Rais Samia: Miradi yote iliyoachwa na Hayati Magufuli ni urithi wetu

Nimeona wabunge wakijadili either kuachana na Miradi ama Kuendelea nayo. Mkiachana nayo mjue tu 2025 mtarudi ikulu kwa njia ya kikomandoo na sio sanduku kura. Mrudi msirudi mimi sina shida.

Madhara ya kuacha mradi wa SGR.
1. Nchi kama Congo, Uganda, Burundi na Rwanda. Ni rasimi sasa zitahamia Mombasa Kenya. Maana hii reli ndio lango kuu la mizigo ya hizi nchi. Hivyo msicheze nao wekeni hapo pesa zote na taifa litainuliwa.
2. Pesa iliyokwisha wekezwa iatakufa kifo cha mende. Yaani ni Zaidi ya hasara.

Madhara ya Kuacha Umeme wa Rufiji.
1. Pesa iliyokwisha wekezwa iatakufa kifo cha mende. Yaani ni Zaidi ya hasara.
2. Itachukua mda mrefu sana kuja kupata tena umeme mwingi kama huu.

Uzuri PM ameshatoa maelekezo na maelezo kwamba umeme wa Rufiji utakamilika June 2022. Sina uhakika na SGR.

Yangu ni hayo tu.
 
Jiwe kawaachia Tu msala wenzake , hyo miradi haina wahisani , na inazd uwezo wa Taifa kuihudumia , maamuz ya kukurupuka na kutoshirikisha wengine ndo yaliyotufikisha hapa, viongoz wengne wajifunze kushirikisha Kwa ukamilifu ili kujua mbivu na mbichi!

Kabla ya kuingia kwenye mega project kama hzo wazee.....Kuiacha itakuwa hasara Sana , na kukomaa nayo Kwa bajeti ya ndani , tutakula michicha mpak tupauuke aisee, the best option mama arande rande huko nje akatfte hela ya kuigharamikia vinginevyo tutakuja kulaumiana hapa
 
Huyu PM wako ana mamlaka zaidi ya Rais? Rais akiamua kusitisha hiyo miradi kama Hayati wako alivyo sitisha ule mradi wa bandari ya Bagamoyo, unadhani huyo PM wako atafanya nini zaidi tu ya kuufyata?
Rais akiamua sisi wananchi tukakataa hapo unasemaje, sisi ndo bosi wa maboss, shubamit we
 
Jiwe kawaachia Tu msala wenzake , hyo miradi haina wahisani , na inazd uwezo wa Taifa to the maximum, inaumiza mno, maamuz ya kukurupuka na kutoshirikisha wengine ndo yaliyotufikisha hapa, viongoz wengne wajifunze kushirikisha Kwa ukamilifu ili kujua mbivu na mbichi....!!!
Inaumiza watu
 
Jiwe kawaachia Tu msala wenzake , hyo miradi haina wahisani , na inazd uwezo wa Taifa kuihudumia , maamuz ya kukurupuka na kutoshirikisha wengine ndo yaliyotufikisha hapa, viongoz wengne wajifunze kushirikisha Kwa ukamilifu ili kujua mbivu na mbichi....!!! Kabla ya kuingia kwenye mega project kama hzo aisee
Hii ndiyo kazi ya kiume, sio ukae kama mrenda mrenda kila siku.

JPM alikuwa mwanamme wa shoka.

Ni ngumu kuja kumpata mtu kama huyu.

Kenya wanapata shida sana na huu mradi maana wanatamani tukwame ili wao wapate biashara.
 
Una jinsia gani wewe ya kumsifia mwanaume hivi? Kama ni ya kike sawa. Ila kama ni ya kiume, basi ujitahidi wakati mwingine kupunguza ukali wa maneno, ili kulinda heshima yako.

Maana wanaume wa shoka tuko wachache! Na tunatambuliwa na wanamke tu! tena ni pale tunapokuwa faragha.
 
Huyu PM wako ana mamlaka zaidi ya Rais? Rais akiamua kusitisha hiyo miradi kama Hayati wako alivyo sitisha ule mradi wa bandari ya Bagamoyo, unadhani huyo PM wako atafanya nini zaidi tu ya kuufyata?
sorry kwani rais SSH amesitisha huo mradi?
 
Rais akiamua sisi wananchi tukakataa hapo unasemaje, sisi ndo bosi wa maboss, shubamit we
kizazi kipi hiko unaongelea? kama ni hiki kizazi cha waoga na unafki. nakwambia utajikuta mwenyewe.
polisi wakichimba biti kidogo tu watu ndani? mtaweza kupingana na serikal nyie?

mnaonge tu kwenye key board ila field hamna kitu.
 
Miradi yote hii itafutiwe wahisani - aliyekuwa anatupiga fix kwamba sisi ni dona country kakimbia kabla ya miradi yake kuimalizia - hatuna mamna ni lazima tuimalizie ila kwa kutumila approach nyingine.

Huwezi kulaza wananchi wako njaa kwa miaka 5 kisa eti unajenga Reli ambayo itadumu kwa miaka zaidi ya 500.
 
Mnaonaje tujikite kwenye Mradi Mmoja kwa wakati kama tukomae na hilo Bwawa mpaka liishe

Bwawa likiisha tunavuta pumzi kidogo halafu ndio tunaugeukia huo Mradi wa SGR tunaupeleka hadi Isaka halafu tunavuta pumzi tena

Hii miradi imefanywa kwa kukurupuka mno
Najua Misukule ya Mataga itakuja na matusi
 
Nimeona wabunge wakijadili either kuachana na Miradi ama Kuendelea nayo. Mkiachana nayo mjue tu 2025 mtarudi ikulu kwa njia ya kikomandoo na sio sanduku kura. Mrudi msirudi mimi sina shida...
Profesa Assad ambaye hana impact hata kwenye ukoo wake alafu anapimana ubavu na mtu mwenye legacy ya 1000 ijayo.
 
Mnaonaje tujikite kwenye Mradi Mmoja kwa wakati kama tukomae na hilo Bwawa mpaka liishe

Bwawa likiisha tunavuta pumzi kidogo halafu ndio tunaugeukia huo Mradi wa SGR tunaupeleka hadi Isaka halafu tunavuta pumzi tena

Hii miradi imefanywa kwa kukurupuka mno
Hapana Sgra nayo ni muhimu kwa sisi tunaosafirisha Ng'ombe kutoka maeneo ya Kahama kuja huko Dar. Tunawasaidia kuganga njaa zenu mna shida sana za mboga.
 
Hapana Sgra nayo ni muhimu kwa sisi tunaosafirisha Ng'ombe kutoka maeneo ya Kahama kuja huko Dar. Tunawasaidia kuganga njaa zenu mna shida sana za mboga.
Endeleeni kutumia yale malori marefu. Treni ya mwendo kasi ni kwa ajili ya abiria na mizigo ya kawaida tu na siyo kwa ajili ya kusafirishia wanyama.

Tumewavumilia sana kule Chato mlipotumia mikokoteni ya punda kuvuka kwenye zile taa za kuongozea vyombo vya moto. Tuseme tu inatosha.
 
kizazi kipi hiko unaongelea? kama ni hiki kizazi cha waoga na unafki. nakwambia utajikuta mwenyewe.
polisi wakichimba biti kidogo tu watu ndani? mtaweza kupingana na serikal nyie?

mnaonge tu kwenye key board ila field hamna kitu.
Hajasitisha mkuu. Nilimjibu tu huyo mpuuzi kama ulivyo mjibu wewe hapo juu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom