RC Makalla: Machinga wote Dar walio katika hifadhi ya barabara, Wataondolewa na vibanda vyao kuanzia Septemba 13, 2021

Yaani walianza kidogo kidogo lakini itafika mahali kila mahali hakuna utaratibu .Ukienda kariakoo shida,ukienda kwenye vituo vya mabasi unawakuta mpaka wananyanganyana nafasi na abiria.Hapa Mbezi tangi bovu ukitaka kukata kuingia main road sisi tunaotoka mitaani unakuta kibanda kimekuziba uoni upande wa barabara ili uingie yaani ni hatari tupu.Ukija hizi barabara za pembeni hapa Mbezi yaani haipitiki yaani ni bajaji ,pikipiki ni vibanda mpaka kuna siku nimejiuliza magari na watu watakuwa hawana njia za kupita Anyway, ni habari ya kuwapanga tu
 
safi sana.
kimsingi Karia koo kwa sasa inapaswa ihamie Maeneo ya MBEZI MWISHO, STENDI YA MAGUFULI.
JIJI la DSR ljnapaswa lipanuke.
tubadilike, wataalamu wa mipango miji wapo lkn hawataki kutumia taaluma zao vyema.
Tatizo sio watalamu Tatizo ni siasa za kijima tulizo nazo.jiwe alivyo leta vitambulisho vya mmachinga na kuruhusuu wakae popote, ulitegemea hao watalamu wafanye nini?.

Kuna watu wakiambiwa mamraka ya rais yadhibitiwe ki katiba hawataki, haya ndio madhara yakeee kua rais anaweza ropokaaa chochote, popote kwa yeyote na asichukuliwe hatua yoyotee.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaama Amos Makalla ameingia Kariakoo kwa kutumia basi la Mwendokasi (haijulikani alikotokea) na kutoa Maagizo kwamba baada ya siku 7 njia zote za watembea kwa miguu kwenye eneo hilo , ambazo zimejaa wamachinga , mama lishe , wachoma mihogo na wauza Alikasusi ziwe wazi

Bali haijulikani ni wapi wamachinga hao watapelekwa .
Kuna nafasi kibao pale Machinga Complex waende pale SI UNAJUA NYUMBA HAIJAAGI hata mje wageni wengi kiasi gani mtaenea tu, hata kama ni kulala sebuleni mtalala! Halfu tuache ushabiki wa kisiasa, ni shida sana ktu kutembea kwa miguu Kariakoo. Jiji limeshona kwa mpangilio ya wamachinga ya hovyo hovyo!
Watamwambia hawana maeneo mbadala ambako watapata wateja, hapo makalla atasemaje.....
 
Ukizingatia kwa sasa tunatanga Dunia ifahamu nchi yetu,ndio maana sasa hivi wale wageni wanatengeneza mkanda wa kionyesha Tanzania huko duniani.
Labda shughuli za wafanyabishara ndogo ndogo zitaharibu picha!
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameingia Kariakoo kwa kutumia basi la Mwendokasi (haijulikani alikotokea) na kutoa Maagizo kwamba baada ya siku 7 njia zote za watembea kwa miguu kwenye eneo hilo , ambazo zimejaa wamachinga , mama lishe , wachoma mihogo na wauza Alikasusi ziwe wazi

Bali haijulikani ni wapi wamachinga hao watapelekwa .
Watarejea walikotoka

Sent from my MRD-LX1F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameingia Kariakoo kwa kutumia basi la Mwendokasi (haijulikani alikotokea) na kutoa Maagizo kwamba baada ya siku 7 njia zote za watembea kwa miguu kwenye eneo hilo , ambazo zimejaa wamachinga , mama lishe , wachoma mihogo na wauza Alikasusi ziwe wazi

Bali haijulikani ni wapi wamachinga hao watapelekwa .
Wiki sio mwaka hebu tuone meno ya hili agizo kama yatauma ama yatauma na kupuliza
 
Watenge mitaa kadhaa itayokuwa maalum kwa ajili yao wamachinga,ila wasiwaondoe kabisa..na bidhaa zao wazipange vizuri kwa unadhifu..

Serikali kupitia SIDO,VETA na wadau wengine watengeneze meza ama vibanda vya kisasa vinavyoweza kuwekwa eneo hilo na kutolewa bila shida yoyote..
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameingia Kariakoo kwa kutumia basi la Mwendokasi (haijulikani alikotokea) na kutoa Maagizo kwamba baada ya siku 7 njia zote za watembea kwa miguu kwenye eneo hilo , ambazo zimejaa wamachinga , mama lishe , wachoma mihogo na wauza Alikasusi ziwe wazi

Bali haijulikani ni wapi wamachinga hao watapelekwa .
Mtapinga kama kawaida yenu.....
 
Huo ni usemi tu, tangu waanze kusema hivyo huu ni mwezi wa tano hakuna lolote walilofanya. Mkuu huyo huyo ameshindwa kuwaondoa Mbagala kwenye ujenzi wa mwendokasi! Wajenzi na wamachinga wamechamganyika kiasi hauwezi kujua panapojengwa kwani wamachinga wanatupa takataka mnamojengwa.
 
Back
Top Bottom