RC Makonda: Yeyote anayeenda katika eneo la manunuzi lazima avae barakoa. Kwenye misongamano watu wakae umbali wa mita 2

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda ameagiza kuwa mtu yeyote anayeenda katika eneo lolote la manunuzi lazima awe amevaa barakoa (mask).

Amesema haijalishi ila lazima watu wavae barakoa “Ununue, ukate kanga, ukate leso na utafute rubber bands. Lazima uwe umevaa barakoa”

Aidha, ameagiza kuwa kuanzia Jumatatu biashara zote zifanyike kwa mfumo wa ‘take away’ yaani ufike sehemu ya kununua bidhaa, nunua na ondoka.

Lakini pia amewataka watu kuhakikisha wanakaa umbali wa mita mbili kila wakiwa eneo la msongamano wa watu huku akiwataka wenye masoko kutafuta mfumo mbadala na mzuri wa kusimama masoko.

 
Mbona yeye mwenyewe hajavaa hiyo barakoa na anafoka kwa nguvu? Pili, huo umbali wa meter mbili ameuzingatia kwenye hiyo video?

Kwanini asitumie radio, mitandao ya kijamii au vyombo vingine vya habari badala ya kuonana moja kwa moja na watu?

Hizo microphone anatumia mtu mmoja au zinachangiwa? Na endapo wanazichangia, zinabadilishwa zile mifuniko za sponge?
 
The Monk,
Na ndio maana nikashauri mambo ya korona waachiwe waachiwe wataalamu hawa wanasiasa achilia mbali UJINGA wao pia wanachanganya watu!!

Hivi hapo dsm hakuna dokta wa mkoa? kwanini asiachiwe yeye atoe maelekezo?
 
Ndio maana masema haya mambo ya kitaalam waachiwe wataalam.
tapatalk_1586783795204.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom