#COVID19 Rais Samia Suluhu: Tutalichukulia kwa uzito suala la COVID-19

watu konachowaua kwenye nchi za jirani especially waliokua na magonjwa nyemelezi ni psychological shock na hofu bora life style lao lingeendelea kama kawaida sisi takwimu hatuzitaki zitazuua taharuki bora tuendelee na maisha yetu kama tulivyozoea

Mbona taarifa za wagonjwa wa ukimwi zilikuwa zinatolewa hakukuwa na taharuki, ama taharuki ndio imeanza kujengeka sasa?
 
Toka mwendazake atutoke hatujasikia vifo vya corona wala vinavyotokana na changamoto ya kupumua,

je, kwanini sasa mnataka kuunda kamati na kwa maslahi ya nani?
Bila shaka ilikuwa inamtafuta imalizane naye kwani ile kitu haitaki dharau. Kumbuka mmoja kati ya chawa wake alipata kuikejeli "kolona" kuwa ikubali kuchagua kuishi Tanzania kwa adabu au iende zake.

Sasa tayari imeshaonesha kuwa yenyewe haipangiwi nidhamu na tayari imekwenda zake.
 
Imani zengine shida kweli.
 
Covid-19 Tanzania(tropical). Ipo lakini sio kama wanavyo izunguzia. Hili janga za Ulaya na America. Sio Tropical(joto). Virus sehemu za joto hawana nguvu. Yeyote. Ivi vimafua tu. Alafu Mungu anatuona Corona haijawai ua mtu Tanzania vifo feki ni consipiration theory. Wasitulazimishe na barakoa na chanjo. Kama wanaona tumeharibu biashara ya chanjo. Wazilete .tulipe pesa keshi. Alafu tutaziputa na kuzichoma usiku. Ili nchi zingine waone tumepokea.tuwape tu pesa.naona wanahisi JPM alikuwa anawaharibia soko la ugonjwa feki tanzania(uvicodi)
 
Hao hao wanaotaka kuunda kamati ya corona ndio hao hao walikuwa wanatuambia Corona ipo kidogo halafu wewe unasema sie tukae pembeni,hadi sasa hao wanaotaka kuunda hiyo kamati hawaonishi kujali kwa kufuata njia za kisayansi za kujikinga na corona hata kwa kuvaa barakoa tu na social distance.
Mimi simo kwenye unajimu wala utabiri kwahiyo sijawajua bado hao members. Kama wewe unawajua tayari labda unitajie..Mimi bado nasubiri.
 
Hakuna chanjo inayoweza kutibu variants zote za Covid-19 na mpaka sasa ziko zaidi ya variants 10.

Hii ndio sababu mganga mkuu wa Serikali ya Uongereza amesema wataanza kuchukulia Covid-19 kama magonjwa mengine ya mafua, because it is here to stay with us for a very long time
Chanjo ya COVID 19 siyo tiba, ni chanjo.
UK kufikia hatua hiyo wamefikia threshold ya herd immunity kupitia chanjo, nyie mmefanya nini hadi mtangaze kama UK ilivyotangaza sera yake juu ya COVID 19? Acheni kukariri!
 
Kamati ikisema maoni yao muwekwe lockdown mtakataa au mtasema wazungu wameacha kuweka watu huko?

Watakachokisema wataalamu tutakipokea kwa mikono miwili.

Kumbe nyie mna majina yenu mifukoni?

Kwa hiyo mna mnachotaka tume iseme na mnavyotaka tume isiseme?

Basi nyie kuweni ndiyo tume mzipe roho zenu mnayotaka kusikia.

Hiiiiii bagosha!
 
Lengo ni kurudisha mahusiano mazuri na wazungu hivyo tutalazimika kufuata yale wanayotaka tufanye kuhusiana na corona hasa kuagiza chanjo za corona,kwahiyo hayo ndio masilahi na ndio ikabidi atolewe pale Kabudi.

Mi najiwazia tu!
HIVI KWANINI MAMA ASIWE MJANJAJANJA yaani tuagize chanjo kwa mbwembwe ili kuwafurahisha tu!zikifika tunabadilisha dawa afu michanjo yao tunachoma Moto kimyakimya!!!
 
WHO ni wakala wa mabeberu!! Wasitupangie!!Mabeberu wamejipanga kupiga hela ya wajinga kupitia corona!! Wana hasiraTanzania tumewabania! Wamejipanga kupiga pesa kupitia upimaji wa kudumu, Chanjo, na uvaaji Wa barakoa!

Kwa mawazo haya bora kuwahi tu kwenu yaani huko mbinguni.
 
Sasa mnatuambia tukitaka kujua kama corona ipo tuwaulize madaktari ila hao madaktari wenyewe ndio hao wanaopotezea corona.
Si uoga? Walikatazwa kutaja Korona na kwa kuwa wanapenda kazi yao basi waliamua kukubaliana na Siasa. Mimi kuna mmoja niliongea naye tu alifunguka. Nafikiri kama woga unaondoka sasa. Na kamati itaundwa. Kitu ambacho hakikutegemewa. Hivyo uwazi upo kwa sasa.
 
Bila shaka ilikuwa inamtafuta imalizane naye kwani ile kitu haitaki dharau. Kumbuka mmoja kati ya chawa wake alipata kuikejeli "kolona" kuwa ikubali kuchagua kuishi Tanzania kwa adabu au iende zake.

Sasa tayari imeshaonesha kuwa yenyewe haipangiwi nidhamu na tayari imekwenda zake.
Hivi haka kachawa tumbili kanapumulia wapi? Yaani yuko kimya kama mfu sasa. Wanamchezea Mungu. Kawachapa vilivyo.
 
Hivi Tanzania haikuwa na ushauri wa kitaalamu na JPM marehemu maamuzi ya corona na hatua alizochukua hakuzingatia ushauri wa wataalamu?

Fitina za aina hii kwa marehemu na utafutaji uungwaji mkono kwa njia hii hazitamsaidia mtu.

Je, anataka Watanzania wa amini suala la corona halikuchukuliwa kwa uzito? Ama ndio njia ya mzunguko kwenda kukubaliana na chanjo za WHO na wajasiriakorona.

Kabisa Mkuu
Ugonjwa wenyewe ni Mpya TZ kuna Wataalam gani wa Covid,
Ugonjwa wenyewe bado wataalam Huko Duniani wanaendelea na Tafiti!
Ila Western wana Maguvu sanaaa Mnooo!
 
Kabisa Mkuu
Ugonjwa wenyewe ni Mpya TZ kuna Wataalam gani wa Covid,
Ugonjwa wenyewe bado wataalam Huko Duniani wanaendelea na Tafiti!
Ila Western wana Maguvu sanaaa Mnooo!

Kwa akili hizi no wonder kulipigwa nyungu sana makwetu.

Hiiiiii bagosha!
 
Si uoga? Walikatazwa kutaja Korona na kwa kuwa wanapenda kazi yao basi waliamua kukubaliana na Siasa. Mimi kuna mmoja niliongea naye tu alifunguka. Nafikiri kama woga unaondoka sasa. Na kamati itaundwa. Kitu ambacho hakikutegemewa. Hivyo uwazi upo kwa sasa.
Sio suala la kutaja corona bali nazungumzia hospitali unaweza kuingia bila barakoa tofauti na hapo nyuma ilikuwa huwezi kuingia getini kama huna barakoa,nilikuwa muhimbili unaingia mpaka ndani huko bila kuulizwa barakoa na hata hao madaktari wenyewe ni wachache tu ndio unakuta wamevaa barakoa ila wengi hawavai barakoa.
 
Hakuna namna nitaingia hospital yoyote Ile bila Barakoa. Hata sehemu za mikusanyiko navaa. Maisha ni yangu. Nitakaposikia kwa wazungu Korona imeisha ndiyo nitavua barakoa. Mpaka yetu iko wazi mno hivyo Corona itaendekea kuwepo tu Tanzania hata kama ni kwa kiwango kidogo lakini ipo. Na mbaya huwezi kumtambua mwenye Korona maana mtu hudumu nayo kwa muda kabla ya kuugua.
 
Hv wabongi tunachotaka kusikia ni nn kuhusu covid 19....
-tuwe na lockdown...?
-namba ya waathirika inayoongezeka pasipo kupungua hata inapotokea watu wamepona....?
-kufungwa kwa mipaka ya nchi, pasiwe na wakuingia wala kutoka...?
Na yote hayo yakitokea yatatufaidisha vipi,
Tuache kukaa kishabiki usio na tija siku ya siku tukaanza kutafuta mchawi nan
 
Hakuna namna nitaingia hospital yoyote Ile bila Barakoa. Hata sehemu za mikusanyiko navaa. Maisha ni yangu. Nitakaposikia kwa wazungu Korona imeisha ndiyo nitavua barakoa. Mpaka yetu iko wazi mno hivyo Corona itaendekea kuwepo tu Tanzania hata kama ni kwa kiwango kidogo lakini ipo. Na mbaya huwezi kumtambua mwenye Korona maana mtu hudumu nayo kwa muda kabla ya kuugua.
Point yangu ilikuwa huku kusema kwamba Madaktari wanajua uhalisia wa corona kwamba wanakutana na wagonjwa wengi wa corona.
 
Back
Top Bottom