Sababu ya Harmonize na Kajala kuachana (Hii ni fundisho kwa wadada na wamama wengine pia wenye tabia kama hizi)

Nobunaga

JF-Expert Member
Mar 22, 2019
1,169
4,985
Kwanza kabisa picha linaanza Harmonize alimpa Kajala password za simu zake na account zake za social media. Yani Kajala alikuwa na access ya every communication ya Harmo na Kajala alifanya same thing, alimpa Harmo password zake zote yani kulikuwa hakuna siri kati yako. Hapo mwishoni ndiyo Harmo alipobadilisha password zake za kila kitu na ndo mtafaruku ulipoanzia. Na sio kwamba alibadilisha password eti sababu ana cheat and so forth, nope, alikuwa anamtafutia sababu waachane.

Kwa kifupi baada ya kuishi na Kajala hii second time design kama Harmo kuna vitu aliviona akaamua hataki tena so akawa anatafuta sababu waachane. Yani ndiyo ile Dai alisema mimi kama sikutaki nitakupiga matukio mpaka uondoke mwenyewe, ndiyo alichofanya Harmo aliamua tu kumpiga matukio Kajala hadi akaweka mikono juu.

Moja ya vitu ambavyo Harmo alivichoka ni ile ya kitu kidogo tu Kajala anatishia kuachana na kuondoka, yani Harmo alijikuta kama mtumwa kila siku kumbembeleza Kajala. Mnaambiwa Kajala alikuwa anampelekesha Harmo kama gari bovu. Harmo simply got tired and wanted out ndiyo akaanza matukio kuchat na wanawake, kubadili password zake zote etc. Hata huo ugomvi wa mwisho yani ni kama Harmo alitafuta sababu ya kuachana na Kajala maana ilikuwa ni show ya Morogoro, kesho yake ndiyo siku waliyoachana rasmi.

Harmo alikuwa anaongea na simu makusudi mbele ya Kajala huku anajibebisha kwenye simu hataki kumwambia anaongea na nani ndiyo balaa likaanzia hapo. Kajala akapanick akasema naondokaaa, weeee mmakonde ikawa ndiyo kama kapewa nafasi sasa akamwambia sawa kabisa naomba uondoke sasa hivi, yani dakika hii usisubiri hadi kesho.

Kajala hakuamini Harmo anamfukuza ndiyo akaanza kulia hataki kuondoka. Na kaondoka kaenda kwake Harmo hajamtafuta wiki nzima ndo Kajala kupiga simu kwa Majey na Jembe anaomba wapatanishwe na Harmo akawagomea wote Jembe na Majey hataki kupatanishwa.

Issue nyingine iliyomboa Harmo ni Paula, yaani Harmo alichoka jinsi Paula anawapelekesha kuhusu hela. Unaambiwa Harmo kila siku ni kuambiwa na Kajala ampe Paula pesa sijui amfanyie hiki, amfanyie kile. Yani ni kama Harmo alikuwa anahudumia wanawake wawili. Kwa kifupi mmakonde alijiona anavyofilisika mchana kweupeee.

Unaambiwa kuna siku Paula aliwakalisha chini wazazi wampe pesa anunue kiwanja ajenge, Harmo akaona hii kitu haiwezekani Paula kaiwaza mwenyewe lazima mamake anamfundisha. Na unaambiwa Harmo asipotoa pesa kwa Paula Kajala akawa anamnunia inabidi abembeleze upyaaa.

So Harmo alishtuka kama vile Kajala ndiyo anataka vile vitu kupitia mgongo wa Paula. Yani ni vitu kama hivi ndiyo vilimboa ndiyo akaanza kumpiga Kajala matukio ili aondoke mwenyewe.

Nimeona sehemu wanasema sijui Harmo alimfumania Kajala. Harmo this time hajamfumania Kajala. Harmo alimfumania Kajala ile first time kabisaaaa na hakumfumania live alimfumania kwa message za simu kati ya Kajala na Paula, Kajala anamwambia Paula kampa Danga fulani namba yake yeye Paula so aongee naye amtulize, baada ya pale ndiyo Harmo alipomvulia nguo Paula.

Watu wengi walidhani ile issue ya Harmo kumtaka Paula ilikuwa ni sababu ya ugomvi wake na RayVanny hapana sababu kuu ilikuwa ni Kajala kuendelea na madanga yake.

So sababu kuu ya Harmo na Kajala kuachana this time ni Harmo ku realize kuwa Kajala sio wife material na kukubaliana na matokeo. By the way Kajala kaapa Miungu yooote kuwa harudishi range. lla ni hivi range moja lazima airudishe atake asitake maana haina jina lake. Ila hata ingekuwa mimi Kajala sirudishiii ng'oooo, tungeuwana ila gari sirudishiii.

Ushauri kwa wanawake wengine, mwanaume akikupenda sana don't push it. Usijisahau ukadhani umemuweka mkononi ukaanza kumpelekesha. Wakichokaga huwa hawaangalii nyuma. Hakuna mwanaume anaweza kukuacha vibaya kama mwanaume ambaye mwanzo alikuwa kama mtumwa kwako. Huwa wanajua kukusuprise mpaka huamini ni yeye aliyekuwa anakuona kama malaika.

Mwanaume akikupenda na wewe mpende usimchukulie kama fala.

Last but not least soon Harmo anaibuka na mtoto wa Kisomali.

Credit: Kwa Hisani ya Dada wa Taifa.
 
Mkuu hivi unajua deni la taifa saivi shng ngapi!?? Endeleeni kujadili ujinga nchi ishauzwa..
Wewe unayejua limekusaidia nini zaidi ya kuishi kwa stress zaidi ya bibi yako asiyejua kusoma?

Sometimes mambo mengine yapotezee tuu mkuu, hivi unajua Marekani wenyewe wanadaiwa deni kubwa kiasi gani?

Ukiona kwako kunafuka moshi jua kwa mwenzio kunateketea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom