Freeman Mbowe: CCM ijenge mifumo ya kudhibiti viongozi wake ndani ya Chama ili wasiumize Watanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Kongamano la Siku ya Wanawake Duniani lilioandaliwa na Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) katika Ukumbi wa Kuringe - Mkoa wa Kilimanjaro leo tarehe 08 Machi, 2023.




C1364DCF-0BE0-4D55-AE4E-652AEB349ACF.jpeg


Rais Samia akipokelewa na Viongozi wa Chadema kwenye uwanja ndege wa KIA baada ya kuwasili.
Rais Samia amewasili ukumbini na kupokelewa na Viongozi mbalimbali wa chadema akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe. Mkutano huu umehudhuriwa pia na Viongozi wa kamati kuu ya Chadema, viongozi wa kanda na mabaraza, Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, viongozi wa dini, wageni wengine waalikwa pamoja na wanachama na wapenzi wa Chadema.

CB903E3E-2197-4E0B-8566-88415FB9D227.jpeg

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwasili ukumbini

CATHERINE RUGE, KATIBU WA BAWACHA
Amemshukuru Rais Samia kwa kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano huo na amesema kuwa hawakumualika Rais kimakosa kwani ni mwanamke mwenzao.

Amejivunia kujenga baraza imara lenye ushawishi mkubwa nchini, amemkumbusha Rais kuwa wanawake ni jeshi kubwa na wapo Milioni 31 kwa mujibu wa Sensa iliyopita. Pamoja na wingi huu, hadhi ya wanawake nchini ni ndogo, wanaishi maisha duni. Kwenye mkutano huu pekee, wanawake 3234 wamehudhuria.


FB963765-4ACA-49DE-A4D9-7D773885F374.jpeg

Catherine Ruge, Katibu wa BAWACHA
Amemshauri Rais Samia kutokuogopa kukatishwa tamaa na wale wasio itakia mema nchi hii ambao kwa kiasi kikubwa ni wanaume kwani mwanamke akiamua jambo lake hulifanya pasipo kurudi nyuma.

BAWACHA imetambua juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Samia akishirikiana na Mhe. Freeman Mbowe katika maridhiano na kutafuta katiba mpya kabla ya mwaka 2025. Ameomba jambo hili liendelee kufanyika kwa kasi kubwa ili matamanio ya watu yaweze kutimia.

Kuhusu Kuuliwa kwa watu na polisi, Mhe. Ruge amesema BAWACHA inalaaani vikali mauaji yanayofanywa na Polisi kwa raia wakiwa Mtaani na vituoni.

"Hatufurahishwi na mauaji yanayotokea katika maeneo mbalimbali yanayofanywa na jeshi la polisi hasa katika vituo vya polisi na maeneo mengine ya ukamataji. BAWACHA tutaendelea kutetea haki ya kuishi, haki ya uchaguzi, haki ya kupata ajira, haki ya kupata huduma bora za afya hasa za wanawake na watoto, haki hizi zote zimekuwa zinavunjwa kinyume cha Katiba" amesema Ruge


SHARIFFA SULEIMAN, MWENYEKITI BAWACHA
Ametaja mafaniko kadhaa yaliyochangiwa na BAWACHA kichama na katika ngazi ya Taifa, pia ameelezea mambo waliyofanyiwa wanawake kwenye chaguzi za mwaka 2019 na 2020 ambao amesema ulikuwa ni unyanyasi mkubwa uliofanywa kidikteta.

2925C6D9-4B2D-44C5-A0C0-3F1B6FD1CFA3.jpeg

Shariffa Suleiman, Mwenyekiti BAWACHA
Kwa niaba ya BAWACHA, Mhe. Sharifa ametoa mambo manne kwa Rais akimuomba Kupunguza bei za vyakula na kudhibiti mfumuko wa bei, Kuongeza kima cha chini cha mshahara, Kuboresha sekta ya afya na Kurejesha mchakato wa Katiba na tume huru ya uchaguzi, katiba itakayorudisha heshima ya nchi.

Kuhusu suala la Wabunge 19 linaloendelea Mahakamani, Mhe. Shariffa amemuomba Rais alitazame kwa undani na kulipatia majibu. Amewakaribisha wanachama waliokimbia nchi wajisikie nyumbani nankuwahakikishia kuwa zama za kutekana na kupotezana hazina nafasi kwa sasa.


JOHN MNYIKA, KATIBU MKUU CHADEMA
Akimkaribisha Mwenyekiti wa Chama chake, Mhe. Mnyika ametoa mapendekezo ya kuikumbusha serikali pamoja na vyama vyote vya kisiasa kuwa kila jambo wanalofanya liwe linazingatia maslahi na makatwa ya wananchi kwa kuwa hii ni nchi yao. Pia, amesema watanzania wanalia ugumu wa maisha na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

9335EB12-ECA4-4BBD-AAB9-4E127961CDF0.jpeg

John Mnyika, Katibu Mkuu Chadema
Amemuomba Rais pamoja na Mhe. Mbowe katika safari ya maridhiano wanayoenda nayo kutokusahau mambo hayo mawilli.

