Rais Samia: Miradi yote iliyoachwa na Hayati Magufuli ni urithi wetu

Najaribu kutafakari jinsi ambavyo marehemu alivyojisifu kwa kujenga miundombinu mingi, hata ile aliyoikuta ipo mwishoni kukamilika yeye akamalizia asilimia 5% wapambe waliimba na kusifu kwamba kajenga yeye.

Sasa kuna miradi na yeye kaacha haijakamilika mingine ndo kwaanza ipo asilimia 0% kama daraja la busisi.

Ikikamilika tusifu na kuimba mapambio kwa mwendazake km kawa au?
Sio kweli, busisi naweza sema limefika 50%, na Sasa hivi Kuna watu wanapita hapo
 
Rais Samia amehawakikishia watanzania kuwa miradi yote aliyoacha Hayati Rais Magufuli lazima itekelezwe na kumalizwa kwa sababu ni urithi wa watanzania na tukiitelekeza tutaambulia laana kutoka kwa Mungu na kutoka kwa aliyeanzisha hiyo miradi.

Rais Samia - Rais Dkt. John Magufuli ametuachia urithi, ametuachia miradi mikubwa miwili, na mwingine wa mkakati ipo, ule ni urithi, na wanasema ukifanya mchezo kwenye urithi Mungu anakulaani au yule aliyekuachia urithi hana radhi na wewe na Mungu hatukuwa na wewe

Bwawa la Nyerere, SGR ,Uwanja wa Msalato, daraja la Kigongo Busisi lazima ikamilike.

---

Hongera sana Rais wetu Samia Suluhu Hassan
Mungu akuongoze akubariki afya pia ukamilishe zile kurasa 303 za ilani ya Chama cha mapindunzi

Mungu ibariki Tanzania 😍🇹🇿🔥🔥🔥🔥
 
Vipi kuhusu nyinyi Mataga? Hakuahidi kuendelea kuyasikiliza yale mapambio yenu?
Hawa ndiyo ingizo jipya la Askofu Chidi ili kuja kumhujumu Mama, Sukuma Gang ni genge hatari sana.
Screenshot_20210407-105433.jpg
 
nyie pambaneni na hao chadema,siye tupo na mama suluhu.
Hao Sukuma Gang vita yao ni kuipasua CCM ili Mama apate ugumu kukiongoza chama pindi atakapokabidhiwa uenyekiti,yaani wana ile falsafa ya bora tukose wote. Wao kazi yao ni kumpinga Mama tu wala hawana mpango na Chadema. Hili ni genge hatari sana chini ya Askofu Chidi.
 
Rais Samia amehawakikishia watanzania kuwa miradi yote aliyoacha Hayati Rais Magufuli lazima itekelezwe na kumalizwa kwa sababu ni urithi wa watanzania na tukiitelekeza tutaambulia laana kutoka kwa Mungu na kutoka kwa aliyeanzisha hiyo miradi.

Rais Samia - Rais Dkt. John Magufuli ametuachia urithi, ametuachia miradi mikubwa miwili, na mwingine wa mkakati ipo, ule ni urithi, na wanasema ukifanya mchezo kwenye urithi Mungu anakulaani au yule aliyekuachia urithi hana radhi na wewe na Mungu hatukuwa na wewe

Bwawa la Nyerere, SGR ,Uwanja wa Msalato, daraja la Kigongo Busisi lazima ikamilike.

---
Itategemea na hali ya uchumi wa nchi. Tushibe kwanza ndipo tuangalie hiyo miradi. Ninaona yatakuwa ma-'white elephants".
 
Najaribu kutafakari jinsi ambavyo marehemu alivyojisifu kwa kujenga miundombinu mingi, hata ile aliyoikuta ipo mwishoni kukamilika yeye akamalizia asilimia 5% wapambe waliimba na kusifu kwamba kajenga yeye.

Sasa kuna miradi na yeye kaacha haijakamilika mingine ndo kwaanza ipo asilimia 0% kama daraja la busisi.

Ikikamilika tusifu na kuimba mapambio kwa mwendazake km kawa au?
Miradi mingi itakwama tu kwa sababu "their financing sources are lamely planned". Uchumi wetu hauwezi kugharamia hiyo miradi 100% bila misaada kutoka nje. Kufanya hivyo ni kuua raia.
 
Sasa mbona mnaipasua hiyo CCM? Ile kazi inayofanywa na lile genge linalotumia account ya Veronica France na Monica France kule FB unaona lina nia njema na chama kweli. Wasukuma mna roho mbaya sana.
Huna cha kuwafanya wasukuma hata kama huwapendi.

CDF ni msukuma
 
Najaribu kutafakari jinsi ambavyo marehemu alivyojisifu kwa kujenga miundombinu mingi, hata ile aliyoikuta ipo mwishoni kukamilika yeye akamalizia asilimia 5% wapambe waliimba na kusifu kwamba kajenga yeye.

Sasa kuna miradi na yeye kaacha haijakamilika mingine ndo kwaanza ipo asilimia 0% kama daraja la busisi.

Ikikamilika tusifu na kuimba mapambio kwa mwendazake km kawa au?
Acha usisifu mkuu watz wanajua!
 
Miradi ya Rais kikwete iliyoachwa na ikapuuzwa kuna mtu kapata laana kwani...
Ni ngumu sana kuuwa legacy ya Magufuli na uzuri jamaa alikuwa anasema hadharani watanzania wanajua.

Ndiyo maana mpinga legacy ya Magufuli hatajibiwa na Magufuli wala watoto wa Magufuli mbali atajibiwa na watanzania.

Kama Ndugai anasema Magufuli alishauriwa vibaya itabidi atueleze huo mkataba unasemaje tofauti na aliyosema Magufuli.

Watakaohoji haya ni watanzania.

Ni kama waliojaribu kuuwa legacy ya Nyerere huwa wanatapa upinzani mkali hadi leo wakati Nyerere alishafariki zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Watu huwa wanarejea hotuba tu.

Maneno huiishi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom