Gharama ya kusajili mtahiniwa binafsi kidato cha nne ni kubwa mno

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
380
573
NECTA na Morogoro Sec ni mtandao wa wezi kwa watahiniwa binafsi. Kujisajili kidato 4 kwa Sh. 160,000 ni kubwa.

Nani anapanga kikomo cha kulipia kwenye vituo vya kufanyia mitihani watahiniwa binafsi?.

Nimefika shule ya sekondari Morogoro kumsajili kijana wangu afanyie mtihani wake wa kuhitimu kidato cha 4 mwaka huu pale kama mtahiniwa binafsi.

Kwa kweli nimeshangazwa na ghalama za kituo kile licha ya kupewa ufafanuzi na mtaaluma wa shule ile. Baraza la mitihani Taifa (NECTA) unalipia 50,000, pale shuleni unalipa 20,000 na kwa Kila somo eti unaongeza 30,000.

Kijana wangu anafanya masomo matatu ya sayansi natakiwa kulipa 90,000. Jumla amesajiliwa kwa Tsh 160,000/= ( 50,000 + 20,000 + 90,000). Hiki ni kiwango kikubwa kwa mzazi wa kipato cha kawaida.

Kwanini isibaki 20,000.
 
Pole sana mkuu, gharama ni kubwa sana na zinaumiza ila hamna namna, mwambie kijana wako akomae tu ili afaulu mitihani yake kufanya paper kama private candidate ni kipengele.
 
Hiyo sio kubwa Kama anafanya na practical.

Then ikiwa umechelewa kulipa huwa kuna penati , Jitahidi umpambanie kijana

Elimu unalipa Sana
 
NECTA na Morogoro Sec ni mtandao wa wezi kwa watahiniwa binafsi. Kujisajili kidato 4 kwa Sh. 160,000 ni kubwa.

Nani anapanga kikomo cha kulipia kwenye vituo vya kufanyia mitihani watahiniwa binafsi?.

Nimefika shule ya sekondari Morogoro kumsajili kijana wangu afanyie mtihani wake wa kuhitimu kidato cha 4 mwaka huu pale kama mtahiniwa binafsi.

Kwa kweli nimeshangazwa na ghalama za kituo kile licha ya kupewa ufafanuzi na mtaaluma wa shule ile. Baraza la mitihani Taifa (NECTA) unalipia 50,000, pale shuleni unalipa 20,000 na kwa Kila somo eti unaongeza 30,000.

Kijana wangu anafanya masomo matatu ya sayansi natakiwa kulipa 90,000. Jumla amesajiliwa kwa Tsh 160,000/= ( 50,000 + 20,000 + 90,000). Hiki ni kiwango kikubwa kwa mzazi wa kipato cha kawaida.

Kwanini isibaki 20,000.
Are you serious? 160K kwa elimu unaona nyingi?
 
Back
Top Bottom