Hili tabasamu la wavuvi nchini ni matokeo ya uweledi wa Rais Samia

Irene Darton

Member
Feb 25, 2024
18
21
Na Mwl Udadis, Nyamagana

Kitendo cha serikali chini ya uongozi wa Rais Samia kutenga kiasi cha zaidi ya bilioni 11 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya wavuvi moja kwa moja ni kitu cha kihistoria. Hatua hii inaleta matumaini makubwa kwa wavuvi wengi, ikiwemo kanda ya ziwa ambapo zaidi ya wavuvi 1200 kutoka katika Mikoa ya Mwanza, Mara, Geita, Kagera na Simiyu watapata manufaa ya moja kwa moja.

Kwa kutoa boti za kisasa, nyavu bora, GPS, na maboya (life jackets), Rais Samia ameonyesha dhamira yake ya dhati katika kuimarisha sekta hii muhimu. Uvuvi ni moja ya shughuli kubwa za kiuchumi nchini Tanzania, na hatua hii itasaidia kukuza ufanisi na usalama katika shughuli za uvuvi.

Wavuvi sasa wataweza kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi na kwa usalama zaidi, huku wakichangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi. Aidha, hatua hii pia inaonyesha utambuzi wa serikali kuhusu umuhimu wa kulinda rasilimali za maji na kusimamia uvuvi endelevu kwa maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho.

Kwa kuwa na viongozi kama Rais Samia Suluhu Hassan, Tanzania inaelekea kwenye njia sahihi ya maendeleo na ustawi wa wananchi. Naungana na watanzania kupongeza juhudi za Rais Samia katika kugusa maisha ya kila mtanzania kwa vitendo na tuendelee kutarajia kuona mafanikio makubwa zaidi katika sekta mbalimbali za maendeleo ya nchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom