RC Mwanamvua MRINDOKO Awataka Watumishi wa Umma Kusimamia na kutunza Mali na Maeneo ya Taasisi za Serikali

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua MRINDOKO amewataka watumishi wa umma waliopewa dhamana ya kusimamia taasisi za serikali kutunza mali na maeneo yote wanayoyasimamia ili yasivamiwe.​

RC Mhe. Mwanamvua MRINDOKO ameyasema hayo katika mkutano wa kusikiliza kero uliofanyika tarehe 05 Machi, 2024 jioni katika Kata ya Shanwe.

"Niwatake wasimizi wa taasisi za serikali kulinda maeneo wanayoyasimamia ili kuepusha migogoro. Haliwezekani mwananchi anavamia eneo la serikali anaanza ujenzi na wewe upo na haujachukua hatua" - Mhe. Mwanamvua MRINDOKO, RC Katavi

Pia, Mwanamvua MRINDOKO amewaasa wananchi waache mara moja tabia ya kuvamia maeneo ya umma, maana yapo kwa ajili yao na hivyo hawana budi kufuata taratibu zilizopo ili kuepusha migogoro.

GH52D1hWYAAJja3.jpg
GH5z4TAWAAE_luY.jpg
GH5z4S7WwAAGIhZ.jpg
GH502RCXgAAkynH.jpg
 
Back
Top Bottom