Dar: Bilioni 44 za Mikopo ya Halmashauri hazijarejeshwa, zimeliwa

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla, ameagiza kufuatiliwa kwa marejesho ya mikopo ya Halmashauri inayotolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu huku ripoti zikionesha tangu mikopo hiyo ianze kutolewa ni bilioni 18 pekee zimerejeshwa huku bilioni 44 zikiwa hazijarejeshwa.

RC Makalla ameyasema hayo leo Septemba 28, 2022, wakati wa kikao chake na Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi, Mameya na wadau wa mikopo hiyo ya Halmashauri huku akihimiza fedha hizo kuwafikia wanufaika waliokusudiwa na serikali.

RC Makalla amesema kuwa, tangu mikopo hiyo ianze kutolewa, mkoa huo katika Halmashauri zake zimekwishatoa zaidi ya bilioni 60.

Chanzo: EastAfrica Tv
 
Mikopo inatolewa kwa kujaza forms manually+ Viongozi kujukopesha wenyewe+ Wakopaji kukopa zaidi ya wilaya 2+ Mikopo hewa+ utunzaji hafifu wa forms za kuombea mikopo na kuliwa na panya na kunyeshewa mvua😁😁 ....
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Amos Makalla amesema Jijini humo kwamba , zaidi ya Shilingi Bilioni 44 zilizotolewa na Halmashauri kama mkopo kwa Wanawake , Vijana na Walemavu hazijarejeshwa tangu utaratibu wa kukopesha makundi hayo ulivyoanza hadi sasa .

Hebu toeni maoni yenu kwenye hili .

Bali inafahamika kwamba Hela nyingi za mikopo hii ya Halmashauri zinapigwa na viongozi wa Halmashauri pamoja na viongozi wa Wilaya wa ccm , badala ya walengwa .

Kwa mfano , huko Temeke , RC Makalla alibaini shilingi mil 300 kukopeshwa kwa Mwenyekiti wa ccm wa Wilaya hiyo peke yake , na tena alizipiga bila kurejesha , Usanii wa kuiagiza TAKUKURU ichunguze ulifanyika , lakini ripoti ya uchunguzi huo hatukuwahi kusomewa hadi leo .

Mungu ibariki Tanzania ukipenda wewe mwenyewe
 
Pongezi kwa serikali maana hakuna afisa maendeleo aliyekonda kipindi hiki.....
Wa kwetu ukienda kupewa mkopo anakupatia masharti mengi kamavile unamuomba moyo hakuna kijana aliyepewa mkopo licha ya baadhi yao kujitahidi kufuata masharti...
Sasa hivi ana gari mbili mpya ndani ya miezi mitano..
 
Sio mbaya
Maana kama huna kadi ya Ccm hupati juo mkopo. Wame kulana wenyewe
 
Wanaopendekeza mikopo itolewe ndiyo haohao wanakwenda kuipokelea upande nyuma unategemea watairudisha?
 
Hayo makundi mfano walemavu je kuna mazingira wezeshi kwa wao kujishughulisha ili waweze kurudisha hio mikopo au wanapewa tu kama zawadi
Ikiwa ni kupewa basi zingeitwa Bakhshishi , lakini ikiitwa mikopo maana yake ni lazima irejeshwe .
 
Pongezi kwa serikali maana hakuna afisa maendeleo aliyekonda kipindi hiki.....
Wa kwetu ukienda kupewa mkopo anakupatia masharti mengi kamavile unamuomba moyo hakuna kijana aliyepewa mkopo licha ya baadhi yao kujitahidi kufuata masharti...
Sasa hivi ana gari mbili mpya ndani ya miezi mitano..
Wacha weeee !!!!
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Amos Makalla amesema Jijini humo kwamba , zaidi ya Shilingi Bilioni 44 zilizotolewa na Halmashauri kama mkopo kwa Wanawake , Vijana na Walemavu hazijarejeshwa tangu utaratibu wa kukopesha makundi hayo ulivyoanza hadi sasa .

Hebu toeni maoni yenu kwenye hili .

Bali inafahamika kwamba Hela nyingi za mikopo hii ya Halmashauri zinapigwa na viongozi wa Halmashauri pamoja na viongozi wa Wilaya wa ccm , badala ya walengwa .

Kwa mfano , huko Temeke , RC Makalla alibaini shilingi mil 300 kukopeshwa kwa Mwenyekiti wa ccm wa Wilaya hiyo peke yake , na tena alizipiga bila kurejesha , Usanii wa kuiagiza TAKUKURU ichunguze ulifanyika , lakini ripoti ya uchunguzi huo hatukuwahi kusomewa hadi leo .

Mungu ibariki Tanzania ukipenda wewe mwenyewe
Pls happyxxx pitia uzi huu,aliyetoa tamko ni deployment wa Chama dola,honestly comment uzi huu
 
CCM ndiye adui mkubwa wa maendeleo nchi hii. Hiki chama, hawezi mtu kupata cheo chochote bila kutoa rushwa. Akipata uongozi ni lazima atafute njia ya kurudisha pesa aliyohonga, na faida juu.

Bila CCM kuondolewa madarakani, wananchi wakapeleka ujumbe wa wazi kwa viongozi na vyama vyote vya siasa kwamba wananchi wana nguvu ya maamuzi dhidi ya kiongozi au chama ambacho kimejengeka kwa misingi ya rushwa, Tanzania itaendelea kuwa nchi ya manung'uniko na maendeleo duni, huku wala rushwa na wevi wakubwa ambao ni CCM, wakiendelea kufurahi ndani ya bwawa la utajiri unaotokana na rushwa, ufisadina wizi.

Wevi, mafisadi na walaji wakuu wa rushwa nchi hii, ni au viongozi wa CCM au watu wenye mashilamano makubwa na CCM. Nje ya hapo, huyo mla rushwa/mwizi, atakamatwa mara moja. Kuwa kiongozi ndani ya CCM ni kama umepewa tiketi ya kuiba, kuhongwa na kufisadi kadiri ya upendavyo bila ya kuguswa na yeyote.
 
Back
Top Bottom