Rangi za bendera ni ujumbe, uzalendo au urembo?

Unashirikisha masaburi au ubongo?Tofautisha bendera na zulia.Askari anashusha bendera kutoka ktk mlingoti na hashushi zulia.
 
Nadhani hadi iitwe bendera ya TZ ni kuwa iwe na mpangilio ule ule,
yaani kijani juu, njano, nyeusi,njano, hizi zinakata toka kona ya juu kwenye mlingoti na kushuka chini kwenye kona upande wa pili, na blue chini
lakini mkusanyiko wa rangi hizi kwa style nyingine sidhani kama ni halali kuita bendera ila ni rangi za bendera ya TZ,
kwa maana hiyo zile fito bungeni na kwenye zuria JNIA hazimaanishi bendera bali rangi nzuri zilizomo kwenye bendera yetu
 
Labda ungeleta maana kama ungeuliza kukanyaga rangi za bendera ya Taifa, heading ya thread yako imenistua kidogo nilifikiri imechukuliwa bendera yenyewe ndio ikawekwa chini na kukanyagwa.
 
Mkuu ile si bendera ni rangi tu katika zulia, nadhani haina tofauti na sasa unaona kuna ti shirt zina nembo ya bendera ya taifa watu wanavaa
 
Mkuu bendera ni ile inayopeperuka juu ya mlingoti,ambayo inashushwa na kupandishwa saa 12 iwe jioni au asubuhi,au ile wanayokabidhiwa wawakilishi wa nchi katika michezo n.k,jana kaondoka Miss TZ kwenda katika mashindano nikuulize ile aliyokabidhiwa ni bendera ya taifa au mfano wa bendera ya taifa ikitokea akashinda anaweza kutoka nayo akajifunika kama wenzetu wa kenya wanavyojifunika na kuringa na bendera yao?.kama zulia tu unakangayikiwa sasa kali ni ile ya jana katika tv tena TBC na ITV nafikiri chanel zote
 
Naona umejibiwa - Hata hivyo niongeze tu.

Watanzania tuliheshimu sana bendera na tukasahau utaifa. Enzi hizo ilikuwa ndra kukuta bendera ndogo au kubwa kwenye ofisi yoyote isipokuwa ya serikali. Watu wanapojivunia utaifa, huvaa alama za bendera ya taifa lao kama skafu, kitambaa kichwani na kushonea kwenye mashati nk. na hii haimaanishi dharau kwa namna yoyote ile.

Tunahitaji tujivunie utaifa wetu na kuutangaza.

Na hayo ni moja katika mabadiliko mema aliyoyafanya JMK.

Bendera si msahafu ni nembo tu. Watu wanaswaga na kuwarubuni watu waandamane wakakanyagwe kanyagwe itakuwa hizo rangi za bendera.
 
Wach masihara jomba, Inamaana hata underpants za bendera za USA or Brasil hujaziona Mkuu? Plz hebu "Chapa kazi" bana achana na hizi porojo!!!

Tofautisha nguo zinazotengenezwa na makampuni binafsi na pale ambapo serikali inaweka mapambo ya rangi za bendera kama vile mazulia, nk! Nionyeshe jengo la taifa moja lililo na zulia lenye mchoro wa bendera yake. Yani kama pale Oval Office ukute zulia ni bendera...hahaha! Waswahili bwana...taabu kweli! Ndio tatizo la kurithi vitu!
 
Kwa wale wenye macho makali na upembuzi wa picha za TV na za mnato mtakuwa mmetupia macho maeneo maarufu mawili hapa nchini. La kwanza ni kwenye njia za ndani ya ukumbi wa Bunge toka milangoni kuja mpaka kwenye eneo la Spika. Hapa kuna zulia ambalo limetengenezwa makusudi kufuata rangi za bendera ya Tanzania kwenye fito zake.

Sehemu ya pili ni uwanja wa ndege wa JNIA (Dsm) wakati ambapo anakuja kiongozi wa nje kwenye ziara ya kitaifa. Hapo huwa linatandazwa zulia jekundu lenye fito za rangi za bendera ya taifa pembeni pia.

Ninavyoamini na kufahamu ni kwamba bendera ndiyo kitambulisho kikuu cha nchi yoyote duniani na kwa utaratibu wa kistaarabu haipaswi kugusa ardhi "deliberately, accidentally or permanently". Ndiyo maana hata wakati inashushwa huwa askari anayeishusha anahakikisha haivuki hata usawa wa magoti yake kuelekea ardhini.

Je, ni busara gani kama si dharau kuruhusu watu bila kujali wadhifa gani wanao kuikanyaga bendera ambayo ndiyo sura ya taifa aidha wanapoteremka kwenye ndege au wanapoingia na kutoka Bungeni?

mbona kipa wa Everton anavaa magwana ya jeshi wakati wa kulinda lango?
 
Kule usa kuna vitambaa vya kufutia jasho'leso' napia kuna tishu na toilet paper ambazo nirangi za bendera ya taifa kuu duniani usa, zinatumika mpk kufutia vinyesi wao wanaona sawa na wanazidi kulitangaza taifalao wewe unashangaa zulia?
 
Na hayo ni moja katika mabadiliko mema aliyoyafanya JMK.

Bendera si msahafu ni nembo tu. Watu wanaswaga na kuwarubuni watu waandamane wakakanyagwe kanyagwe itakuwa hizo rangi za bendera.

Msahafu ni karatasi tuu ambalo unaweza ukatoa photocopy au kuuchoma moto, msahafu ...sahafu... what is mshahafu mbona unampa credit JMK kwa vitu vidogo sana!!!!!!!!!
 
Ni miaka takriban 50 ya uhuru ambayo tunaisherekea kwa mbwembwe na shamrashamra za aina yake lakini najiuliza swali moja muhimu je ni kweli tunaiheshimu bendera yetu ya taifa kama zamani?

Nakumbuka kulikuwa na milio ya filimbi kila asubuhi na jioni saa 12 iliyoashiria kupandishwa au kushushwa kwa bendera yetu tukufu, hapa kila mpita njia alisimama na kusitisha shughuli zake ili kutoa heshima kwa bendera yetu. Nina miaka kama kumi hivi sijashuhudia tukio la namna hii.

Nimejaribu kuchunguza muonekano wa bendera zetu katika afisi mbalimbali zinaonyesha kuwa na hali mbaya kama vile kupauka rangi na kuchanika. Kweli nchi inaenda mrama!

Wazee wenzangu naomba kujuzwa huu utaratibu wa watu kuheshimu bendera umefia wapi
 
Mimi naiheshimu bendera ya Manchester United FC kuliko bendera ya taifa.
 
Mkuu sasa kama heshima ya Taifa yenyewe imeshuka unategemea nini?!Taifa limepoteza mwelekeo!Taifa limekua kama gari moshi lililoacha reli!Sembuse bendera!Kipande cha kitambaa!
 
wewe haujui familia yako itakula nini.. Ukasimame kwasababu filimbi imepigwa. Heshima ya taifa kwanza ni mahitaji muhimu ya mwanadamu!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom