Reincarnation...nazidi kupata uhakika binadamu hatufi

Reincarnation...nazidi kupata uhakika binadamu hatufi

nzalendo

Ukishaondoka duniani haurudi tena mkuu utabakia kwenye kizuizi kaburini mpaka siku ya kufufuliwa kwaajili ya kulipwa wema kwa wema na ubaya kwa ubaya, najua ni mtu mzima sasa, punguza haya matumaini na ujiandae na mauti yako.
Uwe mtu mzima Sasa na wewe mkuu 🤣
Ukitenda mabaya na ukafa hiyo imeisha, habari za kusema Kuna siku eti utatolewa kabulini ulipwe Kwa uliyotenda hizo ni hadithi tu.
Malipo ni hapa hapa Duniani, ukifa haujapata malipo Yako basi imeisha hiyo
 
, je huu ulimwengu wa sasa hauwi ndio ndoto
Hii inaweza kuwa, ila nani yupo kwenye ndoto ya mwezake ? Sisi ndio tupo kwenye ndoto yako au wewe ndio upo kwenye ndoto ya mmoja wetu humu, au wote tunaota ndoto moja kwa pamoja
 
Uwe mtu mzima Sasa na wewe mkuu 🤣
Ukitenda mabaya na ukafa hiyo imeisha, habari za kusema Kuna siku eti utatolewa kabulini ulipwe Kwa uliyotenda hizo ni hadithi tu.
Malipo ni hapa hapa Duniani, ukifa haujapata malipo Yako basi imeisha hiyo
Ila tunajuaje kama hapa ndio mwisho, kwa kuwa hajawahi kurudi mtu na kutuonyesha, mi nahisi unapaswa kuweka possibility kwamba huenda kuna ulimwengu mwingine, mfano kuna jamii imejitenga na dunia hawajui nini kinaendelea hawajui mambo ya mawasiliano ya internet hawajui kuna Artificial intelligence, hivyo kwao wao wanavyoona ndio uhalisia wao ila sio uhalisia wote kwa ujumla, hawajui kuwa kuna dunia nyingine tofauti kabisa na wanayoijua
 
Mbona unakataa halafu unakubali
Unasema kuwa dhana ya ukifa hauendi popote ni uongo, halafu tena maelezo yako yanaonesha unakubali kuwa ukifa hauendi popote, maana yake unapotea mazima
Dhana ya ukifa hauendi popote ni uongo kwakuwa 'wewe' haupo.

'Wewe' ni kitu ambacho kipo sasaivi tu. Hata usipokufa lakini baadae hiyo unayoiita 'mimi' saivi haitakuwepo.

'Wewe' ni kitu ambacho kipo kwenye wakati uliopo basi. Hivo kusema hiyo wewe kuna sehemu itaenda au haitaenda ukifa ni kosa la kimaantiki.
 
Hii inaweza kuwa, ila nani yupo kwenye ndoto ya mwezake ? Sisi ndio tupo kwenye ndoto yako au wewe ndio upo kwenye ndoto ya mmoja wetu humu, au wote tunaota ndoto moja kwa pamoja
Ni swali zuri ila kwa ujuzi wangu ni refu sana kama hujui chochote kuhusu consciousness(ufahamu)/Spirit, mwili na nafsi(soul).
Jibu rahisi kwa uelewa wangu mdogo sana ni kwamba tunaexist in different dimentions at same time. Kwamba muda huu ulimwengu wa ndoto bado unaendelea na wewe na mimi tuko huko pia ila ufahamu wetu upo hapa kwenye cafe na keyboard zetu mf.
Kinachohama ni ufahamu na sio mwili na kwenye ndoto kuna dimention tofauti kulingana na state uliyonayo ndani...mfano hasira, furaha nk. ila pia kumaster jinsi ya kuingia kwenye state fulani ukiwa na ufahamu(ndani ya ndoto) ndio kitu kikubwa kinachotofautisha mtu wa kawaida na mchawi...wao wanaweza wakapanga hadi kukutana kwenye ndoto na wakakutana na wakafanya wanayofanya na wakarudi kuamka wakiwa kila mmoja anajua walifanya nini..
Kwenye kila tunachokijua kuna watu wanajua zaidi na wengi wamefanya ni siri yao na kuongea baadhi ya siri ni lazima uuliwe nk ila ofisini unapofanya kazi kuna mtu anakaa kwenye kiti anaingia astral plane(tuseme ulimwengu wa ndoto ili iwe rahisi), then anakutana na wewe kwenye huo ulimwengu ukiwa hujui chochote(haupo conscious) kwa sababu hauko initiated, than anakupaka mavi nk wakati wewe upo kwenye pc yako unajua mshikaji ana mawazo sana au amepitiwa na usingizi then in physical world mambo coincedences yanaanza kutokea ambayo sio positive kwako...
Fanya research yako, kaa na wazee usiwapuuze, usikubali kupigwa chale na usiamini nilichoandika
 
Dhana ya ukifa hauendi popote ni uongo kwakuwa 'wewe' haupo.

'Wewe' ni kitu ambacho kipo sasaivi tu. Hata usipokufa lakini baadae hiyo unayoiita 'mimi' saivi haitakuwepo.

