Rais Samia; Urais wa nchi ni mambo makubwa

CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,072
2,000
Habari wana JF,

Binafsi nafurahia uongozi wako Mh Rais Samia, lakini napenda kutoa mtazamo tofauti ili kuboresha kwa kuwa bado una muda.
Rais wangu, asikudanganye mtu, Uongozi wa Nchi ni mambo makubwa, ni juu ya hatma ya kesho, sio leo tu, ni juu ya leo na vizazi vijavyo.

Nchi hii bado ni maskini sana, askidunganye mtu. Wanachi wetu bado ni fukara wa kutupwa, asikudanganye mtu yeyote.
Ninatembea kila kona ya Tz, wanachi wako bado ni fukara sana. Kupiga siasa pekee hakutawasaidia wananchi wako.

Hivi mheshimiwa Rais unajua zipo wilaya, % kubwa ya watu wake hawawezi hata kulipia hela ya kufungua jalada hospitali?
Ni Elfu 1 tu, lakini hana na hapo ni ugonjwa. Anaumwa kwelikweli!

Ngoja nizungumze kidogo kama Nyerere.

1. Tunataka Rais anayejua hali halisi za wanachi wake, kwamba Watanzania bado ni maskini sana.
Bado tu fukara sana. Bahati mbaya ni kwamba mfumo wetu wa kiuongozi unawatenga sana nyinyi mliojuu na sisi wa huku chini.
Ni hakika ukiwa Rais nchi hii huwezi abadani kuhisi shida za watu wako. Shida MFUMO. Shida WAPAMBE.
Watakwambia aaah!, mambo yako sawa Mheshimiwa.

Nitoe mfano halisi kwenye Uongozi wako.

Jana ukiwa na wanawake kwa mara ya pili, binafsi, nimekusikia ukisemea swala la maiti kuzuiwa ktk hospitali za umma ili kulipwa gharama za matibabu.

Ukasema (na uliwahi kusema), Wizara iangalie, labda mgonjwa awe anapewa bili yake kidogo kidogo kadri anavyoendelea na tiba!
MOYO WANGU UNAUMIA SANA.

Hebu Mh Rais yachimbe haya mambo kiundani. Wajue wananchi wako kiundani, itakusaidia. Wananchi wako ni fukara sana, asikudanganye mtu!!

Tatizo sio bili kidogo kidogo! Okay tuseme amelazwa, siku ya pili akapewa bili akashindwa kulipa yote, je madaktari wasitishe huduma ili alipe kwanza?

Hivi maskini anayevumilia maumivu ya kichwa asiweze kununua panadol, ndiye wakupewa bili kidogo kidogo!

Wapo watakaonishambulia hapa, kwamba unataka Rais asemeje, watibiwe bure?! Okay wasikilize tu.

2. Tunataka Rais anayejua kwamba UJINGA, UMASKINI na MARADHI sasa ni maadui waliokubuhu.

Unaogopa nini kuvunja-vunja mfumo wa elimu yetu huu, uutengeneze upya?

Tuna elimu ya ajabu, hata vitabu wanavyosoma watoto wetu leo havichangamshi akili hata kidogo.

Halafu hii ya kujenga shule moja ya wasichana kila mkoa, kwamba tunajaribu au? Hebu Mama acha Legacy, usijaribu-jaribu.

Tunahitaji Rais anayewajua Watanzania wote, kuanzia Machinga, Wakulima, Matajiri, Wafanyabiashara, Wafanyakazi, Wawekezaji, Rika zote, Rangi zote, Jinsi zote, Kabila zote, n.k.

Tunataka Rais anayejua kwa dhati kuwa huu ni "uzandiki" na huu ndio "ukweli", na akatae waziwazi uzandiki wowote ule hata kama umeletwa na rafiki/ndugu yake.

Tunataka Rais anayejua shida za watu wake, 'Matajiri na Maskini', maana wote tajiri na maskini wana shida/mahitaji.
Anayejua kuwa wote wanatakiwa kusaidiwa bila upendeleo, wala kukanyaga mgongo wa mwingine.

Naomba hii iwe part 1

Asante Mh Rais kwa usikivu wako.
 

CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,072
2,000
Siku mtu huwezi hata kutoa constructive criticism humu bila ya kuambiwa unamchukia Samia!

SMH
Umesema kitu kikubwa sana.

Binafsi sielewi kwa nini ukitoa hoja juu ya Mh Rais,, unaambiwa "Unateseka nini wewe SukumaGang, mara MATAGA".

Watu wafuatilie hata nyuzi zangu na koment zangu, nilimkosoa sana Hayati. Sasa iweje nongwa kumkosoa Rais wetu wa awamu ya sita?
 

kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
4,024
2,000
Naungana na wewe nchi ina matatizo makubwa sana hasa ukishuka wilayani kwa wananchi wa hali ya chini. Isipowekwa mikakati madhubuti na ufuatiliaji makini hali itakua mbaya sana huku chini. Wiki mbili zilizopita nimepita kijiji kimoja nimekuta zahanati imefungwa muuguzi na tabibu wote wameenda semina nilijiuliza maswali mengi sana hela za dawa hakuna ila hela za semina zipo na niliambiwa wanakimbizana kumaliza hela kabla mwaka wa serikali haujaisha.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,210
2,000
Naungana na wewe nchi ina matatizo makubwa sana hasa ukishuka wilayani kwa wananchi wa hali ya chini. Isipowekwa mikakati madhubuti na ufuatiliaji makini hali itakua mbaya sana huku chini. Wiki mbili zilizopita nimepita kijiji kimoja nimekuta zahanati imefungwa muuguzi na tabibu wote wameenda semina nilijiuliza maswali mengi sana hela za dawa hakuna ila hela za semina zipo na niliambiwa wanakimbizana kumaliza hela kabla mwaka wa serikali haujaisha.
Tatizo hawalipwi vzr na wana madeni kwenye taasisi za fedha nao ni binadamu
 

CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,072
2,000
Tumpe muda,kumaliza hawa maadui inahtaji muda
Atakuja Rais mwingine nae atasema hivohivo.

Asikudanganye mtu, ukipewa kuongoza nchi miaka 10 tu, inatosha kuleta mapinduzi makubwa na neema kwa wananchi wako.

Shida viongozi wetu wanarudia makosa hadi ya watangulizi wao.

Mfano:-

Kikwete aliwapiga watu wa Mtwara kwamba watake wasitake 'gesi' lazima itoke, eti kwa manufaa ya Tz. Leo tumefaidika nini na hio gesi.

Hayati JPM nae akawapiga 'korosho' eti lazima zitoke/serikali inunue. Leo tumepata nini kwa maamuzi hayo.

Mama awe makini, uongozi wa nchi ni mambo makubwa.

Dira ni ipi. Leo wanawake, kesho vijana. Mapinduzi unaya-frame kupitia angle ipi?
 

MPIGA ZEZE

JF-Expert Member
May 16, 2011
2,544
2,000
CWR2016 umetoa hoja nzuri na inayohitaji tafakuri. Mojawapo ya chanzo cha ufukara unaozungumzia na ambao ni kweli kabisa ni UFISADI (sio kwa maana ya 'kamusi' ya CCM) bali katika maana halisi ya dhana ya kleptocracy ('wizi' wa mali ya umma uliohalalishwa na walioshikilia madaraka). Kwa mfano ni mishahara na posho za waheshimiwa wabunge.

BUNGE ni kleptocracy iliyosukwa wakati wa awamu ya Mkapa. Hii ningeiita SUSTAINABLE KLEPTOCRACY ambapo wanasiasa watawala wanajihakikishia wao na familia zao zinaneemekea (chukua mfano wa Jakaya Kikwete, leo hii anapata mafao ya ustaafu wa urais, mtoto ni mbunge, mke ni mbunge,na soon hata mjukuu atakuwa mbunge; Hayati Sitta, alikuwa mbunge na mama mbunge, kama sikosei wanamwandaa mtoto kuja kuchukua mikoba). Haya marupurupu watu wanayolalamikia, hayakutokea kwa bahati mbaya!

Wakati ule wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana tulipoambiwa hapa JF kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CDM - TL -aliomba apelekewe maswali ambayo angekuja kuyajibu (hatukupewa mrejesho), mimi nilimuuliza swali moja kuwa je akipata nafasi ya kuwa rais alikuwa na mpango gani wa kufutilia mbali UFISADI unaopitia katika hiki kitu kinaitwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz? Kinachofanywa na hii institution inayoitwa BUNGE katika dimbwi la ufukara wa waTz ni laana!
 

CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,072
2,000
Umewahi kuona wapi Rais wa nchi kwenda kugawa mashuka 200 hospitali serious?
Nilishangaa, halafu anasema eti kidogo kidogo tunaenda.

Na hii ya kujenga shule moja ya Bweni ya Wasichana kila mkoa.

SERIOUS?

Ni kama anafanya 'favour' au anatoa zawadi.

Tunawezaje kupaka rangi tatizo kubwa tena ktk 'level' ya Urais?

Mambo mengin hata washauri wake waone aibu.

Hiyo ya mashuka 200 haikutakiwa hata kutangazwa in public.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,210
2,000
Nilishangaa, halafu anasema eti kidogo kidogo tunaenda.

Na hii ya kujenga shule moja ya Bweni ya Wasichana kila mkoa.

SERIOUS?

Ni kama anafanya 'favour' au anatoa zawadi.

Tunawezaje kupaka rangi tatizo kubwa tena ktk 'level' ya Urais?

Mambo mengin hata washauri wake waone aibu.

Hiyo ya mashuka 200 haikutakiwa hata kutangazwa in public.
Huyu ni mswazi hana issue sn bora apige taraabu zake taratibu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom