Rais Yoweri Museveni akiwa na umri wa miaka 79 na miaka 37 ya Urais wa nchi ya Uganda

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,411
11,061
Mwasibota Bazzukulu!

Ndugu Rais Yoweri Kaguta K Museveni aliingia madarakani kama Rais nchini Uganda kwa njia ya mtutu wa bunduki, kama muasi dhidi ya serikali ya Milton Obote mwaka 1986, wakati huo Bwana Museveni akiwa na umri wa miaka 42, tangu wakati huo amekuwa madarakani kama Rais wa Uganda kwa miaka 37.

Amevunja rekodo ya kuwa Rais aliekaa madarakani eneo la nchi za Afrika Mashariki.

Ni nadra sana Marais kuvuka miaka 40 madarakani, mpaka sasa nadhani record kwa Afrika inashikiliwa na Rais Paul Bia wa Cameroon mwenye miaka 40+ madarakani.

Kumekuwepo na Tetesi kwamba afya yake si njema sana iko on and off, anawaza kuondoka ila kigugumizi na Giza Nene limetawala japo mpango mkakati wa mwanae Muhoozi mzaliwa wa Jiji la DSM miaka ya 80 aliyekulia Sweden kwa miaka kadhaa.

Ndani ya miaka hii miwili 2023-2025 tutashuhudia mageuzi katika kiti cha Urais nchini Uganda.

Madaraka yanalevya kama ilivyo shibe mwanalevya.

Tusubiri yajayo East Africa jijini Kampala.

UGA wa kikanda

Wadiz
 
Back
Top Bottom