unaweza ukafa na ukabaki hapa hapa, isipokuwa mazingira yanabadilishwa kidogo tu wanakuweka kwenye ulimwengu unaofanana na ule uliokuwamo awali.

Kwanza hutajua kama umekufa, utaendelea tu huku wao wanakuchekaaaa!

Hii ni kwa wachache sana.
Hii nayo mpya
 
Kuna dini Moja ambayo wanawachukulia majini kama ndugu zao katka imani. Litakuwa Mojawapo ya jidubeadhika hilo
 
Naam hili jambo nilikuwa nalichukulia poa...lakini baada ya kuamua kufuatilia kidogo naanza kupata uthibitisho pasi kuwa na shaka juu ya mzunguko wa maisha ya viumbe sisi bin adamu.

Kwa kifupi sana tafiti ni nyingi lakini......nilipata kuishi nyanda za juu kusini mwa Tanzania nikiwa kijana mdogo miaka mingi sana iliyopita.

Nilikuwa nina rafiki yangu Mbulushi...rafiki yangu huyu kwa bahati mbaya alifariki.

Siku ya siku sina hili wala lile nikiwa katika nchi ya mbali sana nikakutana na kijana mmoja amefanana na yule rafiki yangu kwa zaidi ya asilimia 90%...nikabaki namshangaa...kitu cha ajabu na yeye kama alikuwa ananishangaa...nikamuuliza ulishawahi kuishi.

Tanzania...akasema hapana hata Neno Tanzania ndio leo analisikia.
Ajabu zaidi anasisitiza kwamba ananifahamu lakini hakumbuki ni wapi tulisha wahi kuonana
Mahali ambapo nilipata mshituko niliona alama katika mkono wake wa kulia sawasawa na yule rafiki yangu,,,(alama hii naikumbuka kwa sababu alianguka na baiskeli akachanika na kushonwa katika hospitali ya Aga khan)....sasa huyu jamaa anasema hiyo alama amezaliwa nayo hivyohivyo.

Nikijaribu kumuuliza yeye asili yake ni wapi anasema ni Afganistan na hana ndugu wala jamaa Afrika.

Kwa kifupi sana 1.Sauti yake 2.Ongea yake 3.Namna anavyotembea ni yule marehemu kabisa kabisa.

Yule Marehemu leo angekuwa na miaka kama 70 hivi na huyu niliyekutana nae yuko kwenye miaka ya 30 katikati.
Wewe Una miaka mingapi?
Naona tunaendana
 
Uwe mtu mzima Sasa na wewe mkuu 🤣
Ukitenda mabaya na ukafa hiyo imeisha, habari za kusema Kuna siku eti utatolewa kabulini ulipwe Kwa uliyotenda hizo ni hadithi tu.
Malipo ni hapa hapa Duniani, ukifa haujapata malipo Yako basi imeisha hiyo
Na wataksokufa kwa wema pia inakuwaje kwa upande wao
 
1st ujue kuwa umeletwa duniani kwa malengo gani, ukishayajua basi hayo ndio maandalizi yenyewe, ni rahisi tu Google tumeumbwa kwaajili gani?! utapata majibu, kila la kheri.
Hakuna sababu yoyote ya sisi kuletwa duniani. Sisi wote ni matokeo ya binadamu wawili kujamiiana, na kisha tukazaliwa kupitia mwili wa mwanamke. It's just nature, hakuna malengo yoyote yale ya sisi kuwepo hapa
Na hakuna namna yoyote ya kujiandaa na kifo
 
Basi tusubiri majibu kila mmoja atayapata kwa wakati wake.
 
Hiyo haina haja ya kuandika ila maisha yote ni kama ndoto , kwa vile hatuwezi kurudi nyuma basi tunaishi katika nadharia ila sote tunapita...Nikiangalia picha ya Graduation ya jamaa nilisoma naye Advance mpaka chuo.

Huyu jamaa alikuwa talkative sana ila alikufa kwa ajali ,yaani nikizidi kuangalia nahisi mpaka sauti yake kama yupo yaani.
 
Naam hili jambo nilikuwa nalichukulia poa...lakini baada ya kuamua kufuatilia kidogo naanza kupata uthibitisho pasi kuwa na shaka juu ya mzunguko wa maisha ya viumbe sisi bin adamu.

Kwa kifupi sana tafiti ni nyingi lakini......nilipata kuishi nyanda za juu kusini mwa Tanzania nikiwa kijana mdogo miaka mingi sana iliyopita.

Nilikuwa nina rafiki yangu Mbulushi...rafiki yangu huyu kwa bahati mbaya alifariki.

Siku ya siku sina hili wala lile nikiwa katika nchi ya mbali sana nikakutana na kijana mmoja amefanana na yule rafiki yangu kwa zaidi ya asilimia 90%...nikabaki namshangaa...kitu cha ajabu na yeye kama alikuwa ananishangaa...nikamuuliza ulishawahi kuishi.

Tanzania...akasema hapana hata Neno Tanzania ndio leo analisikia.
Ajabu zaidi anasisitiza kwamba ananifahamu lakini hakumbuki ni wapi tulisha wahi kuonana
Mahali ambapo nilipata mshituko niliona alama katika mkono wake wa kulia sawasawa na yule rafiki yangu,,,(alama hii naikumbuka kwa sababu alianguka na baiskeli akachanika na kushonwa katika hospitali ya Aga khan)....sasa huyu jamaa anasema hiyo alama amezaliwa nayo hivyohivyo.

Nikijaribu kumuuliza yeye asili yake ni wapi anasema ni Afganistan na hana ndugu wala jamaa Afrika.

Kwa kifupi sana 1.Sauti yake 2.Ongea yake 3.Namna anavyotembea ni yule marehemu kabisa kabisa.

Yule Marehemu leo angekuwa na miaka kama 70 hivi na huyu niliyekutana nae yuko kwenye miaka ya 30 katikati.
Binafsi naona kama unajichanganya wewe mwenyewe mkuu. Reincarnation maana ake ni kuzaliwa mara ya pili na ili kitu kizaliwe maya ya pili lazima kife, sasa unaposema kuwa binafamu "HATUFI" huku ukilinganisha na REICARNATION naona it's a confusion. In between your supportive lines umesema kuwa huyo rafiki yako kwasasa angekuwa na it's na huyo muafghanistan ni 30's, sasa huoni mada yako na kichwa cha habari haviendani?
Nadhani labda kama ungesema kuwa binadamu tukifa unaamini tunazaliwa mahali pengine kabisa tofauti na ulipokuwa mara ya kwanza huku fahamu za kwanza zikiwa zimefutwa kabisa. This will make a certain kind of sense.
Karibu....
 
Back
Top Bottom