Rais Samia; Urais wa nchi ni mambo makubwa

Yote na yote yanasababishwa na vitu vitatu, umasikini, ujinga na malazi na hapo Raisi yupo sawa kuna vitu unatakiwa kuwa strong Ili kuvitatua ukifanya mfumo wa kubembeleza watu wanabetweka mfano sasa hivi wanawake wameamua kweli kupigania masilahi yao yawe vizuri kwa njia ya upendeleo au kwa njia za kiungwana lakina wanaume waliopewa jukumu la kuwa vichwa wao wamekaa kimya hata kuomba shule za ufundi ziwe za jinsia za kiume kama wanawake wanavyofanya.

Sasa hapo wakulaumiwa ni hao walioamua kukaa kimya, na pia uwajibikaji umepungua sana kwa vijana na wababa ukisema wapewe huduma bure kesho unakuta wanaume wote bar wakisherekea hawana jukumu la kuuguza, ukisema elimu bure hivyo hivyo inakuwa hivyo wanaume tuamuke kuwajibika na kudai fursa zitakazo inua vipato vya familia sioni dunia ya Leo bado watu wanafanya kazi mchana tena masaa 8 kinachotakiwa ni kazi za shift walioingia Asubuhi watoke jioni na jioni watoke Asubuhi, iwe shule, hospital, umeme au gesi, kujenga, usafirishaji, viwandani, hata michezo hivyo hivyo kusiwepo muda wa kupoteza hapo hizo gharama za kulipa huduma zitapatikana tena kwa gharama ndogo maana vitu vyote vitazalishwa kwa wingi na nchi yote itakuwa nuru muda wote hata mabaya yatakaa mbali.
 
CWR2016 umetoa hoja nzuri na inayohitaji tafakuri. Mojawapo ya chanzo cha ufukara unaozungumzia na ambao ni kweli kabisa ni UFISADI (sio kwa maana ya 'kamusi' ya CCM) bali katika maana halisi ya dhana ya kleptocracy ('wizi' wa mali ya umma uliohalalishwa na walioshikilia madaraka). Kwa mfano ni mishahara na posho za waheshimiwa wabunge.

BUNGE ni kleptocracy iliyosukwa wakati wa awamu ya Mkapa. Hii ningeiita SUSTAINABLE KLEPTOCRACY ambapo wanasiasa watawala wanajihakikishia wao na familia zao zinaneemekea (chukua mfano wa Jakaya Kikwete, leo hii anapata mafao ya ustaafu wa urais, mtoto ni mbunge, mke ni mbunge,na soon hata mjukuu atakuwa mbunge; Hayati Sitta, alikuwa mbunge na mama mbunge, kama sikosei wanamwandaa mtoto kuja kuchukua mikoba). Haya marupurupu watu wanayolalamikia, hayakutokea kwa bahati mbaya!

Wakati ule wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana tulipoambiwa hapa JF kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CDM - TL -aliomba apelekewe maswali ambayo angekuja kuyajibu (hatukupewa mrejesho), mimi nilimuuliza swali moja kuwa je akipata nafasi ya kuwa rais alikuwa na mpango gani wa kufutilia mbali UFISADI unaopitia katika hiki kitu kinaitwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz? Kinachofanywa na hii institution inayoitwa BUNGE katika dimbwi la ufukara wa waTz ni laana!
Mkuu umezungumza hoja nzito sana.

UFUKARA wa nchi hii umejengwa kisiasa sana.

Na kuna mwanasiasa anaweza akaamka akasema watanzania ni wavivu. Ni dharau sana.

Niliwahi kwenda Njombe, na Bukombe (Geita) huko watu ni mafukara mpaka unahisi ni laana.

Nilikuwa Geita huko mama mmoja akampeleka mwanae(wa mwaka mmoja) hospital, akaambiwa dawa hamna akanunue, nikampa elfu 20.

Halafu wanasema matibabu bure. Unatamani kulia nchi hii.

Na kinamama wengi wanasema ni kama haijawahi kuwa bure.

NCHI HII...
 
Uongozi ni Mamlakaa ,uongozi ndio dira ya mafanikio,uongozi unahitaji ujasiri ,kuthubutu ,maamuzi ya faida kwa wotee!
Mama asimame. Tz inamtazama yeye kwa sasa.

Najua uongozi sio rahisi. Lakini ana bahati ana support ya wananchi ktk huu mwanzo.

Aongoze mambo makubwa.
 
Yote na yote yanasababishwa na vitu vitatu, umasikini, ujinga na malazi na hapo Raisi yupo sawa kuna vitu unatakiwa kuwa strong Ili kuvitatua ukifanya mfumo wa kubembeleza watu wanabetweka mfano sasa hivi wanawake wameamua kweli kupigania masilahi yao yawe vizuri kwa njia ya upendeleo au kwa njia za kiungwana lakina wanaume waliopewa jukumu la kuwa vichwa wao wamekaa kimya hata kuomba shule za ufundi ziwe za jinsia za kiume kama wanawake wanavyofanya.

Sasa hapo wakulaumiwa ni hao walioamua kukaa kimya, na pia uwajibikaji umepungua sana kwa vijana na wababa ukisema wapewe huduma bure kesho unakuta wanaume wote bar wakisherekea hawana jukumu la kuuguza, ukisema elimu bure hivyo hivyo inakuwa hivyo wanaume tuamuke kuwajibika na kudai fursa zitakazo inua vipato vya familia sioni dunia ya Leo bado watu wanafanya kazi mchana tena masaa 8 kinachotakiwa ni kazi za shift walioingia Asubuhi watoke jioni na jioni watoke Asubuhi, iwe shule, hospital, umeme au gesi, kujenga, usafirishaji, viwandani, hata michezo hivyo hivyo kusiwepo muda wa kupoteza hapo hizo gharama za kulipa huduma zitapatikana tena kwa gharama ndogo maana vitu vyote vitazalishwa kwa wingi na nchi yote itakuwa nuru muda wote hata mabaya yatakaa mbali.
Basi Mh Rais asimamie haya.

Kama ni kazi usiku na mchana aseme. Uletwe mpangokazi wa haki, kiufupi asimamie mageuzi makubwa. Sio vijimambo mambo. Atatue mambo kwa upana.

Anaogopa nini?
 
Tusiishie kulalamika tu. Kosoeni kisha toeni ushauri nini kifanyike maana hata yeye alizungumza ataunda kamati ambayo itatoa ushauri wa namna nzuri ya kufanya.
 
Mkuu umezungumza hoja nzito sana.
UFUKARA wa nchi hii umejengwa kisiasa sana.
Na kuna mwanasiasa anaweza akaamka akasema watanzania ni wavivu. Ni dharau sana.
Niliwahi kwenda Njombe, na Bukombe (Geita) huko watu ni mafukara mpaka unahisi ni laana.
Nilikuwa Geita huko mama mmoja akampeleka mwanae(wa mwaka mmoja) hospital, akaambiwa dawa hamna akanunue, nikampa elfu 20.
Halafu wanasema matibabu bure. Unatamani kulia nchi hii.

Na kinamama wengi wanasema ni kama haijawahi kuwa bure.

NCHI HII......
Ni Jambo jema ulimsaidia huyo mtoto, lakini baba wa mtoto alikuwa wapi? Unajua sasa hivi kuna wanawake wanazaa tu hata bila waume? Sasa hiyo ni sawa kama siyo kuongeza mizigo kwa Taifa? Tuweke displine Kwanza kwenye jamii zetu Ili kuondoa hayo mambo yanaoongeza unyonge wa mtu na familia, sasa hivi imekuwa sifa mtu kujiita mnyonge au masikini wakati makosa ni yake yeye kila mmoja aangalie wapi anakosea Kama yeye kujiinua kiuchumi, kinachotakiwa sasa nikuomba gharama za vitu zipunguzwe Ili wanapambana na msingi wa dunia wanufaike maana msingi wa Mungu ni kazi Ili tupate vipato, sasa tusilalamike kulipa gharama maana ni wajibu ila tuombe gharama zipunguzwe maana vipato vyetu ni vidogo.
 
Mimi nitakua wa kwanza kukuunga mkono..! Asilimia kubwa ya sisi watanzania sio masikini tu bali ni mafukara. Hivyo Mhe. Raisi asidanganywe kama hali ni shwari. Hali si shwari kabisa.
Asante kunielewa.
Nimetembea Mara, Simiyu, Mwanza, Geita,Kagera, Tabora, Shinyanga, Pwani, Iringa, Njombe, Mbeya, Kigoma, Lindi, n.k tena wilaya za ndani ndani. Aisee WaTz ni hoibintaaban. Kuna wilaya huwa mpaka 'nasali kwa Mungu'. Ni nini hiki. Ni ufukara uliopitiliza.

NCHI HII......
 
Basi Mh Rais asimamie haya.
Kama ni kazi usiku na mchana aseme. Uletwe mpangokazi wa haki, kiufupi asimamie mageuzi makubwa. Sio vijimambo mambo. Atatue mambo kwa upana.

Anaogopa nini?
Uko sawa kabisa ndicho nilichomaanisha, kwa mfano hao vijana wanaokwenda kuongea na Raisi wanatakiwa ajenda yao kuu iwe, sisi ni vijana tunanguvu na tupo wengi tupo tayari kufanya kazi sasa Raisi tuongezee ajira zifanyike mchana na usiku Ili zitoe matunda mengi na sisi vijana tupate vipato tujiandae kujenga Taifa tukiwa vijana lakini cha ajabu vijana wataenda kulialia kwa Raisi kwamba wao ni dhaifu wanahitaji kusaidiwa nguvu.
 
Ndugu yangu, shida zetu, umaskini wetu na kila aina ya matatizo tuliyonayo hayawezi kumalizwa au hata kupunguzwa na Madam SSH.

Kwa kifupi hakuna Rais yeyote yule anayeweza kubadilisha maisha yetu isipokuwa mmoja tu....

Huyo ni MFALME AJAYE, yaani YESU KRISTO. Yeye atakapokuja atamaliza matatizo YOTEE!!.
 
Umesema kitu kikubwa sana.
Binafsi sielewi kwa nini ukitoa hoja juu ya Mh Rais,, unaambiwa "Unateseka nini wewe SukumaGang , mara MATAGA".
Watu wafuatilie hata nyuzi zangu na koment zangu, nilimkosoa sana Hayati. Sasa iweje nongwa kumkosoa Rais wetu wa awamu ya sita?!
Umeelezea vizuri. Hilo la elimu ni kweli kabisa. Lakini siyo elimu tu. Tanzania inahitaji kujitathmini upya. Tujiulize mbona kila rais anayeingia hafanikiwi na akimaliza muda anayeingia anakuwa kama anaanza upya? Jibu ni kuwa system yetu ya uongozi siyo nzuri kabisa. Tunatakiwa tufumue fumue kila kitu tuweke mfumo mzuri zaidi. Wanasiasi wamekuwa wengi na wako kila mahali. Ndiyo wanafanya kila jambo na mbaya zaidi wengi ni vilaza na matapeli waliokimbilia huko kwa sababu tu ni mabingwa wa kupiga gumzo. Tufumue mfumo wetu viongozi wawe wachache na asilimia ndogo tu wateuliwe na rais. Bila kufanya hivyo mama Samia hatakuwa na jipya tena atachokwa haraka sana.
 
Asante kunielewa.
Nimetembea Mara, Simiyu, Mwanza, Geita,Kagera, Tabora, Shinyanga, Pwani, Iringa, Njombe, Mbeya, Kigoma, Lindi, n.k tena wilaya za ndani ndani. Aisee WaTz ni hoibintaaban. Kuna wilaya huwa mpaka 'nasali kwa Mungu'. Ni nini hiki. Ni ufukara uliopitiliza.

NCHI HII......
Umenifanya nikumbuke vijiji fulani mkoa wa Morogoro (navihifadhi kwa majina) magari hayafiki huko na watoto wadogo wanasikia tu kuna vitu vinaitwa magari hawayajui. Pia kwenye vijiji vya delta ya mto Rufiji hali ndio hiyo. Kwenda shule na hospitali lazima uvuke mto, hamna umeme pia. Na hawa kipindi cha uchaguzi wanapelekewa masanduku ya kupigia kura.

