Rayvanny aweka video mtandaoni akiwa mahabani na Paula mtoto wa Kajala, Hamisa Mobetto adaiwa kuhusika kumlewesha na kumrubuni

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
5,363
2,000
Haya haya jamani mji umechafuka kwa mara nyingine tena...

photo_2021-02-14 16.13.03.jpeg


Wakati Kajala anaendelea kutrend kutokana na picha zake na Harmonize wakiwa Zanzibar ikidaiwa wawili hao ni wapenzi, leo hii yameibuka mapya baada ya Rayvanny kutoka WCB kupost video akiwa na Paula Mathysse ambaye ni mtoto wa Kajala na PFunk Majani wakiwa kwenye huba huku akimuita daddy na kumpiga makiss.Paula ambaye ni mwanafunzi aliyefaulu juzijuzi tu mitihani yake ya kurudia form 4, amekuwa akiandamwa mitandaoni kutokana na picha anazoweka hususani Instagram huku Kajala akilaumiwa kwa malezi mabaya hata na mzazi mwenzie, P Funk aliyesema "amemwachia mama yake mtoto maana amemshindwa".

KAJALA AZUNGUMZA

Kupitia mtandao wa Bongo5, Kajala amesema yafuatayo akimshushia mzigo wa lawama Hamisa Mobetto:

"Mimi ni mzazi ambaye namlea mtoto wangu kwa katika mazingira magumu sana kutokana na tofauti moja mbili tatu na baba mtoto wangu lakini mimi nilikuwa nikipambana na kumpa kila anachotaka mtoto wangu ili aweze kutimiza ndoto zake kama msichana mana kesho nitakuja kumtegemea.

photo_2021-02-14 16.12.51.jpeg


Lakini pia nilikuwa nikikumbana na changamoto tofauti tofauti ambazo zinamkumba paula kama msichana lakini shutuma nyingine huwa zinanijia mimi direct kama mzazi wa Paula sina budi ya kuzipokea na kukumbana nazo as long as Mungu anajua ukweli wangu ,jinsi gani namtunza mwanangu na kiasi gani napambana kwa ajili ya mwanangu,basi yote yaliyotokea ya kunichafua na kunifanya nionekane mbaya kwenye jamii huwa namwachiaga Mungu tu.

Ilikuwa tarehe 9 saa 6 mchana Hamisa Mobetto aliniomba kutoka lunch na mwanangu, sikuona haja kumkatalia kwa sababu nilijua yeye ni mzazi ambaye ana mtoto pia wa kike,kumbe ndo hiyo siku alitake advantage kwenda kumkutanisha na rayvanny kwa manufaa yake binafsi, walimrubuni mtoto mdogo kwa kumnywesha pombe, wamemrecord video Chafu sawa mimi ni Mnyonge siwezi wafanya Chochote basi Hata Muogopeni Mungu.

photo_2021-02-14 16.12.57.jpeg


Kama Mungu Hamumuoni Hamuiogopi serikali ? na kuvujisha video bila woga wakati ni mtoto mdogo anasubiria mwezi wa 6 kuingia form 5 siamini kama kuna alie juu ya sheria Katika taifa hili kama leongo lilikuwa ni Kudet Mtoto Mdogo ili Kutimiza Matendo Haya Machu Ya Kustaajabisha haitoshi mnampatia mtoto pombe na kumrecord Video chafu lengo lilikuwa nini Kama sio kuharibu Maisha ya msichana wa kitanzania ?

Nimeumizwa mno na Hamissa mzazi mwenzangu hata kama iwe paula ndo alimwambia anaenda kukutana na rayvanny kama yeye mzazi ange Vaa kiatu changu na kujiuliza kinachoenda kutokea ni kitu gani au kama ni mimi nafanyiwa hivi ningejisikiaje? nimeshikwa na bumbuazi sina nguvu naomba Mamlaka husika wanisaidie kwenye hili mana hili pigo ni lawazazi Wote Duniani.

Paula ni msichana mdogo sana ana ndoto zake leo hii ameharibiwa profile nzima Je mmefikiria maamuzi gani anaweza chukua huyu mtoto kuona video kama hizi zinatambaa mtandaoni kama akiamua kujinyonga je?

Naomba sana msaada serikali yangu na mamlaka husika juu ya hili. 🙏"

HAMISA AJIBU, AAHIDI KUCHUKUA HATUA ZA KISHERIA KWA KUCHAFULIWA
Katika ukurasa wake wa Instagram, Hamisa ameandika:

"Jamani hata kama HAMISA MOBETTO ndio jumba bovu lenu la kutupia takataka ifike mahala ifike ukomo. Siamini kama baada ya kukaa na kutafakari cha kuexplain kuhusu haya mmeona mimi ndio minaweza kuwa Damage Controller.

Kajala hiyo tarehe 9 mwanao aliniomba nimtoe Lunch, nikamwambia inabidi niongee na wewe kwanza, na nikakupigia ukaona ni sawa tu. Nilimtoa Lunch na muda wote nilikuwa naongea na wewe kwenye simu mpaka nimemrudisha hapo Gym kwako Mimi mwenyewe soon after lunch. Na huoni kama unaongea uongo hadharani bila woga? Siku ninatoka na Paula alikuwa na nywele hizo za kwenye videos?

Naomba nilaumiwe kwa kukubali ombi la kumpeleka mwanao lunch na si vinginevyo. Mimi ni mama, mfanyabiashara, mdau na balozi wa makampuni mbalimbali. Brand yangu nimeijenga kwa muda mrefu hivyo ningependa iheshimike na isichafuliwe kwa shutuma za uongo kama hizi.

Mimi pia ni mzazi na mtoto kwa mama yangu kama ilivo wewe. Nimeona nisafishe upepo mchafu huu uliouelekeza kwangu siku hii ya wapendanao, lakini zaidi you'll hear from my lawyer. Rest assured sitaliacha hili lipite bure, nafikiri itakuwa fundisho zuri na kwa wale woooooote ambao wamekuwa wakichafua jina langu kwa upuuzi wao."

HARMONIZE AZUNGUMZA NA RAY KUPITIA INSTAGRAM

“(RAY) MY YOUNG BROTHER AND 💙

Yafuatayo sitoyasema kama mimi ni mzazi wa Paula, no! Naandika kama mzazi niliye na mtoto wa kike (ZUREKHA). Lakini pia naandika kama msanii mwenzio.

Najiuliza tu, ulipata wapi ujasiri huu wa kutembea na mwanafunzi wa kidato cha 5 wakati ni wazi ya kwamba ni kosa la jinai ambalo hukumu yake sio chini ya miaka 30?

Lakini pia isitoshe unarekodi video ukiwa unakiss yaani unaonesha kwamba Serikali haiwezi kukufanya kitu. Nawaza, lengo lilikuwa kuonesha kuwa uko juu ya sheria?

Hebu angalia future ya mtoto wa watu umeiweka wapi kwa tamaa za siku 1? Kama kweli mlikuwa mnapendana, mko in-love video ilikuwa ya haja gani and lengo la kuvujisha nini?

Lakini pia Serikali itajiuliza una videos ngapi za watoto wa shule kama umeweza kuwa na hii na kuivujisha? Je, uliwaza wasichana wa rika lake ambao walikuwa mashabiki zako watafurahishwa na hichi kitendo cha kinyama? Maana kama leo umemfanyia mwenzao ni wazi kesho utawafanyia wao. Huoni kama umewapoteza mashabiki imara? Wataipata wapi nguvu ya kujirekodi ngoma zako na kupost ikiwa umemdhalilisha msichana mwenzao mdogo (Kingono)??

Je, kuhusu wazazi wenye watoto wa kike watakutazama sura gani? Usisahau kuna vijana wenzio ambao wana wadogo zao wa kike watakuonaje?

Kwanini usiendelee kuimba muziki tu? Huhitaji kujiingiza katika kuhatarisha maisha yako kama hivi. Tazama mifano ya wasanii wakubwa akina R. Kelly mpaka leo wanasota ndani kwa ajili ya mambo hizi za watoto wa shule.

Kama tatizo lilikuwa mimi kumpenda mama yake P na watu wengi wakavutiwa na sisi si ungetafuta mkubwa mwenzio? Why mwanafunzi tena wa miaka hii ya JPM?

Serikali ya leo iko macho sana maana watendaji wengi ni vijana. Je, watakubaliana na hili? Unadhani Waziri wa Sanaa, Michezo na Burudani atakalia kimya? Umejiuliza kama Mashirika yanayojihusisha na Haki za Wanawake watalifumbia macho? Mamlaka za elimu je?

Licha ya yote you are still my brother ila trust me hili suala limeniumiza kama kijana niliyebarikiwa mtoto.

Mungu akuvushe kaka, najua upo katika kipindi kigumu sana. Kama msanii mwenzio sina la kufanya zaidi ya kukuombea msamaha na huruma ya Serikali. #Pray4Rayvanny “
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom