Reincarnation...nazidi kupata uhakika binadamu hatufi

Reincarnation...nazidi kupata uhakika binadamu hatufi

Aliyetueleza ametuumba kwa utaratibu huu na huu, na sayansi imethibitisha ndio yeye ametueleza tukifa tunaenda wapi, na uhalisia ni shahidi mzuri, umeona mtu amekwepa kifo?! hata uwe Buddha wa nyota 70 siku ikifika unaenda na maji kirahisi sana, so na wewe ukiuza simu punguza kujipa matumaini jiandae na mauti yako.
Kwani nani amesema haufi? Hapa mleta mada anamaanisha baada ya kifo, kwamba kuna uwezekano mtu akazaliwa kwenye mwili mwingine
Hakuna tofauti na wanaoamini kuhusu motoni na peponi
Pia unaposema nijiandae na umauti, actually mimi sijiandai na kifo chochote kile, ninaishi kawaida kivyangu mpaka umauti utakaponikuta wenyewe. Kwa nini nijiandae na sijui nakufa lini?
 
Sio tu haufi, au sio tu kwamba utazaliwa tena na tena, unaweza ukafa na ukabaki hapa hapa, isipokuwa mazingira yanabadilishwa kidogo tu wanakuweka kwenye ulimwengu unaofanana na ule uliokuwamo awali.

Kwanza hutajua kama umekufa, utaendelea tu huku wao wanakuchekaaaa!

Hii ni kwa wachache sana.
 
Mabudha wanasema kila nafsi huwa ina mission yake maalum inabidi ikamilishe kabla ya kufa, hivyo kama hujakamilisha utakuwa unazaliwa tena na tena mpaka ukamilishe. Na ukisha kamilisha unaenda kuungana na ufahamu wa ulimwengu na kuwa moja na ufahamu huo.
 
 
Naam hili jambo nilikuwa nalichukulia poa...lakini baada ya kuamua kufuatilia kidogo naanza kupata uthibitisho pasi kuwa na shaka juu ya mzunguko wa maisha ya viumbe sisi bin adamu.

Kwa kifupi sana tafiti ni nyingi lakini......nilipata kuishi nyanda za juu kusini mwa Tanzania nikiwa kijana mdogo miaka mingi sana iliyopita.

Nilikuwa nina rafiki yangu Mbulushi...rafiki yangu huyu kwa bahati mbaya alifariki.

Siku ya siku sina hili wala lile nikiwa katika nchi ya mbali sana nikakutana na kijana mmoja amefanana na yule rafiki yangu kwa zaidi ya asilimia 90%...nikabaki namshangaa...kitu cha ajabu na yeye kama alikuwa ananishangaa...nikamuuliza ulishawahi kuishi.

Tanzania...akasema hapana hata Neno Tanzania ndio leo analisikia.
Ajabu zaidi anasisitiza kwamba ananifahamu lakini hakumbuki ni wapi tulisha kuwahi kuonana
Mahali ambapo nilipata mshituko niliona alama katika mkono wake wa kulia sawasawa na yule rafiki yangu,,,(alama hii naikumbuka kwa sababu alianguka na baiskeli akachanika na kushonwa katika hospitali ya Aga khan)....sasa huyu jamaa anasema hiyo alama amezaliwa nayo hivyohivyo.

Nikijaribu kumuuliza yeye asili yake ni wapi anasema ni Afganistan na hana ndugu wala jamaa Afrika.

Kwa kifupi sana 1.Sauti yake 2.Ongea yake 3.Namna anavyotembea ni yule marehemu kabisa kabisa.

Yule Marehemu leo angekuwa na miaka kama 70 hivi na huyu niliyekutana nae yuko kwenye miaka ya 30 katikati.
Ukifa unazaliwa nch nyingine
 
Kuna maeneo au watu ni kama umeshawahi kuwaona sehemu lakini uwakumbuki....ni kama mlishawahi kuonana au ulishawahi kuishi sehemu fulani fulani lakini huezi elezea na kukumbuka vizuri.....we are not alone on this one!
 
Hata mimi nahisi hatufi mazima
Lakini kuna dhana ambayo naona ipo sahihi zaidi. Nayo ni kwamba ukifa ndio unapotea mazima, haurudi tena duniani na ndio inakuwa imeisha hiyo
Hii naiamini kwa asilimia nyingi zaidi, japo kuna muda nikiwaza hata hiyo ya kwamba ukifa unazaliwa tena inamake sense kuliko hizi habari za kwenda motoni na peponi
Dhana ya Ukifa hauendi popote ni uongo kwasababu hakuta kuwa na 'wewe' wa kwenda popote. Kama ambavyo hakukuwa na 'wewe' kabla hujazaliwa..ndivo itakavokuwa utakapokufa.

Na hii ni kwasababu hakuna kitu kinaitwa 'wewe'

Kila kitu unachomaanisha usemapo 'mimi' hakipo.
 
Back
Top Bottom