RC Morogoro awasweka rumande Wakuu wa Shule baada ya shule wanazozisimamia kufanya vibaya mtihani wa Taifa

Wakion
Mkuu wa mkoa Morogoro amewaweka rumande Wakuu wa Shule ambao shule zao zimeshindwa kufanya vizuri katika mtihani wa taifa kidato cha pili na cha nne mkoani humo pamoja na kuwavua madaraka ya ukuu wa shule

Hatua hiyo imefikiwa hapo jana siku ya Alhamisi tarehe 16/01 2020 kwa kile kilichodaiwa kuwa ni matokeo mabaya ya shule hizo pamoja na makosa mengine.
Wakiona inafaa wanawapa kesi ya uhujumu uchumi wa taifa kwa lengo la kuwanyoosha zaidi!
 
Kwahiyo anataka kutuambia kwamba walimu wao nao wafanye mtihani?

1. Mbona mishahara haipandishwi wakati maisha yamepanda? Au anataka Uwaziri nae

2. Elimu ni bure lakini elimu yetu haina thamani maana elimu inayotufaa ni UFUNDI KWA BAADHI YA WANAFUNZI secondary hawezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm nikiwa mwalimu sitokubali upumbavu wa kuwekwa ndani cjui na DC au RC. Kwa wanafunzi kufeli.aisee cjui aniweke nimekufa..
 
Ipo sheria ya utumishi wa uma inayosimamia mienendo ya utendaji kazi wa watumishi. Kuna
Umuhimu wa viongozi wa kisiasa kufundishwa madhumuni ya uwepo wa sheria hizi.
kuwaelimisha hakuwasaidii mkuu...wa africa tumeenda madarasani lakini ona tulivyo...sema wawajibishwe wanapovunja hizo sheria...
 
Mkuu wa mkoa Morogoro amewaweka rumande Wakuu wa Shule ambao shule zao zimeshindwa kufanya vizuri katika mtihani wa taifa kidato cha pili na cha nne mkoani humo pamoja na kuwavua madaraka ya ukuu wa shule

Hatua hiyo imefikiwa hapo jana siku ya Alhamisi tarehe 16/01 2020 kwa kile kilichodaiwa kuwa ni matokeo mabaya ya shule hizo pamoja na makosa mengine.
Busara zaidi ni waziri mwenye dhamana kumuweka ndani huyo mkuu wa mkoa kwa matokeo kuwa mabaya katika mkoa anao uongoza,lakini pia ni vizuri Mh.rais akamuweka ndani waziri kwa kushindwa kusimamia ufaulu katika mikoa kadhaa ikiwemo Morogoro...

Hivyo yaani...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakitoka huko ndani warudi mashuleni kwao, warekebishe matokeo ya wanafunzi. Haiwezekani mwalimu mkuu akubali matokeo halisi halafu aachwe hivi hivi tu!!

Mkandarasi wa kichina ambaye ili kazi iishe nae awekwe ndani. Akiwa huko ndani huku nje kazi ya miezi 4 imalizike katika siku mbili atakazokuwa ndani!!
Historia itakuwa 'katili' sana kwa watu kama huyu RC pale itakapoandikwa miaka 20-50 baadae. Wajukuu watakwepa kutumia jina la RC huyu
 
Jamaa.. uelewa wake ni mdogo sana kwa hili alilo fanya. Je kufanya hivyo ndio kuinua ufaulu shuleni.... Changamoto ni nyingi sana. Kwanza kipaumbele cha taifa, wazazi, mtoto mwenyewe na waalimu. Amekurupuk na huenda wakafanya vibaya zaidi kama asipo jisahihisha kosa alilofanya elimu haihitaji nguvu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuchitimbo,
Baadhi ya maamuzi ya wanasiasa wetu yanasikitisha sana. Kuna wakati tumepata taarifa kwamba wazazi wa pande zote mbili ambao watoto wao wamepeana mimba waswekwe ndani pamoja na watoto wao waliofanya kosa hilo. Shangaa, kosa wafanye wengine halafu adhabu wapewe watu wasiohusika kabisa. Tendo lenyewe hufanyika kwa siri, sasa mzazi anaingiaje hapo?
 
Ukitazama kila pande ya nchi unakutana na ujinga, kuanzia viongozi mpaka vyombo vya habari, unaweza ukahitimisha kuna tabaka la juu linalofanya juhudi za makusudi za kuumea.
Angalia tofauti ya vipindi vinavyotengenezwa kwa fedha ya walipa kodi BBC na aina ya uwekezaji kwenye maudhui ya TBC.
Unamsikiliza katibu mkuu wa chama tena msomi huoni cha kupanua akili, bora umsikilize Greta, binti wa miaka 16 utatoka na kitu.
Wajuvi nipeni jibu,ualimu kazi gani
Walimu na majaribu,mnawawazia nini
Waalimu wanatabu,kwani wamekosa nini
Ualimu unagubu,walimu andamaneni

Morogoro morogoro,shule si wenu mfano
Mnawaza vigodoro,mkajishike viuno
Daftari si kiporo,eti unywe na wino
Morogoro kupo doro,wekeni maelewano
 
Mkuu wa mkoa Morogoro amewaweka rumande Wakuu wa Shule ambao shule zao zimeshindwa kufanya vizuri katika mtihani wa taifa kidato cha pili na cha nne mkoani humo pamoja na kuwavua madaraka ya ukuu wa shule

Hatua hiyo imefikiwa hapo jana siku ya Alhamisi tarehe 16/01 2020 kwa kile kilichodaiwa kuwa ni matokeo mabaya ya shule hizo pamoja na makosa mengine.
KAMA N KWELI HUUU N UZALILISHAJI NAMSUBIR MAMA PROF SEMI YAKE ANASEMAJE
HAWA WATU WANAFAMILIAA HII TABIA IFIKE IKOMESHWE KABISA

WAZAZI WA WANANFUNZI WAKISIKIA MNAHISI WANAFANYAJE NEXTY
 
Back
Top Bottom