Rais Samia Suluhu ashangaza wengi kasi ya Ukuaji Uchumi Tanzania

Asante mkuu Jf lazima tuheshimu kila mtu na tupishane kwa hoja tu kwani sote ni watanzania,

Ila Mama hajawahi kuniangusha mkuu wangu,

Hii nchi ilikuwa inaelelekea shimoni lazima tuwe wa kweli na Mungu atatubariki kwa ukweli wetu,
Kwa sasa ndio inaelekea kaburini kabisa! Watu wanateseka na njaa mitaani nyie mkikaa kwenye vyumba vyenye ac na kupewa posho mnahisi maisha ni mazuri kwa wote. Ipo siku kitatokea kitu cha kustaajabisha sana.

Mtaani vitu bei juu pesa haipatikani
 
CM 1774858. Kila siku yuko kwenye STK na nyumba ya bure na Kila mwezi kwenye ATM Kuchukua chake.
Namuangaliaga humu na ngonjera zake za mapambio! Unajua siku zote mwenye shibe humdharau mwenye njaa na mbaya zaidi humuona kama vile hana akili😅 ila ipo siku yaja watu wataamua tugawane mbao tu!

Naiombea sana hio siku ifike kabla sijaenda kwenye futi 6! Inachosha ifikie mahali wote tuone balaa zito ili tuweze kukaa katika vikao vya maridhiano. Ubinafsi ndo unatumaliza kabisa mkuu maana sikuhizi tatizo lako ni lako tu jamii inajifanya haina habari kabisa hasa wenye ahueni ya maisha wao wanaona mradi ada zinalipwa wanakula na kusaza wao inawatosha.
 
Haya mawazo ya kishetani Tanzania Mungu anailinda mno najua unalijua hili
 
awesomefully,

Niliwaambia huyu Mama atafanya maajabu makubwa sana Tanzania baadhi yenu hamkunielewa, Nadhani kwa sasa mmeanza kuelewa taratibu, Hongera Sana Mama Samia,
Kama tungempata Mama Samia miaka mitano iliyopita tungekuwa mbali sana
 
Chawa
 
 
Huwezi amini mimi ni mkulima tu huku maporini hata Mungu anajua Mimi sina cheo chochote ila ni Mzalendo sana kwa Taifa na Rais wangu,

#Vijana tuweni Wazalendo kwa nchi yetu na Rais wetu,
Unasemaje kuhusu kauli yake ya kuleni kwa urefu wa kamba yenu
 
Kama mambo ndio haya basi Tanzania kama kuna wakati tumepata Rais bora na wa kweli nadhani ni sasa,Tufanye kazi kwa bidii sana,

Hakika huyu Mama ni Mpango wa Mungu,

#WATANZANIA TUFANYE KAZI KWA BIDII
 
Hiyo principle ipo dunia nzima, Wewe unakula kulingana na nini?
Sikuelewi, na misifa unayommwagia mama humu kila siku kumbe wapo pale kupiga tuu na kwa baraka za mama, kama unaweza support Raisi wa namna hiyo utakuwa na matatizo na wewe pia
 
" Kwa mwendo huu Tanzania tutafika tunakotaka kwenda tena kwa kuwahi sana, Hongera Mama Samia, Watanzania tuko nyuma yako We chapa kazi achana na Wasio na jema "
 
Kaziiendelee Tanzania na Rais Samia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…