Tuli Daslma tunaona mambo ni swafi kabisa...!!
 
Ni Jambo jema ulimsaidia huyo mtoto, lakini baba wa mtoto alikuwa wapi? Unajua sasa hivi kuna wanawake wanazaa tu hata bila waume? Sasa hiyo ni sawa kama siyo kuongeza mizigo kwa Taifa? Tuweke displine Kwanza kwenye jamii zetu Ili kuondoa hayo mambo yanaoongeza unyonge wa mtu na familia, sasa hivi imekuwa sifa mtu kujiita mnyonge au masikini wakati makosa ni yake yeye kila mmoja aangalie wapi anakosea Kama yeye kujiinua kiuchumi, kinachotakiwa sasa nikuomba gharama za vitu zipunguzwe Ili wanapambana na msingi wa dunia wanufaike maana msingi wa Mungu ni kazi Ili tupate vipato, sasa tusilalamike kulipa gharama maana ni wajibu ila tuombe gharama zipunguzwe maana vipato vyetu ni vidogo.
Na kwa nini watu wetu hawawezi kujiongoza hata kwa mambo ya kijamii. Je, ni mfumo wa elimu usiojenga? Au hulka gani?

Pili: Tunataka serikali na Rais mwenye uwezo wa kusimamia mageuzi makubwa.
 
Ndugu yangu, shida zetu, umaskini wetu na kila aina ya matatizo tuliyonayo hayawezi kumalizwa au hata kupunguzwa na Madam SSH.

Kwa kifupi hakuna Rais yeyote yule anayeweza kubadilisha maisha yetu isipokuwa mmoja tu....

Huyo ni MFALME AJAYE, yaani YESU KRISTO. Yeye atakapokuja atamaliza matatizo YOTEE!!.
Aahahhhahaa bwashee taratibu..! Kwa hiyo tusubiri mpaka Yesu atakapokuja?? Hahahahaa.., em tuache kwanza
 
Uko sawa kabisa ndicho nilichomaanisha, kwa mfano hao vijana wanaokwenda kuongea na Raisi wanatakiwa ajenda yao kuu iwe, sisi ni vijana tunanguvu na tupo wengi tupo tayari kufanya kazi sasa Raisi tuongezee ajira zifanyike mchana na usiku Ili zitoe matunda mengi na sisi vijana tupate vipato tujiandae kujenga Taifa tukiwa vijana lakini cha ajabu vijana wataenda kulialia kwa Raisi kwamba wao ni dhaifu wanahitaji kusaidiwa nguvu.
Unaowazungumzia hapo ni vijana wachachesana wenye maono kama wewe. Vijana wengi hapa kwetu wameathiriw na singeli na viduku. Kila wakiamka wao ni instagram na facebook kusifia wasanii
 
Umeelezea vizuri. Hilo la elimu ni kweli kabisa. Lakini siyo elimu tu. Tanzania inahitaji kujitathmini upya. Tujiulize mbona kila rais anayeingia hafanikiwi na akimaliza muda anayeingia anakuwa kama anaanza upya? Jibu ni kuwa system yetu ya uongozi siyo nzuri kabisa. Tunatakiwa tufumue fumue kila kitu tuweke mfumo mzuri zaidi. Wanasiasi wamekuwa wengi na wako kila mahali. Ndiyo wanafanya kila jambo na mbaya zaidi wengi ni vilaza na matapeli waliokimbilia huko kwa sababu tu ni mabingwa wa kupiga gumzo. Tufumue mfumo wetu viongozi wawe wachache na asilimia ndogo tu wateuliwe na rais. Bila kufanya hivyo mama Samia hatakuwa na jipya tena atachokwa haraka sana.
Kiukweli li-mfumo hili hata mimi sielewi.
Kila Rais anaonekana eti anaanza. Yani nchi ni kama TUNABAHATISHA.

Sasa je, kama walioko ndani ya mfumo ni wanufaika. Unategemea wataufumua huo MFUMO?!

AU WANASUBIRI SHIDA ZA WANACHI ZIWAPIGE HADI MATAKONI, TUSHIKANE MASHATI...!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom