Waziri Simbachawene asisitiza matumizi ya Serikali Mtandao kwa Taasisi za Umma ili kuepusha malalamiko ya Wananchi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Snapinsta.app_381293897_1290782384902144_5253396255696806297_n_1080.jpg

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amesisitiza matumizi ya Serikali Mtandao katika kudhibiti vitendo vya uvunjifu wa Maadili katika Utumishi wa Umma ambavyo vinaleta malalamiko Serikalini.

Mhe. Simbachawene amesema hayo leo tarehe 21 Septemba, 2023 wakati akifungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kilichowashirikisha wadau kutoka Taasisi Simamizi za Maadili ya Utendaji, Taasisi Simamizi za Maadili ya Kitaaluma na watumishi kutoka kwenye Wizara mbalimbali na taasisi za kitaaluma katika ukumbi wa PSSSF-Makole Dodoma.

“Ni matarajio yangu kuwa mikakati itakayofikiwa katika kikao hiki itasaidia kuondoa malalamiko kuhusu vitendo vya uvunjifu wa maadili kwa watumishi na Taasisi za Umma zinazosimamia upatikanaji wa haki” amesisitiza.

Aidha, Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa malalamiko yanayotolewa na wananchi yanapaswa kufanyiwa kazi kwa kutoa elimu kwa wanataaluma na watumishi wa umma wote ili wazingatie Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia maadili ya utendaji kazi na miiko ya taaluma zao.

Snapinsta.app_380483038_3669013610000086_8357835384113180751_n_1080.jpg

Vilevile, ameelekeza viongozi katika Ofisi yake kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu. Pia, Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma zinapaswa kusimamia na kuchukua hatua stahiki kwa wakati kwa wale wanaokiuka maadili ya taaluma zao kwa lengo la kuendelea kujenga imani kwa wananchi na kuongeza uwajibikaji na usikivu.

“Ofisi yangu itaendelea kushirikiana na Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma kutoa ushauri wa kitaalamu pale itakapohitajika; kutoa ushauri katika mapitio na maboresho ya Kanuni za Maadili za Kitaaluma; kujenga uelewa kuhusu Maadili ya Utumishi wa Umma; na kushirikiana nanyi katika kuleta mabadiliko ya fikra miongoni mwa watumishi wa umma ambao nao ni wanataaluma katika Taasisi mnazoziwakilisha” amesema.

Chanzo: Rainer Budodi-Dodoma
 
Watu wenyew wa serikali ndo hao akina nape wanafunga mpaka replies mtandaon 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom