Rais Samia: Miradi yote iliyoachwa na Hayati Magufuli ni urithi wetu

Endeleeni kutumia yale malori marefu. Treni ya mwendo kasi ni kwa ajili ya abiria na mizigo ya kawaida tu na siyo kwa ajili ya kusafirishia wanyama.

Tumewamulia sana kule Chato mlipotumia mikokoteni ya punda kuvuka kwenye zile taa za kuongozea vyombo vya moto. Tuseme tu inatosha.
Ahaaaa, acha utoto unazeeka sasa.
 
Rais Samia amehawakikishia watanzania kuwa miradi yote aliyoacha Hayati Rais Magufuli lazima itekelezwe na kumalizwa kwa sababu ni urithi wa watanzania na tukiitelekeza tutaambulia laana kutoka kwa Mungu na kutoka kwa aliyeanzisha hiyo miradi...
Haivina msaada
 
Hao Sukuma Gang vita yao ni kuipasua CCM ili Mama apate ugumu kukiongoza chama pindi atakapokabidhiwa uenyekiti,yaani wana ile falsafa ya bora tukose wote. Wao kazi yao ni kumpinga Mama tu wala hawana mpango na Chadema. Hili ni genge hatari sana chini ya Askofu Chidi.
Acha uongo Mama Samia anahitajika sana kanda ya ziwa kuliko jana, nyie mnajaribu kupenyeza fitna ili aonekane anapigwa vita kanda ya ziwa Mama Samia kwa kanda ya ziwa ni dada yetu na shangazi yetu, amefanya kazi na Mjomba wetu na kaka yetu. Mama Samia bado tuna jambo letu kwake, kwa miradi kibao ambayo inahitaji ufadhili wa serikali ya awamu ya sita.

Chadema mna kesi kanda ya ziwa kwa kutubatiza SUKUMA GANG, kesi ile itahukumiwa 2025, mnatuona tumekaa kimya mkidhani tumefurahi na huo ubaguzi wenu. 2025 Mama Samia anazoa kura 95% bila jasho.

Jana Mwenyekiti wenu kaongoe kwa upole huku akijua kabisa chama chake kimeingiza ubaguzi kwa kuwaita kanda ya ziwa SUKUMA GANG.Tusubiri muda utaongea
 
Kuna watu watashangaa sana kwa kulisema hili, lakini sijakosea kusema hivyo! Nina maanisha

Sioni ulazima wa Mh Rais kubebeshwa mzigo ambao haku uasisi yeye, hata hayati Magufuli kuna miradi iliyoasisiwa na mtangulizi wake Mh Kikwete lakini yeye alivyoingia madarakani akaachana nayo, Yes tunatambua alikuwa Makamu wa Rais lakini siyo kweli kila alichopanga aliyekuwa Rais wa JMT hayati JPM basi Mama Samia nae aliridhia.

Mh Rais sasa ndio wakati wake wa kufanya lile analoliamini na kutambua lipo ndani ya uwezo wake ,

Watanzania watamkumbuka kwa yale atakayoyafanya na kuyakamilisha, Rais kuamua kuendeleza miradi mikubwa ambayo pengine hakuiridhia tunaweza kusema anajiingiza mtegoni pasipo kufaham kwani muda aliopewa kama Rais ni mchache sana na pengine asi accomplish hata asilimia 30% ya miradi aliyoiacha Magufuli.

Mh Rais chagua tena upya miradi michache uipe kipaumbele na ukiamini inatekelezeka katika mfumo wa makusanyo halali ya kodi,

Miradi mingi mtangulizi wako aliitekeleza kwa kodi nyingi za kubambikiza ambazo sasa wewe umeshasema wananchi wasibambikiziwe kodi, miradi mingi imetekelezwa kwa faini ya makosa ya uhujumu uchumi ambazo ni kesi zilizokuwa na chembe ya uonevu pia vilevile.

Miradi mingi aliyoiasisi mtangulizi wako haitegemei kodi halali za watanzania, inachochea deni la Taifa kupaa kila kukicha.

Narudia tena kukushauri Mh Rais fanya machache na wananchi watakukumbuka nayo;

Kwa mfano

1. Boresha Kilimo cha Mtanzania ikiwemo upatikanaji wa Maafisa ugani,Pembejeo za kilimo pamoja na masoko ya uhakika

2. Bima ya Afya kwa Kila Mtanzania, hili lipe uzito kamili

3. Utawala Bora wa Sheria na Uwajibikaji

4. Boresha miundombinu ya Hospitali kila mkoa, wilaya na kata

5. Boresha mazingira mazuri ya Kibiashara na Uwekezaji.

6. Boresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama.

7. Imarisha Demokrasia nchini.

8. Dhibiti mfumuko wa bei hasa bidhaa za vyakula na ujenzi.

9. Suala la KATIBA lipe kipaumbele na historia itakukumbuka Mh Rais
 
Huwezi Acha miradi ambayo tayari ulishaingia mkataba utashtakiwa,au ukubali kulipa fidia ile kwako.Miradi yote haina tatizo shida ni miradi mingi mikubwa isababishayo mambo mengine kusimama kusubiria Hadi ikamilike.
 
