Nilivyoelewa kauli ya Mbowe ni kuwa lengo la CHADEMA ni kumsaidia Mama kuongoza vizuri na sio kushika Dola

busar

JF-Expert Member
Dec 22, 2011
1,068
1,060
Asalam,

Jana katika kumsikiliza Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe nikaona ametoa tafsiri ambayo sikuwa naijua ya malengo ya vyama vya upinzania Tanzania. Kwa ufupi anasema LENGO KUU NI KUMSAIDIA MAMA KUONGOZA VIZURI (kwa Tafsiri yangu na nyongeza kidogo ni sawa na kusema lengo sio kushika dola). Hebu msome hapa kidogo halafu nitaendelea na uchambuzi

"Unafiki na uongo hulaanisha taifa, taifa letu linawatu wengi wasiosema na kuuwishi ukweli, hili ni chimbuko kubwa la mporomoko wa maadili, nakusihi sana mama epuka mtu yeyote anayejiita chawa wako, Mhe.Rais sisi wengine tumechagua kusema ukweli, na kukataa dhambi ya unafiki, tumelipa gharama kubwa kwa misingi na misimamo yetu hiyo, tunaamini ukweli, uwazi kutokuwa wanafiki, ndio njia bora ya kukusaidia uweze kuwa kiongozi bora"Mhe.Mbowe (ITV 8.MARCH, 2023).

1. Kwa kauli hii ya Mwenyekiti sasa rasmi CHADEMA sio mshindani wa kuingia Ikulu ya Tanzania. Lengo la msingi kabisa la chama cha siasa linapaswa kuwa kuingia Ikulu na sio kukisaidia chama kilichopo madarakani kuendelea kubaki madarakani. Hili lengo sikuwahi kulijua kama ndio msingi wa CHADEMA.

2. Kujitofautisha na chawa wengine. Kwa mara ya kwanza CHADEMA imejinasibu kujiunga na uchawa lakini ikijaribu kujitofautisha na chawa wengine kuwa wao ni chawa bora zaidi. CHADEMA imepoteza credibility katika hili. CHADEMA imeachana rasmi na siasa za kisera na kimabadiliko.

3. Kwa kauli za Wenyeviti wa Vyama hivi jana. CCM ina haja ya kumpongeza Mama kwa uwezo mkubwa, ujasiri, na ufundi sio tu wa kuwalainisha wapinzania lakini kufika mahali sasa wamekuwa rasmi upande wa chama kinachotawala.

kwa haya machache ushindi kwa CCM serikali za mitaa 2014, na uchaguzi mkuu 2025 ni dhahiri. CCM ndio itaamua CHADEMA au ACT wazalendo wapate nini kwenye serikali za mitaa na uchaguzi mkuu. kwa sasa kwaheri vyama vya upinzania Tanzania.

Wasalam
 
Tuukubali tu ukwel kwasasa chadema imebaki kopo tuuu debe tupuuu
 
Asalam...
Jana katika kumsikiliza Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe nikaona ametoa tafsiri ambayo sikuwa naijua ya malengo ya vyama vya upinzania Tanzania. Kwa ufupi anasema LENGO KUU NI
Hakuna mkate mgumu mbele ya chai!
 
Maneno ya Mbowe yako wazi alisema wao wana matumaini Mungu akipenda watashika dola, hilo moja, la pili, kazi yao kwa sasa ni kuikosoa serikali au kwa kifupi uongozi wa mama Samia,ili akiwa msikivu atafuata ushauri wa CDM na kwa kufanya hivyo atakuwa na uongozi bora.

Hili halimaanishi hawezi kuondolewa kwenye uongozi iwapo ata mess up na kwa sanduku la kura wananchi wakamuondoa na CDM kuchukua dola au chama chochote kile.

Hivyo, lengo la CHADEMA kushika dola huwezi kulitenganisha na ushauri wao wa kisera kwa CCM ili wakiudharau iwapo ni mzuri kazi kwao. Mbowe yuko sahihi katika maelezo yake.
 
Dawa imeanza kuingia huko🏃🏃🏃
 
Asalam...
Jana katika kumsikiliza Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe nikaona ametoa tafsiri ambayo sikuwa naijua ya malengo ya vyama vya upinzania Tanzania. Kwa ufupi anasema LENGO KUU NI KUMSAIDIA MAMA KUONGOZA VIZURI (kwa Tafsiri yangu na nyongeza kidogo ni sawa na kusema lengo sio kushika dola). Hebu msome hapa kidogo halafu

Wasalam
Hukuelewa kitu wewe.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom