Kwanini kuna kasi ya wanafunzi kuacha shule hasa wa kiume? Taifa linaangamia

Nyamesocho

JF-Expert Member
May 5, 2023
476
1,244
Ni janga la wanafunzi kuacha shule, sijui kama Serikali inalijua hili

Wakati nchi nyingi duniani zinahakikisha wananchi na watoto wote wanapata elimu bila kumuacha hata mmoja ili kukabiliana na maendeleo ya sayansi na teknolojia hali ni tofauti nchini Tanzania.

Watoto wanaoandikishwa kuanza shule huwa ni wengi mfano shule X inaweza kuandikisha wanafunzi 120 wanaoanza darasa la kwanza lakini watakao hitimu darasa la saba ni 60,wanafunzi wengine 60 hawajulikani walipo ,imagin hapo ni shule moja je vipi hali ya nchi nzima?

Achana na shule za msingi tunakuja secondary zetu za kata,shule X ilipokea wanafunzi 200 kuanza kidato cha kwanza lakini watakaofanya mtihani wa Taifa kidato cha nne ni 80,je hao 120 wameenda wapi?

Kwa sasa kuna kasi sana ya wanafunzi kuacha shule kuanzia msingi mpaka sekondari,je profesa Mkenda analijua hili?

Cha ajabu zaidi watoto wa kiume wanaongoza kuacha shule,kusoma wameachiwa watoto wa kike!

Tutakuja kuwa na Taifa la kipekee duniani,Taifa la kijima la watu wasio na elimu?
 
Hata mimi bila ya mikwaju ya mama ningeacha kitambo sana....
Na mda huu ningekua mtu mwingine kabisa 🤓🤓🤓

Mdogo angu mtoto wa mama mdogo yeye aliacha toka la darasa la 4 hivi sasa ni mtaalamu wa kuvua huko lindi kiufupi yupo vizuri.

Mara nyingi ananifariji ""kaka usione mi nimetoboa wewe ni msomi siku ukija toboa wewe kimaisha mimi sitokufikia hata robo""

Jamaa angu mwingine tumefika form 2 yeye akaachana na habari za shule.

Akawa konda wa mabasi makubwa.

Mpaka sasa hivi yupo south africa hiko na wazazi wake wanajivunia kuwa na mtoto kama yule maana ana fanya Wonder kwa wazazi wake kwa financial support

Kidato cha tano mwana mwingine aka drop.

Unajua muscular ya PCB.

Jamaa akaingia maeneo ya kabwe mbeya pale piga harakati zake sana.

Now hii ana duka moja la simu kabwe pale stand tu,, sio duka ana ma project mengine kibao

Bado chuo mwaka wa kwanza semister ya pili mwanangu wa faida wizzy. Mambo ya coding kaona sio poa ka drop... huyu siongei sana ila.

Kwa sababu kama hizo hata mi najuta why nilisoma aiseeee.

Mungu alikua ananipa kila dalili lakini wapi. yaani wanangu wote hao now ni watu wengine washajipata
 
Kuna sababu za kuangalia pia.
Kutoka form 1 mpka form 4
Kutoka la 1 mpaka la 7.....
Kufeli kidato cha pili huwa ni wachache mnoo ni sawa na asilimia 0.001,wanaohama ni asilimia ndogo hata moja haifiki, wengi wanaacha shule hasa wavulana, hii nchi itakuja kuwa na vibaka wengi saaana
 
Hata mimi bila ya mikwaju ya mama ningeacha kitambo sana....
Na mda huu ningekua mtu mwingine kabisa

Mdogo angu mtoto wa mama mdogo yeye aliacha toka la darasa la 4 hivi sasa ni mtaalamu wa kuvua huko lindi kiufupi yupo vizuri
Mara nyingi ananifariji ""kaka usione mi nimetoboa wewe ni msomi siku ukija toboa wewe kimaisha mimi sitokufikia hata robo""

Jamaa angu mwingine tumefika form 2 yeye akaachana na habari za shule.
Akawa konda wa mabasi makubwa.
Mpaka sasa hivi yupo south africa hiko na wazazi wake wanajivunia kuwa na mtoto kama yule maana ana fanya Wonder kwa wazazi wake kwa financial support

Kidato cha tano mwana mwingine aka drop.
Unajua muscular ya PCB.
Jamaa akaingia maeneo ya kabwe mbeya pale piga harakati zake sana
Now hii ana duka moja la simu kabwe pale stand tu,, sio duka ana ma project mengine kibao

Bado chuo mwaka wa kwanza semister ya pili mwanangu wa faida wizzy. Mambo ya coding kaona sio poa ka drop... huyu siongei sana ila....

Kwa sababu kama hizo hata mi najuta why nilisoma aiseeee.
Mungu alikua ananipa kila dalili lakini wapi..... yaani wanangu wote hao now ni watu wengine washajipata
Kusoma si kwamba ni lazima upate ajira,elimu inakusaidia kupambana na mazingira uliyomo, na kusoma inakusaidia baadhi ya mambo kama masuala ya afya na kijamii,na anayetoboa kisa hana elimu ni mmoja Kati 1000,sisi hatuangalii mtu mmoja tunasemea majority kuacha shule ni hatari kwenye Taifa
 
Sawa
 
Ni janga la wanafunzi kuacha shule,sijui kama Serikali inalijua hili

Wakati nchi nyingi duniani zinahakikisha wananchi na watoto wote wanapata elimu bila kumuacha hata mmoja ili kukabiliana na maendeleo ya sayansi na teknolojia hali ni tofauti nchini Tanzania

Watoto wanaoandikishwa kuanza shule huwa ni wengi mfano shule X inaweza kuandikisha wanafunzi 120 wanaoanza darasa la kwanza lakini watakao hitimu darasa la saba ni 60,wanafunzi wengine 60 hawajulikani walipo ,imagin hapo ni shule moja je vipi hali ya nchi nzima?

Achana na shule za msingi tunakuja secondary zetu za kata,shule X ilipokea wanafunzi 200 kuanza kidato cha kwanza lakini watakaofanya mtihani wa Taifa kidato cha nne ni 80,je hao 120 wameenda wapi?

Kwa sasa kuna kasi sana ya wanafunzi kuacha shule kuanzia msingi mpaka sekondari,je profesa Mkenda analijua hili?

Cha ajabu zaidi watoto wa kiume wanaongoza kuacha shule,kusoma wameachiwa watoto wa kike!!!!

Tutakuja kuwa na Taifa la kipekee duniani,Taifa la kijima ,la watu wasio na elimu?
Acha porojo leta ripoti ya utafiti
 
Acha porojo leta ripoti ya utafiti
Hii haitaji digrii kufanya utafiti, huko mtaani kwako si kuna shule,na shule ni mali ya umma hivyo wanatoa taarifa, fika na ulizia hali ya utoro watakupa taarifa, pia angalia watoto wanaozurura mtaani asubuhi na kwa umri wao walipaswa wawe shule, je hilo hulioni huko uliko?
 
Ni janga la wanafunzi kuacha shule, sijui kama Serikali inalijua hili

Wakati nchi nyingi duniani zinahakikisha wananchi na watoto wote wanapata elimu bila kumuacha hata mmoja ili kukabiliana na maendeleo ya sayansi na teknolojia hali ni tofauti nchini Tanzania.

Watoto wanaoandikishwa kuanza shule huwa ni wengi mfano shule X inaweza kuandikisha wanafunzi 120 wanaoanza darasa la kwanza lakini watakao hitimu darasa la saba ni 60,wanafunzi wengine 60 hawajulikani walipo ,imagin hapo ni shule moja je vipi hali ya nchi nzima?

Achana na shule za msingi tunakuja secondary zetu za kata,shule X ilipokea wanafunzi 200 kuanza kidato cha kwanza lakini watakaofanya mtihani wa Taifa kidato cha nne ni 80,je hao 120 wameenda wapi?

Kwa sasa kuna kasi sana ya wanafunzi kuacha shule kuanzia msingi mpaka sekondari,je profesa Mkenda analijua hili?

Cha ajabu zaidi watoto wa kiume wanaongoza kuacha shule,kusoma wameachiwa watoto wa kike!

Tutakuja kuwa na Taifa la kipekee duniani,Taifa la kijima la watu wasio na elimu?
Sababu iko wazi..
Kuwalazimisha vijana woote wafuate mfumo mmoja..
Hii si sawa..

Wengine wanahitaji kwenda kuwa drivers..wafanya biashara...ufundi mbalimbali...

Nafikiri hili liko addressed ktk mabadilko ya mitaala. Tusubiri utekelezaji.
 
Malezi ya sasa yanawapa sana uhuru watoto wakifikisha umri wa balehe ndipo wanapopotea huo umri unahitaji kusimama imara kimalezi
 
Nilimaliza form 4 nikafaulu vizuri tu.Ila nikaona huu upuuzi kwa nn nisiingie front kupambana na life Ugomvi ulikua mkubwa sana wa ndugu na wazazi maana hawakunielewa kwa nn nimeacha shule.Mpaka sasa hivi wamenyosha mikono maana nashukuru Mungu nimefanya vitu vikubwa tu.Shule ni mhimu ila sio kwa kila mtu.
Safi..
Ulichonacho kilikuwa naturally given by almighty God.

Si wote wanafanikiwa.
 
Hata mimi bila ya mikwaju ya mama ningeacha kitambo sana....
Na mda huu ningekua mtu mwingine kabisa

Mdogo angu mtoto wa mama mdogo yeye aliacha toka la darasa la 4 hivi sasa ni mtaalamu wa kuvua huko lindi kiufupi yupo vizuri.

Mara nyingi ananifariji ""kaka usione mi nimetoboa wewe ni msomi siku ukija toboa wewe kimaisha mimi sitokufikia hata robo""

Jamaa angu mwingine tumefika form 2 yeye akaachana na habari za shule.

Akawa konda wa mabasi makubwa.

Mpaka sasa hivi yupo south africa hiko na wazazi wake wanajivunia kuwa na mtoto kama yule maana ana fanya Wonder kwa wazazi wake kwa financial support

Kidato cha tano mwana mwingine aka drop.

Unajua muscular ya PCB.

Jamaa akaingia maeneo ya kabwe mbeya pale piga harakati zake sana.

Now hii ana duka moja la simu kabwe pale stand tu,, sio duka ana ma project mengine kibao

Bado chuo mwaka wa kwanza semister ya pili mwanangu wa faida wizzy. Mambo ya coding kaona sio poa ka drop... huyu siongei sana ila.

Kwa sababu kama hizo hata mi najuta why nilisoma aiseeee.

Mungu alikua ananipa kila dalili lakini wapi. yaani wanangu wote hao now ni watu wengine washajipata
Unakuta ungekua wee umeacha, ungekuwa bado apeche alolo.
 
Ni janga la wanafunzi kuacha shule, sijui kama Serikali inalijua hili

Wakati nchi nyingi duniani zinahakikisha wananchi na watoto wote wanapata elimu bila kumuacha hata mmoja ili kukabiliana na maendeleo ya sayansi na teknolojia hali ni tofauti nchini Tanzania.

Watoto wanaoandikishwa kuanza shule huwa ni wengi mfano shule X inaweza kuandikisha wanafunzi 120 wanaoanza darasa la kwanza lakini watakao hitimu darasa la saba ni 60,wanafunzi wengine 60 hawajulikani walipo ,imagin hapo ni shule moja je vipi hali ya nchi nzima?

Achana na shule za msingi tunakuja secondary zetu za kata,shule X ilipokea wanafunzi 200 kuanza kidato cha kwanza lakini watakaofanya mtihani wa Taifa kidato cha nne ni 80,je hao 120 wameenda wapi?

Kwa sasa kuna kasi sana ya wanafunzi kuacha shule kuanzia msingi mpaka sekondari,je profesa Mkenda analijua hili?

Cha ajabu zaidi watoto wa kiume wanaongoza kuacha shule,kusoma wameachiwa watoto wa kike!

Tutakuja kuwa na Taifa la kipekee duniani,Taifa la kijima la watu wasio na elimu?
Watoto wao wanasoma shule za kisasa hawana taabu na watoto wa maskini.....

Kikubwa wana uhakika wa kutawala milele basi tutaisoma sana
 
Back
Top Bottom