Rais Samia Suluhu ashangaza wengi kasi ya Ukuaji Uchumi Tanzania

===
According to National Bureau of Statistics (NBS) Pato la Tanzania Tanzania Gross Domestic Product GDP limekua kwa kasi ya ajabu na kufikia asilimia 5.2 robo ya tatu ya mwaka kutoka asilimia 4.1 robo ya kwanza wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani yaani kuanzia tarehe 19|03|2021 takribani miezi tisa sasa,

Kwa lughal rahisi tunaweza kusema Rais Samia Suluhu Hassan kwa miezi hii michache amekuza Pato la nchi nzima kwa ukuaji "Chanya" wa Uchumi wa asilimia 5.2 wakati huu huu ambapo majirani zetu wakishuhudia ukuaji "Hasi " wa Uchumi wao,

Mtakumbuka,hali ilikuwa mbaya zaidi mwaka 2019 pale ambapo AfDB waliikadiria Tanzania Pato lake kushuka kutoka wastani wa ukuaji wa asilimia 7 hadi ukuaji wa asilimia 2.1 mwaka 2019|2020 na sababu ikiwa ni Covid 19,

Wakati huohuo baadhi ya nchi za Africa Mashariki walishuhudia ukuaji hasi wa Uchumi mathalani Rwanda ilirekodi ukuaji hasi wa asilimia 3 & 6 huku Kenya wakishuhudia ukuaji hasi wa asilimia -2.1 robo ya pili ya mwaka 2021 wakati Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan tulirekodi ukuaji Chanja wa asilimia 4.4,

Kuimarika kwa kasi kwa Utalii na uwekezaji mkubwa toka nje na kilimo vimetajwa kuwa ni sababu za kukua kwa kasi kwa Uchumi wa Tanzania hasa katika robo ya tatu ya mwaka 2021 uliofikia TZS 32 trilioni kutoka TZS 30.3 trilioni katika robo ya tatu ya mwaka 2020.

Katika robo ya tatu ( Q3 ) mwaka 2020 Tanzania ilipokea Jumla ya Watalii 72,147 pekee wakati katika kipindi kama hicho mwaka 2021 Tanzania imepokea Jumla ya Watalii 243,565 sawa na ongezeko la Watalii 171,418 ambao ni sawa na asilimia 338

Utalii katika robo hii ya tatu ( Q3 ) umechangia asilimia 18.1 kwenye Uchumi wa Taifa na hii inachagizwa zaidi utengenezaji wa "Royal Tour Film " itakayozinduliwa rasmi 22|04|2022 huku kilimo kikichangia asilimia 15,


VIVA TANZANIA || VIVA SAMIA VIVA

Samia na JPM walituambia tupo uchumi wa Kati .​

Leo anatuambia ukuaji wa Uchumi umefikia 5.2% kutoka 2.1%?​

Kwa maana nyingine wakati Akiwa makamu wa Rais uchumi wa Tanzania ulikuwa 2.1%?​


EAC8DC0E-8751-4CF3-836D-AC3B4DF07230.jpeg
 
Tatizo lilikuwa Corona, Tatizo watanzania wanapenda udaku sana badala ya hoja,
Corona wakati mshahara kila mwezi ulilipwa na posho za kukutosha?
Miezi 8 tangu JPM afariki ametufikisha 5.2% ukuaji wa uchumi. Kwa kifupi Maza hajui hesabu
 
Asante mkuu Jf lazima tuheshimu kila mtu na tupishane kwa hoja tu kwani sote ni watanzania,

Ila Mama hajawahi kuniangusha mkuu wangu,

Hii nchi ilikuwa inaelelekea shimoni lazima tuwe wa kweli na Mungu atatubariki kwa ukweli wetu,
Wewe kakupiga cheo kumfagilia must
 
Huwezi amini mimi ni mkulima tu huku maporini hata Mungu anajua Mimi sina cheo chochote ila ni Mzalendo sana kwa Taifa na Rais wangu,

#Vijana tuweni Wazalendo kwa nchi yetu na Rais wetu,
Mkulima? Ukiona mkulima anamsifia Rais ujue hajui kusoma wala kuandika Mkuu. Sasa Wewe wapi na wapi?
 
Halafu mnasema waarabu wabaya ,Huyo Samia majuzi alitokea kwa wazee wake waliopo biladi Nezwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom