Rais wa Zanzibar Dkt.H.Mwinyi kumwapisha Mhandisi Zena Ahmed Said kuwa Katibu MPYA wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi ni tarehe 02-01-2021

Elisha Sarikiel

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
889
1,515
Updates :-
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Mhandisi Zena Ahmed Said kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na katibu Mkuu Kiongozi, akichukua nafasi ya Dkt. Abdulhamid Yahya mzee aliestaafu. Hafla hiyo ya kiapo imefanyika Ikulu Jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Kitaifa, akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, Mawaziri, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Dk. Abdulhamid Yahya Mzee pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid.

Rais Dk. Mwinyi amemuapisha kiongozi huyo kushika wadhifa huo baada ya kumteua Januari mosi mwaka huu, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 49 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Zena Ahmed Said alikuwa Katibu mkuu Wizara ya Nishati katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika hatua nyingine, akizungumza na vyombo vya habari, Mhandisi Zena alisema atajitahidi kufanya kazi zake kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliopo ili kufikia matarajio ya Wazanzibari. Pia atafuata kanuni na sheria na kujiongeza katika ubunifu ili aweze kufikia malengo, huku akiahidi Serikali kuangalia kwa undani umuhimu wa ajira kwa vijana.

Aidha alitowa wito kwa wanawake nchini kote kujiamini na kufanya kazi zao kwa weledi pamoja na kuwataka kufanya shughuli zao kwa kuzingatia wakati na nafasi zao, sambamba na kutosubiri kusaidiwa. Mhandisi Zena Ahmed Said, anakuwa mwanamke wa kwanza nchini kushika wadhifa wa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, tangu Mapinduzi ya 1964.






1609581942006.png

1609582001528.png



1609582043235.png


1609582081643.png


===========================================================================================================

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi; siku ya Jumamosi tarehe 02/01/2021 saa 05:00 mchana atamuapisha Mhandisi Zena Ahmed Said kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi.

Taarifa kutoka Ikulu habari Zanzibar.


Image may contain: 1 person, sitting


 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi; siku ya Jumamosi tarehe 02/01/2021 saa 05:00 mchana atamuapisha Mhandisi Zena Ahmed Said kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi.

Taarifa kutoka Ikulu habari Zanzibar


Image may contain: 1 person, sitting


View attachment 1664521
Mheshimiwa Mhandisi Zena Ahmed Said
Duh huyu ni Mhandisi Dah Chombo kinono hiki.
 
Mbona anateuwa machotara watupu kuna nini hapa au ndo kashirikiana na maalim seif wanataka kutimiza adhma yao kuleta waarabu Zanzibar
 
Mbona anateuwa machotara watupu kuna nini hapa au ndo kashirikiana na maalim seif wanataka kutimiza adhma yao kuleta waarabu Zanzibar
Wacha ubaguzi wewe! Mzanzibari ni mzanzibar tu. Amezaliwa na amekulia zanzibar. Mbona hukuuliza Rais yeye mwenyewe na asili yake? Mzee rukhsa ametokea wapi?
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi; siku ya Jumamosi tarehe 02/01/2021 saa 05:00 mchana atamuapisha Mhandisi Zena Ahmed Said kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi.

Taarifa kutoka Ikulu habari Zanzibar


Image may contain: 1 person, sitting


View attachment 1664521
Mheshimiwa Mhandisi Zena Ahmed Said
Utakuta hata ukimuambia adizaini beam tu hajui. Alafu anajiita injinia.

Huyu ni political engineer.
 
Ametoka Ruangwa sio mzanzibar amepandikizwa kule kuwatawala
Rangi yako halisi ni hii sasa 'kupitia hiyo comment'

Wewe ndiye unayehusudu waarabu, na matamanio yako ni kuona waarabu wana take over Zanzibar (kisiasa na kiutumishi katika serikali ya mapinduzi)

Na unaumia unapoona wazanzibari weusi wanaendelea kutake over
 
Utakuta hata ukimuambia adizaini beam tu hajui. Alafu anajiita injinia.

Huyu ni political engineer.
Kafanya kazi Barabara ya Wazo Hill(Tegeta) mpaka Bagamoyo Km 43 tena kama Works Supervisor

Alikua na Interest ya Kusoma Mechanical Engineering ila akaamua kwenda Civil Engineering kwakua chuo alichopata cha Mech ilibidi ajifunze kituruki kwanza. So huyu uhandisi ni passion iko kwenye damu

Kasoma ubungo National akachaguliwa Jangwani O-level na A-level miaka ile walikua wanachukua cream babu so sio wa kumchukulia poa

Mpemba aliyehamia Tanga na baadae Dar alikokulia, na kazi kafanya TANROSDS kabla ya kuwa RAS Tanga wakat wa JPM na baadae akawa karibu Mkuu wa wizara ya Nishati mpaka alivyoteuliwa kurudi Zanzibar jana

Huyu sio mwanasiasa usimchukulie poa
 
Back
Top Bottom