Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Pumzika mtani. Jumamosi tupo na wewe fainali Copa del Rey. Tuko na maswali mengi sana ya kuiuliza defense yenu!

😅😅😅😅😅
 
Kama tulivyosema nyakati nyingi hapa,timu kwa ujumla inahitaji mabadiliko makubwa sana,kuanzia eneo la beki hadi katikati pale,beki za kati na pembeni zipo hoi,haswa za pembeni,kaumia Carvajal basi kila mahali ni tobo hakuna muongozaji wa eneo la ulinzi,katikati hapo Valverde nafikiri ni uchovu sana na kuhamishwahamishwa namba,Tchoumeni na Ceballos ni wafangakazi hewa,hata Camavinga pia...hili eneo linahitaji mabadiliko makubwa sana...babu Modric huu uwe msimu wa mwisho kwake,hawa madogo kama hawaaminiwi basi watolewe...eneo la kati kwa maana ya namba 6 tunahitaji watu katili kweli kweli wenye uwezo wakunusa hatari na wanaoweza kujitoa kwa timu,huyu Fran Garcia kashindwa hata kuchukua kadi nyekundu kwa faida ya timu hata iwe draw..benchi la ufundi nalo litoke tu maana mbinu zao zimeshapitwa na wakati.

Yote kwa Yote,tuonane msimu ujao,huu kwetu umeshakwisha kwa aibu..tutarudi tukiwa imara msimu ujao.

Tchou, camavinga ni brainless hamna kitu pale. Sifa wanazopewa ni kubwa mno kuliko uwezo wao sio players wa caliber ya Madrid wale ni players wa Espanyol huko.
 
Nilisema hivi kwenye Uzi mwingine. Mtu yeyote aliyedhani RM inapita hii draw hajui mpira.

Screenshot_20250417_023357_Chrome.jpg
 
Acha wamalize hasira zao zimewajaa vifuani mwao miaka nenda rudi,huwezi kuwa na mafanikio mara dufu ya wao tena combined halafu ukaungwa mkono,they know sisi ndio vizingiti kwao,so kututoa huwa ni zaidi ya sherehe kwao...ndio maana unaona penalt waliopata wao,the same scenario ndio hiyo tulionyimwa sisi ila hakuna anayeiongelea hilo,this is because "We are Real Madrid"..
Kabisa mkuu hii ni sherehe kwao.
 
Tchou, camavinga ni brainless hamna kitu pale. Sifa wanazopewa ni kubwa mno kuliko uwezo wao sio players wa caliber ya Madrid wale ni players wa Espanyol huko.
Tumeamua tu kuwazingatia hawa lakini Madrid kuna takataka nyingi sana mchezaji kama Vasquez, Garcia, Militao ,Endrick,Diaz na Guler wanafanya nini Madrid,

Kingine wachezaji quality madrid hawana consistent mfano Vini na Rodrigo hawawezi cheza miezi 2 consecutive kwa kiwango kile kile.
 
Ni wakati sahihi wa Don Carlo kupumzika maana hamna kipya kwake anategemea tu individual brilliant kwa key players
 
Ni Madrid wenyewe kuleta vyuma vya kazi, Jana Saka na Martinelli wote walikuwa wakirudi Hadi chini kabisa kukaba na imekuwa hivyo Kila siku Kwa arsenal, Sasa hivi mido ya Rice, Partey na Odegaard Iko compact sana na akili nyingi, Arsenal walikuwa hawatembei tu uwanjani Kila movement waliyofanya hata kama hawakuwa na mpira ilikuwa na maana.

Kilichoamua ni ubora wa Arsenal, hata mechi ingerudiwa mara kumi Bado Madrid angefungwa tu... Arsenal msimu huu Yuko Bora sana hivyo mara nyingi hufungwa Kwa ujanja ujanja na mpira wa kihuni huni, ukisema uende nao toe to toe kama ni mchovu hutoboi, mfanyie uhuni basi unamfunga...Subirini muone ikitokea Arsenal akakutana na Inter Milan, utaona jinsi mpira wa kihuni ulivyo na unavyochezwa.
 
Back
Top Bottom