Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991

Rais Samia amesema amemhamisha Maharage Chande kutoka TCCL ili kuondoa mgongano wa kimaslahi kwa kuwa ana biashara na taasisi hiyo.
"Maharage tumekutoa TANESCO na nikachukulia uzoefu wako wa DSTV nikaona sekta ya TTCL ingekufaa zaidi. Sasa baadae nikagundua una biashara ndani ya TTCL na kwa sababu kampuni ile inafanya vizuri na ndio maana imemuwezesha kijana yule nae kufanya vizuri nikasema hapana, usiende mahali ambapo una biashara, itakuwa conflict of interest. Nikaona sasa nikupe u postamasta mkuu" Amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amebainisha kuwa Postamasta wa sasa amekwenda kwenye mafunzo na akirudi atapangiwa kazi nyingine. Amemtaka Maharage kwenda kuikuza sekta hiyo ili iende kidigitali.

Rais Samia amesema taarifa za mambo yanayofanywa na watendaji ziwe zinaandikwa na kutumwa ili aweze kuelewa vyema wakati wa kutoa maamuzi na kuondoa changamoto ya kuondoa watu wanaostahili kuwepo kwenye sehemu husika.
Msigwa.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Bw. Gerson Partinus Msigwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Septemba, 2023.

303f3441-f8d7-4e6d-bcd1-5298400997bf.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Bi. Bahati Ibrahim Geuzye kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Septemba, 2023.


Kuhusu changamoto ya kukatika kwa umeme, Rais Samia ametoa miezi 6 kwa mkurugenzi wa sasa ili aweze kuondoa tatizo hili linalochangiwa na mambo mengi ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa na ukarabati wa mitambo.

"Tatizo la kukatika kwa umeme si la mtu, ni letu kitaifa. Kwa hiyo sasa tumejipanga vizuri, tunafanya ukarabati wa hizo mashine, lakini pia tuna mipango mingine ya kujenga substations, kuunganisha mikoa kwenye gridi ili umeme usikatike. Kwa hiyo, nenda kaanzie pale Maharage alipoishia. Najua utaweza, nakupa miezi 6, nakuangalia pale TANESCO. Kazi yako ya kwanza kusimamia ukarabati wa mitambo, lakini baada ya miezi 6 nisisikie kelele za kukatika kwa umeme"

c50216ca-4dcc-49b5-9ada-1dfded070015.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Said Othman Yakubu kuwa Balozi kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Septemba, 2023.

Viongozi.jpeg

Viongozi mbalimbali wakila Kiapo cha Maadili ya Utumishi wa Umma Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Septemba, 2023.
Samia Majaliwa Chalamila.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi kwenye picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali walioapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Septemba, 2023.
 
Kwa hiyo akiwa postmaster ndo hataleta msuguano wa kimaslahi huko TTCL, ngumu kumeza hii.....atuondolee na wale wanaomiliki vituo vya mafuta, mabasi na malori maana wanatuletea shida kubwa huko kwenye bei za mafuta na kuhujumu kuanza kwa safari za SGR.​
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom