Rais Samia: Miradi yote iliyoachwa na Hayati Magufuli ni urithi wetu

Najaribu kutafakari jinsi ambavyo marehemu alivyojisifu kwa kujenga miundombinu mingi, hata ile aliyoikuta ipo mwishoni kukamilika yeye akamalizia asilimia 5% wapambe waliimba na kusifu kwamba kajenga yeye.

Sasa kuna miradi na yeye kaacha haijakamilika mingine ndo kwaanza ipo asilimia 0% kama daraja la busisi.

Ikikamilika tusifu na kuimba mapambio kwa mwendazake km kawa au?
Both of them
 
Anataka kuweka rekodi sawa

Anayetoa hela ndiye anayejenga. Hao wengine wanakuwa ni watendaji ama ambao wameajiriwa kutekeleza majukumu kwa ajili ya tajiri (mlipa kodi).

Wanasiasa wametengeneza mazingira ya kutufanya tuone kama wanatupa favor kutekeleza majukumu yao.
 
šŸ˜„Hatari sana
1617780181977.png
 
Kataja miradi miwili tu ya kimkakati ambayo ni SGR na Bwawa la Umeme. Usimuongezee maneno please

Alisema ā€œmiradi mikubwa miwili na ile miradi ya kimkakatiā€ na yes aliitaja uwanja wa Msalato,unataka kubisha nini sasa,uzuri pale Kigongo kazi inaendelea tena usiku na mchana.
 
Rais Samia amehawakikishia watanzania kuwa miradi yote aliyoacha Hayati Rais Magufuli lazima itekelezwe na kumalizwa kwa sababu ni urithi wa watanzania na tukiitelekeza tutaambulia laana kutoka kwa Mungu na kutoka kwa aliyeanzisha hiyo miradi.

Rais Samia - Rais Dkt. John Magufuli ametuachia urithi, ametuachia miradi mikubwa miwili, na mwingine wa mkakati ipo, ule ni urithi, na wanasema ukifanya mchezo kwenye urithi Mungu anakulaani au yule aliyekuachia urithi hana radhi na wewe na Mungu hatukuwa na wewe

Bwawa la Nyerere, SGR ,Uwanja wa Msalato, daraja la Kigongo Busisi lazima ikamilike.

---

Mkuu vipi kuhusu haya:

1. Urasimu uliokuwapo mama anasema je?
2. Upigaji mkubwa wa pesa uliokuwapo mama anasema je?
3. Ugonjwa wa Corona uliopo mama anasema je?
4. Kuhusu wawekezaji na umuhimu wao mama anasema je?
5. Kuhusu mashirikiano na mataifa mengine mama anasema je?
6. Kuhusiana na kodi za dhuluma mama anasema je?
7. Nk, nk. Tango mengi lukuki.

Hiiiiii
 
Najaribu kutafakari jinsi ambavyo marehemu alivyojisifu kwa kujenga miundombinu mingi, hata ile aliyoikuta ipo mwishoni kukamilika yeye akamalizia asilimia 5% wapambe waliimba na kusifu kwamba kajenga yeye.

Sasa kuna miradi na yeye kaacha haijakamilika mingine ndo kwaanza ipo asilimia 0% kama daraja la busisi.

Ikikamilika tusifu na kuimba mapambio kwa mwendazake km kawa au?

Alikua anajigamba pia kuwa daraja la kigambon kajenga yeye,Ili hali yeye kaenda kuzindua tuh
 
Ile miradi ya Chato hakuitaja mbona, Stadium, Chuo kikuu na mahospitali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom