RC Morogoro awasweka rumande Wakuu wa Shule baada ya shule wanazozisimamia kufanya vibaya mtihani wa Taifa

HABARI WAKUU. HII HABARI HUU NI UZUSHI. MIMI NIKO MOROGORO NA NILIKUA KATIKA HICHO KIKAO. N KWELI KUNA WATU WALIWEKWA NDANI LAKINI SI WALIMU NA WALA SI ISHU ZA WANAFUNZI KUTOFANYA VIZURI MTIHANI. HAPA ALIYETOA TAARIFA ANATAKIWA AJISAHIHISHE KABISAAA.
Sababu sahihi ni ipi boss! Kama ni kweli itakuwa ni aibu kwa mkuu wa mkoa.
Anayesimamia Sera ya Elimu ni Wizara. Mmkuu wa mkoa ana haki hiyo wakati wa ufundishaji. Hapo alikuwa na haki ya kuwasweka ndani kwa kutotimiza wajibu wao.

Kwa uhuni wa waalimu wa shule za serikali kweli anastahili kufanya hayo wakati wa akufundisha.
 
Kuna watoto wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma then wanafaulu vizuri tu. Halafu tunakaa tunaimba sifa na mapambio kwamba ufaulu wa darasa la saba umepanda.

Then haya ndio matokeo yake.

Hiki kilichofanyika siyo sawa hata kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kile chama cha serikali wenyewe wanakiita cha Walimu ngoja tuwasikie, unaweza kuta hata kutoa neno wasitoe

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna sababu nyingi za watoto kutofanya vizuri katika mitihani yao.
1. Msingi wa mtoto toka awali.
2. Miundombinu ya elimu.
3. Walimu mahiri na wa kutosha.
4. Vitabu.
5. Madawati
6. Maabara.
7. Ni.
 
Mpaka shule hizo zilizo kwenye mkoa wake kufanya vibaya hata yeye anastahili kuwekwa ndani kwa uzembe wa kutowasimamia hao walimu/shule mapema. Sasa watoto wameisha fail ndiyo anakumbuka shuka saa mbili asubuhi. Mzembe wa kutupa huyo rc.
 
KARLO MWILAPWA,
Kama Mtumishi hawezi kazi si ashushwe cheo?!!? Kumsweka rumande kunasaidia nini, akitumikia adhabu mnamrudisha kwenye nafasi yake? Kuna shule naskia zimepewa elfu 45 zijiendeshe. Elimu bure balaa. Hizo shule zinazofaulisha kaangalie gharama yake. Tusilete siasa. Mtu hawezi kazi apigwe chini.
 
Itabidi waalimu wajitahidi kutumia mbinu zote halali na haramu shule zao zifaulishe!
Mbinu haramu utegemee Nini katika maisha ya baadae kwa watanzania?.
Utapasuliwa jicho badala ya kung'olewa jino.
Chezea elimu uone
 
Kama Mtumishi hawezi kazi si ashushwe cheo?!!? Kumsweka rumande kunasaidia nini, akitumikia adhabu mnamrudisha kwenye nafasi yake??? Kuna shule naskia zimepewa elfu 45 zijiendeshe. Elimu bure balaa. Hizo shule zinazofaulisha kaangalie gharama yake. Tusilete siasa. Mtu hawezi kazi apigwe chini.
Namkumbuka Jackson Makweta akiwa waziri wa elimu,alikuwa kweli Ni waziri wengine walopita mbele yake sioni wa kuvaa viatu vyake.
Waziri wa elimu alitakiwa kukemea wanasiasa wanao ichafua elimu,naye yupo tu kana kwamba hayupo
 
Moro inachangamoto sana katika miundombinu ya elimu&jamii.
Kama kafanya hivyo kweli,basi
hajawatendea haki.
 
Back
Top Bottom