'Wewe' ni kitu ambacho kipo kwenye wakati uliopo basi. Hivo kusema hiyo wewe kuna sehemu itaenda au haitaenda ukifa ni kosa la kimaantiki.
Sasa si ndo maana yake hiyo, kwamba ukifa unapotea mazima
Hiyo "wewe" itaondokaje yenyewe bila kupotea, lazima ufe kwanza.
Mwanzo kabisa nilisema ukifa unapotea mazima, maana yake hauendi popote, you just disappear
Na ni sahihi kwa sababu kitu ambacho hakipo yani kimekuwa disappeared hakiwezi kwenda kokote, kwa sababu hakipo in existence.
Naona unacomplicate tu ila nilichosema ndio hichohicho unachokisema. Zaidi unaweka tu more clarification, na si kupinga
 
Hivi kabla hatujazaliwa tulikuwaga wapi?
Mfano mimi nimezaliwa 1/1/1990, je December ya 1989 nilikuwa wapi?
Je inawezekana tukifa tunarudi kule tulikokuwa kabla ya kuzaliwa?
Kabla ya kuzaliwa hatukuwa na ufahamu wowote, inawezekana na tukifa tunakuwa hatuna ufahamu wowote kama tilivyokuwa kabla.ya kuzaliwa?
Na hapa tunachoongelea kwamba kina incarnate ni nafsi au roho? Navitofautishaje hivyo viwili?
Very confusing stuff 😆
 
Hivi kabla hatujazaliwa tulikuwaga wapi?
Mfano mimi nimezaliwa 1/1/1990, je December ya 1989 nilikuwa wapi?
Je inawezekana tukifa tunarudi kule tulikokuwa kabla ya kuzaliwa?
Kabla ya kuzaliwa hatukuwa na ufahamu wowote, inawezekana na tukifa tunakuwa hatuna ufahamu wowote kama tilivyokuwa kabla.ya kuzaliwa?
Na hapa tunachoongelea kwamba kina incarnate ni nafsi au roho? Navitofautishaje hivyo viwili?
Very confusing stuff 😆
Unawaza kama mimi. Ni kama tukifa inakuwa tu kama kipindi ambacho hatukuzaliwa tayari, kama wewe umezaliwa 1990, basi ukifa inakuwa sawa na ilivyokuwa mwaka 1989 kabla hujazaliwa
Yani habari yako ndo imeishia hapo

Ila najiuliza ni nani aliyeamua iwe hivi? Na faida yake ni nini? Nani alikuwa wa kwanza kuzaa binadamu na kisha tukazidi kuzaliana hadi leo, au ndio kwamba kuzaana hakuna mwanzo au mwisho, na kama hakuna mwanzo wala mwisho inafikirisha sana, kitu kinawezaje kutokuwa na mwanzo
Na kama kuna aliyetuumba yeye alitokea wapi? Kuna mambo mengi sielewi kabisa. Au ukute yanaeleweka ila uwezo wetu wa kufikiri sisi binadamu ni mdogo sana kiasi kwamba hatuwezi kuelewa inawezekanaje kuzaliana kusiwe na mwanzo wala mwisho. Au aliyeumba vyote hivi ni nani na anafaidika na nini 🤔
 
Ila vitu vingine vinatisha asee, hasa mlipogusia mambo ya dejavu dahh nimekumbuka jambo zito sana lililowahi kunitokea
 
Hata mimi nahisi hatufi mazima
Lakini kuna dhana ambayo naona ipo sahihi zaidi. Nayo ni kwamba ukifa ndio unapotea mazima, haurudi tena duniani na ndio inakuwa imeisha hiyo
Hii naiamini kwa asilimia nyingi zaidi, japo kuna muda nikiwaza hata hiyo ya kwamba ukifa unazaliwa tena inamake sense kuliko hizi habari za kwenda motoni na peponi
Naamini Mungu wetu ni Mungu wa haki,maandiko yanasema mtu anaweza kuua watu hata 10,000 lakini siku ya mwisho akitubu ataona pepo ,na mtenda mema akiharibu siku yake ya mwisho atapotea , dhana hizi ukichek hazina Haki lakini apa kwenye Reincarnation ndipo haki upatikana utaishi vile uliwatendea binadamu wenzako kwenye previous life,kama uliwatendea ubaya utayaishi hayo maisha ,kama uliwatendea mazuri ,pia utayaishi hayo mazuri
 
They say we’re fundamentally made of atoms, and atoms can neither be created nor destroyed. Ukiingia deeper kwenye quantum mechanics,mambo ya entanglement na superposition, unanifanya nianze kuamini kwamba hakuna kufa kabisa, we don’t disappear, tuna evolve tu
 
Kwani nani amesema haufi? Hapa mleta mada anamaanisha baada ya kifo, kwamba kuna uwezekano mtu akazaliwa kwenye mwili mwingine
Hakuna tofauti na wanaoamini kuhusu motoni na peponi
Pia unaposema nijiandae na umauti, actually mimi sijiandai na kifo chochote kile, ninaishi kawaida kivyangu mpaka umauti utakaponikuta wenyewe. Kwa nini nijiandae na sijui nakufa lini?
Ukifa cha kwanza ni kuvuliwa nguo na kila ulichonacho kinatolewa iwe pete, mkufu, saa n.k so jiandae kwasababu unaenda bila chochote mkuu.
 
Hii ina ukweli, kila baada ya muda fulani huwa naota maisha ya kale nipo sehemu moja hivi ambayo inafanana mara zote, nimeshawahi kuota zaidi ya mara 5 na eneo lenyewe daah! Huwa nafikiria saana! Mbaya zaidi mabasi yale ya zamani sana, halafu miundomibunu mibovu!
 
Back
Top Bottom