Maneno Mazito aliyoyasema Mhandisi Zena Ahmed Said, Katibu Mkuu Kiongozi wa SMZ Katika Siku ya Wanawake Duniani

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,906
945
"Kauli Mbiu ya Wekeza kwa Mwanamke Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii. Huwezi kutoa usichokuwanacho. Wanawake ndiyo watoaji wakubwa wa mambo mengi kuanzia watoto wanavyozaliwa" - Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mhandisi Zena Ahmed Said

"Kama tutakuwa na Wanawake wanaoingia kwenye familia wakiwa hawana vitu vya msingi vya kwenda kutoa kwa watoto wakike na kiume basi tunaanza kutengeneza msingi usio imara sana kwa watoto na hawa watoto ndiyo wanakuja kuwa viongozi mbalimbali kesho" - Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mhandisi Zena Ahmed Said

"Kuwekeza kwa Wanawake ni muhimu sana kwasababu watakapokuwa wana Mambo mazuri vichwani mwao na mioyo yao wataenda kutengeneza msingi mzuri wa Taifa letu maana wao ndiyo Programmer wa watoto wote" - Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mhandisi Zena Ahmed Said

"Wataalam wanasema mtoto wa tangu kuzaliwa mpaka miaka 5-7 anakuwa kama Sponge, ana absorb vitu vingi anavyopewa. Akipewa ujinga au insecurities anapokea kama kilivyo. Utakachomfundisha ndicho atakachokibeba" - Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mhandisi Zena Ahmed Said

"Tunahitaji mwanamke awe na "Good Emotional Intelligence, aweze ku manage vizuri Stress na Social Intelligence ili ku interact na watu vizuri. Akiwa hivyo hata watoto wake atajua namna ya kuwalea vizuri kwasababu watu wamelelewa kwa mazingira mbalimbali na huwezi kumhukumu mtu kwa kumuangalia tu" - Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mhandisi Zena Ahmed Said

"Mwanamke anatakiwa kujengewa uwezo wa kuwasilina (Communications Skills) na Kuwekeza katika utatuzi wa migogoro (Disputes Resolution), watoto wakigombana nyumbani Mwanamke ndiyo wa kwanza kuingilia kati, pia ajengewe uwezo wa kupanga bajeti kwa kuweka vipaumbele vya familia" - Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mhandisi Zena Ahmed Said

"Siyo siri tena, Wanawake ni nguzo muhimu katika kuchangia maendeleo ya Taifa na jamii kwa ujumla. Sisi tuliopata dhamana ya kulitumikia Taifa katika Utumishi wa umma tunatakiwa tujitathimini na kupima namna tunavyotekeleza Majukumu yetu ili kuchangia maendeleo ya Taifa" - Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mhandisi Zena Ahmed Said

"Wanawake tuliopewa dhamana ya kuongoza tutaweza kuwa na mchango kwenye Taifa kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi, ubunifu, uaminifu na uadilifu mkubwa ili kufikia malengo binafsi, Taasisi na Taifa kwa ujumla" - Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mhandisi Zena Ahmed Said

"Tunatambua Mchango wa Serikali zetu mbili, zimeweka vipaumbele mbalimbali kuhakikisha bandari zetu zinafanya kazi kwa ufanisi. Niwaombe kuboresha miundombinu ya bandari, kutumia mifumo ya kisasa ya TEHAMA na kununua vitendea kazi bora vya kuhudumia Meli na Shehena na kuboresha maeneo yetu ya utendaji kazi" - Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mhandisi Zena Ahmed Said

Aidha, Mhe. Mhandisi Zena Ahmed Said amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mkeli Mbossa kwa kuhakikisha wakinamama kuwa sehemu ya mafanikio ya Bandari pamoja na mikakati yake ya kuwajengea uwezo Watumishi Wanawake wa TPA.

Pamoja na mambo mengine Mhe. Mhandisi Zena Ahmed Said amewapongeza Watumishi Wanawake wa TPA kwa kutoa kiasi cha shilingi Milioni 60 kusaidia jamii ya Watu wenye uhitaji kwa kuwa kwa kufanya hivyo kunamfurahisha Mwenyezi MUNGU na kuunga mkono Serikali katika kuboresha huduma kwa jamii.

GIXoXMLWwAAoTMQasqw.jpg
GIXoXMQXcAAMHH9asqwz.jpg
GIXoXMNWgAA5WBHcvfdrt.jpg
GIXoXMPWAAAVfAvtyujhg.jpg
 
Back
Top Bottom