Rais Samia: Kwa sura nazoziona hapa (CHADEMA) hamna dhamira ya kushika dola 2025, mnajua mama yupo

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,547

Rais Samia akiwa katika Maadhimisho amezungumza mambo mbalimbali. Akiwa anajibu hoja ya Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa BAWACHA kuhusu nia yao ya kushika dola 2025 Rais Samia amesema:

"Ndugu zangu siasa ni mchezo wa kulumbana kwa hoja Wote tukiwa na lengo la kushika dola kama alivyosema Mwenyekiti wa BAWACHA na Freeman Mbowe. Kwa sura nazoziona hapo hamna nia ya kushika dola 2025 mnajua Mama yupo dhamira hiyo haipo."

"Lakini niseme yes wote tuna lengo hilo lakini tukafanye kistaarabu kama Wanaadamu kama watu. Tuheshimiane, tuheshimike duniani."

Aidha Rais Samia ameongeza;

"Nataka niwaambie kitu kwa kipindi hiki kifupi nchi yetu inaheshimika sana duniani. Kwahiyo tusiirudishe chini, tusiirudishe nyuma. Twendeni na mwendo huu tuweke heshima ya nchi yetu pale inapostahiki.


Tanzania ni taifa kubwa tusilitolee sifa yake."
 
Chadema kama watakuwa wana Akili kesho naomba waanze kurahani na kutoa kauli kali,hivi mama inakuwaje anaalikwa kwenye chama cha wenzake alafu mwishowe anawambiaa CCM hoye.

Aisee hii kauli kwakweli mm imenivurugia sherehe nzima ya leo.

Na chadema walivyo manyumbu Nimesikia wanaitikia Ccm oyeeeee!!!
 
Back
Top Bottom