Rais Samia, ulitaka wananchi tukataaje tozo za miamala ya simu?

Kama kungekuwa na vyama imara vya upinzani hili lilikuwa tundu la kutokea.
Uimara wa vyama hivyo utatoka wapi ikiwa hata kufanya mikutano kunadi sera wanazuiwa? Ikiwa mwananchi kujiunga na upinzani hayupo huru? Kama kugombea uongozi eg ngazi ya Mtaa, udiwani, au ubunge kupitia upinzani unaenguliwa?
 
Endeleeni kuupiga mwingi si ndio nyie mlipiga vigelegele kuwa sasa mumempata mtu wa watu, msikivivu na misifa kibao, leo kulikoni? sisi wengine bado tuko kwenye maombolezo ya mwendazake, enzi zake haya mambo yasingetokea asilani. Kama mwendazake aliweza iweje sasa huyu ashindwe? jua kuna kitu hapa, mngeanza kwanza kumkataza kuruhusu ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambayo haina tija na kuna watu wanufaika na hiyo kandarasi ya kitapeli na ndio sasa wanakomaa ili wao na familia zao wazidi kuneemeka, pamoja na ukwasi walio nao lakini bado tamaa zimewazidi, sasa wamekuwa ndio Alfa na Omega wa nchi hii, enzi za mwendazake waliwekwa kapuni. Kwa haya yanaoendelea tutazidi kumkumbuka jabali mwendazake.

Nyie mmefanya nini kupinga hizo tozo, au mmewakabidhi jukumu hilo waliomsifia? Kwa taarifa yako hizo tozo ilikuwa ni mpango wa dhalimu ndio maana alilazimisha watu wasajili line za simu kwa alama ya vidole. Na hizo tozo Ilikuwa ni lazima maana dhalimu alikopa fedha nyingi ni ili kusaka sifa za kisiasa, kwa sasa hawa waliongia wamekuta hazina hakuna kitu na huko nje hatukopesheki kutokana na deni kuwa kubwa.

Sisi wengine sasa hivi hatutumi tena hela kwa miamala ya simu, na tunatuma kwa njia hiyo ikibidi sana. Na tumefanya ushawishi kwa watu wengine waachane na hiyo biashara, madhara kwa sasa yapo dhahiri.
 
Kodi ifundishe mashuleni Tena uzuri watu wapate kuelewa na kuipenda

Watu wapende kulipa kodi ili wastaafu wa ccm wakajengewe mahekalu? Huku watawala majizi ya kura ya ccm wakitanua na maVXR?
 
Mko Lumumba pamoja na johnthebaptist ?
Rais na Mwenyekiti wangu wa CCM Taifa, umenifikirisha na kunisikitisha sana. Nimekusikiliza na kukutazama kwenye mahojiano yako na mwandishi na mtangazaji nguli Salim Kikeke. Nimekufuatilia hadi nikalia ulipokuwa ukijibu maswali bila kujali athari.

Juu ya tozo za miamala ya simu, nimekusikia na kukuona ukisema kuwa wananchi hatukukataa tozo husika. Sijakuelewa;sitakuelewa na sikuelewi juu ya kauli hii. Zilipoanza tu tozo zilizua mzozo. Wananchi walisema kwa kuhema; waliandika na kusikika kupinga tozo husika. 'Walimsema na kumlaani' hata mwanzilishi wa hoja ya tozo. Yupo hadi aliyetinga mahakamani kupinga tozo hizo.

Tuliambiwa na Waziri Mwigulu kuwa wewe Rais umesikia kilio chetu na kinafanyiwa kazi. Ulisikia kilio kipi kama si malalamiko na masikitiko yetu wananchi yanayoonesha kuwa tunazipinga tozo hizo? Ulitaka na kutamani wananchi wapingeje zaidi ya hivyo?

Labda ulitaka wananchi tuandamane. Labda ulitaka wananchi tuache kutuma na kupokea pesa kwa njia ya miamala ya simu. Labda ulitaka wananchi tuanzishe vurugu na kupafanya mitaani kuchafuke. Lipi hapo lingekuonesha kuwa tumezipinga na kuzikataa tozo za miamala ya simu? Kauli yako siwezi kuielewa kirahisi.

Rais Samia, sisi watanzania tunazipinga na kuzikataa tozo za miamala ya simu kwa ujumla wake.

Pumzika kwa amani mtani na mdogo wangu Elias Kwandikwa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mwanza Mjini)
 
Mimi Namuombea Huyo Mzanzibari azidi kuwa katiri zaidi ya Mwendazake... na azidi kuwa zaidi ya Mfalme Juha... na alewe madaraka... Nimemchukia kusema ukweli... Pengine alikuwa ni msukule wa Mwendazake huyu
 
Back
Top Bottom