Hii nchi wajinga wengi Sana,hivi unaujua Umuhimu wa miundo mbinu ndani ya Taifa?

Kweli uache kutafuta umeme wa uhakika kwa ajili ya viwanda na uendeshaji wa shughuli mbalimbali?
Uache kutanua wigo wa njia za usafirishaji wa hizo bizaa unazosema zizalishwe kwenye kilimo?
 
Tuwe objective ndugu zangu. Miradi inajengwa kwa mkataba maalumu ya kisheria. Ukivunja kwa mihemko unalipa gharama zote za mradi bila kupata kitu.!

Muacheni amalizie hiyo, ila sianze mingine mikubwa. Kipaumbele kiende kwenye uchumi mdogo, uchumi wa watu " micro-economy"!
 
Kuna watu watashangaa sana kwa kulisema hili, lakini sijakosea kusema hivyo! Nina maanisha

Sioni ulazima wa Mh Rais kubebeshwa mzigo ambao haku uasisi yeye, hata hayati Magufuli kuna miradi iliyoasisiwa na mtangulizi wake Mh Kikwete lakini yeye alivyoingia madarakani akaachana nayo, Yes tunatambua alikuwa Makamu wa Rais lakini siyo kweli kila alichopanga aliyekuwa Rais wa JMT hayati JPM basi Mama Samia nae aliridhia.

Mh Rais sasa ndio wakati wake wa kufanya lile analoliamini na kutambua lipo ndani ya uwezo wake ,

Watanzania watamkumbuka kwa yale atakayoyafanya na kuyakamilisha, Rais kuamua kuendeleza miradi mikubwa ambayo pengine hakuiridhia tunaweza kusema anajiingiza mtegoni pasipo kufaham kwani muda aliopewa kama Rais ni mchache sana na pengine asi accomplish hata asilimia 30% ya miradi aliyoiacha Magufuli.

Mh Rais chagua tena upya miradi michache uipe kipaumbele na ukiamini inatekelezeka katika mfumo wa makusanyo halali ya kodi,

Miradi mingi mtangulizi wako aliitekeleza kwa kodi nyingi za kubambikiza ambazo sasa wewe umeshasema wananchi wasibambikiziwe kodi, miradi mingi imetekelezwa kwa faini ya makosa ya uhujumu uchumi ambazo ni kesi zilizokuwa na chembe ya uonevu pia vilevile.

Miradi mingi aliyoiasisi mtangulizi wako haitegemei kodi halali za watanzania, inachochea deni la Taifa kupaa kila kukicha.

Narudia tena kukushauri Mh Rais fanya machache na wananchi watakukumbuka nayo;

Kwa mfano

1.Boresha Kilimo cha Mtanzania ikiwemo upatikanaji wa Maafisa ugani,Pembejeo za kilimo pamoja na masoko ya uhakika

2.Bima ya Afya kwa Kila Mtanzania, hili lipe uzito kamili

3.Utawala Bora wa Sheria na Uwajibikaji

4.Boresha miundombinu ya Hospitali kila mkoa, wilaya na kata

5.Boresha mazingira mazuri ya Kibiashara na Uwekezaji

6.Boresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama

7.Imarisha Demokrasia nchini

8.Dhibiti mfumuko wa bei hasa bidhaa za vyakula na ujenzi

9.Suala la KATIBA lipe kipaumbele na historia itakukumbuka Mh Rais
Muangalieni mtu mjinga huyu....
kasome ilani ya CCM kurasa 303
unadhani kiongozi wa nchi anabuni miradi yake kichwani!!???
Tz kuna mijitu mijinga kweli kama hili hamnazo
 
Si ameshasema yeye na JPM ni kitu kimoja!?

Na akafafanua kwamba maana ya kauli mbie yake KAZI IENDELEE ni kuendeleza yale waliyokua wamepanga?!

Isitoshe JPM ni role model wake na alishanshukuru kwa kumnyoosha na kumwabia anaweza kumpumzika huku yeye akimhakikishia ana uwezo wa kuwanyoosha wengi...... au hili nalo hulijui

Kazi inaendelea chakii
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom