huku ni kutokujua maana ya uzalendo ukweli natamani kila mtanzania awe na bendera ya taifa nyumbani kwake kukosekana kwa uzalendo ndio kumefikisha taifa hapa nchi ambazo bendera ya taifa iko huru wanaipenda sana nchi yao maana wanajua uzalendo kuliko sisi ambao tuliaminishwa bendera utaiona kwenye ofisi za serikali au sehemu muhimu tu matokeo yake ndio haya hatuna uzalendo wa kutetea hata mali, zetu wananchi wetu nk.Lakini hairuhusiwi kupeperusha bendera ya taifa kwa mtu yoyote isipokuwa ofisi za serikali na nyumba za viongozi wakuu.
Mzalendo,
Asante sana. Nimefika salama Iringa. Na utalii nimeufanyia Ruaha Mbuyuni, kununua vitunguu!
Maggid,
Iringa.
Mawazo mazuri, ila punguza kupersonalize blog yako. Tunajua ni ya kwako, lakini habari zingine kama kueleza safari zako, unelala kwa nani, amekupa chakula gani, huyu ni nani na mnahusiana naye vp, zinatuboa tunaotegemea blog kupata habari. Hilo tu.Ndugu zangu,
Ni kweli, Watanzania tunaendekeza sana siasa za vyama na kuiasahau Tanzania yetu. Leo asubuhi sana niliianza safari yangu kutoa Msamvu , Morogoro kuja Iringa. Ni kawaida kando ya barabara kwenye makazi ya watu au vibanda vya biashara kukuta ikipepea, ama, bendera ya CCM, Chadema, CUF, Simba au Yanga. Lakini, ni nadra sana kuiona ikiperushwa bendera ya taifa letu.
Leo pale kijijini Mtandika, nje kidogo ya Ruaha Mbuyuni niliona kwenye banda moja la biashara ikipepea bendera ya taifa. Nilishtuka kuiona , niliguswa pia. Nlipunguza hata mwendo kumwangalia kijana yule aliyekuwa akifanya biashara yake ya vitunguu huku bendera ya nchi yake ikipepea.
Maana, bila shaka kijana yule kwa mapenzi ya nchi yake aliitafuta mwenyewe bendera ile ya taifa. Kwa vile, unapoona mahali kuna vijana wanapeperusha bendera za vyama yaweza kuwa na tafsiri ya ama, ni wapenzi wa vyama hivyo, na kuwa wamezitafuta wenyewe, au kuna kada wa chama husika aliyekuja na kugawa bendera hizo kwa vijana hao.
Ndio, tunahitaji kufanya jitihada za kuwafanya watu wetu waipende nchi yao waliyozaliwa, kutoka ndani ya mioyo yao. Na moja ya jitihada hizo ni kuwapa maarifa yatakayowawezesha kujitambua, kujiamini na kuthubutu.
Maggid,
Iringa.
0788 111 765.
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
Mawazo mazuri, ila punguza kupersonalize blog yako. Tunajua ni ya kwako, lakini habari zingine kama kueleza safari zako, unelala kwa nani, amekupa chakula gani, huyu ni nani na mnahusiana naye vp, zinatuboa tunaotegemea blog kupata habari. Hilo tu.