RC Morogoro awasweka rumande Wakuu wa Shule baada ya shule wanazozisimamia kufanya vibaya mtihani wa Taifa

polokwane

JF-Expert Member
Dec 16, 2018
3,359
5,808
Mkuu wa mkoa Morogoro amewaweka rumande Wakuu wa Shule ambao shule zao zimeshindwa kufanya vizuri katika mtihani wa taifa kidato cha pili na cha nne mkoani humo pamoja na kuwavua madaraka ya ukuu wa shule

Hatua hiyo imefikiwa hapo jana siku ya Alhamisi tarehe 16/01 2020 kwa kile kilichodaiwa kuwa ni matokeo mabaya ya shule hizo pamoja na makosa mengine.
 
Mkuu wa mkoa Morogoro amewaweka rumande wakuu wa shule ambao shule zao zimeshindwa kufanya vizuri katika mtihani wa taifa kidato cha pili na cha nne mkoani humo

Hatua hiyo imefikiwa hapo jana sikuwa ya Alhamisi tarehe 16/01 2020 kwa kile kilichodaiwa kuwa ni matokeo mabaya ya shule hizo pamoja na makosa mengine.
Haya ndiyo mambo ya taaluma kuweka siasa. Kwani hao walimu ndio walifanya mitihani? Yaani uongozi ni talanta sio mabavu. Kuwaweka selo itabadilisha matokeo au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Changamoto za elimu hazitokani na walimu pekee bali kila mtu.

Kuna wanafunzi ni watukutu ,hawasikii na wanajiona wanajua kuliko walimu wao, kumweka ndani Mwalimu kisa mwanafunzi huyu si sawa kabisa.

Kuna wanafunzi hawana utamaduni wa kujisomea mpaka pale mitihani inapokaribia. Kumuweka ndani Mwalimu kwa mwanafunzi kama huyu si sawa.

Kuna wanafunzi wengine hawahudhurii darasani kutokana na changamoto mbalimbali na anatokea wakàti wa mitihani tu.

Walimu pia hawawekwi mbali na lawama za kufeli kwa sababu:

Kuna baadhi ya walimu hawafundishi na wakamaliza topic kwa wakàti matokeo yake mitihani ikikaribia wanalazimisha kumaliza topic na kuwafanya wanafunzi kushindwa kuelewa.

Baadhi ya wakuu wa shule Wana ' Poor management skills' ,yeye ni kushinda ofisini hasikilizi kero za wanafunzi wake kujua changamoto za walimu wake nà walimu wanafanya wanachofanya kwa kuamini hakuna wa kuwakemea.

Ofisi za wakuu wa shule baadhi zimekuwa kama vituo vya polisi, si walimu Wala wanàfunzi wanatamàni kuingia hivyo matatizo ya shule kutotatuliwa kwa wakàti kama linahusu kujadiliana na mkuu wa shule.

Kwa upànde wa walezi/ wazazi

Kunà bàadhi ya wazazi hawafuatilia maendeleo ya mtoto wake shule. Hii inachangia wanafunzi kuwa watoro

Uhusiano hafifu baina ya wazazi na uongozi wa shule unachangia mzazi kutopata taarifa za mtoto wake kwa wakàti

Baadhi ya tabia ambazo Mwalimu hawezi kuzirekebisha kwa wanafunzi ambazo ni mzazi mwenye jukumu Hilo zirekebishwe.

Jukumu la mzazi katika kuasa, kuonya, kukanya tabia mbaya za mtoto wake lisifumbiwe macho maana hiko ndio chanzo Cha matokeo mabaya shuleni
 
Wakitoka huko ndani warudi mashuleni kwao, warekebishe matokeo ya wanafunzi. Haiwezekani mwalimu mkuu akubali matokeo halisi halafu aachwe hivi hivi tu!!

Mkandarasi wa kichina ambaye ili kazi iishe nae awekwe ndani. Akiwa huko ndani huku nje kazi ya miezi 4 imalizike katika siku mbili atakazokuwa ndani!!
 
Alitaka walimu waibe mitihani wawape wanafunzi?
Kama mitoto haijisomei na wazazi wao hawana mguso kwa elimu ya watoto wao,alitaka walimu ndo wawasomee na kuwaingiIa kichwani?.

Logic kwa walio Soma, Yaonesha hata na yeye alifanyiwa mitihani na walimu wake,na hivo alitaka walimu wa wakati huu wafanye Kama yy alivofanyiwa.maana Kama mtoto kufeli ndo iwe sababu?.
Walishafeli wangapi?

Kama Wana makosa mengine sawa la la Kama Ni wanafunzi kufeli,sikubali naye.
Mheshimiwa Rais wetu Hadi namuonea huruma,anatumia pesa ndefu kwa hawa watoto lakini ndo yanazidi kufeli tu,Bora hata angewapa form V na VI hapo Ni Safi,ila hawa wa o level Ni shida tupu.
 
Mkuu wa mkoa Morogoro amewaweka rumande wakuu wa shule ambao shule zao zimeshindwa kufanya vizuri katika mtihani wa taifa kidato cha pili na cha nne mkoani humo

Hatua hiyo imefikiwa hapo jana sikuwa ya Alhamisi tarehe 16/01 2020 kwa kile kilichodaiwa kuwa ni matokeo mabaya ya shule hizo pamoja na makosa mengine.

Hizi siasa zimeleta shida sana, zitakuja kuuwa elimu.

- Sasa serikali inawaleta wanafunzi ambao ufaulu wao ni daraja la chini kwa sababu tu wametokea katika eneo husika, na ili shule ionekane inawanafunzi, basi wanajazwa pale.

- Viongozi wa Serikali wakiambiwa waajiri waalimu, hawafanyi hivyo, utakuta darasa moja - kidato lina wanafunzi zaidi ya 500 amapo ki utaratibu, kilasomo hapo linahitaji angalau waalimu 3, sasa utakuta wapo waalimu 1 au 2 kwa kila somo kwa darasa moja.

Wanasiasa wanapaswa wafahamu yafuatayo:
1: Mwalimu amewekwa pale kwa elimu yake na si kunyoshewa kidole - kuteuliwa.

2: Wanasiasa wapo katika nafasi za kwa kuteuliwa,
 
Mkuu wa mkoa Morogoro amewaweka rumande wakuu wa shule ambao shule zao zimeshindwa kufanya vizuri katika mtihani wa taifa kidato cha pili na cha nne mkoani humo

Hatua hiyo imefikiwa hapo jana siku ya Alhamisi tarehe 16/01 2020 kwa kile kilichodaiwa kuwa ni matokeo mabaya ya shule hizo pamoja na makosa mengine.
kuwa katili haimanishi wewe ni shujaa
 
Mkuu wa mkoa Morogoro amewaweka rumande wakuu wa shule ambao shule zao zimeshindwa kufanya vizuri katika mtihani wa taifa kidato cha pili na cha nne mkoani humo

Hatua hiyo imefikiwa hapo jana siku ya Alhamisi tarehe 16/01 2020 kwa kile kilichodaiwa kuwa ni matokeo mabaya ya shule hizo pamoja na makosa mengine.
Ipo sheria ya utumishi wa uma inayosimamia mienendo ya utendaji kazi wa watumishi. Kuna
Umuhimu wa viongozi wa kisiasa kufundishwa madhumuni ya uwepo wa sheria hizi.
 
Ipo siku madokta nao watawekwa ndani kwa kuwa wagonjwa wanakufa aisee. Hatari sana.
 
Back
Top Bottom