FREEMAN MBOWE, MWENYEKITI WA CHADEMA
Amewashukuru wanawake wa BAWACHA pamoja na Rais Samia kwa kushiriki mkutano huu wenye lengo la kuimarisha umoja na mshikamano kama taifa.

Amesema kuwa wanawake wa Chadema kama walivyo wanaume wa chama hicho hubaguliwa na kupitia maumivu mengi kwa sababu za kichama. Amekumbusha kuwa baada ya kualikwa Ikulu siku ya kwanza alipotoka jela walisisitiza haki kwa kuwa huliinua taifa.

Pasipo haki, Taifa hulaanika. Amemshukuru Rais kwa kuyapa nafasi maridhiano pamoja na kuonesha nia ya kuthubutu katika kurejesha haki na kuondoa mpasuko wa kitaifa uliokuwepo.

Suala la watu kujiita chawa wa mama, Mhe. Mbowe amesema "Unafiki na uongo hulaanisha taifa. Taifa letu lina watu wengi wasio sema na kuuishi ukweli. Hili ni chimbuko kubwa la mporomoko wa maadili. Nakusihi sana mama, epuka mtu yeyote anayejiita chawa wako"

3DC32F67-F14C-494A-B5B3-D94AACD5D4DD.jpeg

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Kama wapinzani wataendelea kuishughulikia serikali pasipo uoga na uchawa. Lakini Viongozi wa nchi wanapaswa kuwa na hofu ya kweli ya Mungu pasipo kujinasibu kwa maneno pekee. Wanapaswa kuchaguliwa na kuingia madarakani kwa njia za kidemokrasia na kuwatumikia wananchi bila kuwaumiza.

Kwa Miaka mingi, CCM imekosa uhalali wa kukemea maovu yanayofanyika nchini hasa rushwa na ufisadi kwa kuwa CCM imeliumiza taifa hili. Kama mbavyo mtaani mwizi wa kuku huitwa mwizi, mtu anayeiba kura pia ni mwizi. Serikali na CCM walipaswa kuwaomba msamaha watanzania kwa mambo waliyopitia, wanapaswa kujenga mfumo wa kuwawajibisha viongozi wao pale wanapotenda uovu bila kuwakumbatia.

Suala la Wabunge 19, Mhe. Mbowe amesisitiza kuwa chama chake hakikuwateua, bali walipelekekwa Bungeni kwa hila na Serikali iliyopita.

“Kuna baadhi ya vyombo vya habari vimevumisha kuwa sisi tumekubaliana kupeleka Wabunge 19 ambao hawakutokana na maamuzi yetu ya chama ni uhuni na uvunjaji wa sheria ambao unapaswa kupingwa na yeyote anayependa haki.

Ameongeza "Jambo la Wabunge 19 linatukwaza sana na nina hakika linawakwaza watu wengi sana. Pamoja na kuwa kesi ipo Mahakamani lakini hakuna zuio lolote linawafanya Wabunge wale 19 waendelee kuwa Wabunge, wale hawawakilishi watu bali wanawakilisha familia zao."

Amemuomba Rais kuzihurumia kodi za wananchi wanyonge wanaolipa kodi ambazo baadhi yake zinaenda kulipa hao wabunge wasio na baraka ya chama na wananchi.

SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Ameshukuru kwa kualikwa kwenye mkutano huu wenye lengo la kuwathamini na kuwapa haki wanawake wa Tanzania na duniani kote. Rais Samia Suluhu Hassan amesema “Huwezi kuitwa na Wananchi wako ukasema ‘siji’, nilifurahi kuja kwa kuwa nitasikia CHADEMA wanasema nini, na nimesikia Wanawake wa CHADEMA na CHADEMA kama chama kinasema nini.”

Ameongeza, “Wanasema haijapata kutokea, kwangu mimi ni faraja na leo tunaandika historia mpya ya kuendelea kuliunganisha taifa letu.

DD311D6E-9F73-4C59-BBFA-2E058EE1FF09.jpeg

Samia suluhu Hassan, Rais wa Tanzania

Kuhusu Kutembelea Jukwaa la JamiiForums, Rais Samia Suluhu Hassan amesema “Huwa napitia Jamii Forums nasoma maoni yenu kule ndani, nasoma ninacheka, nasema lakini huu ni utamaduni mpya si rahisi kukubalika kwa ghafla, kwahiyo pande zote Tanzania nzima si rahisi kukubali utamaduni huu mpya kwa haraka
Amesema Watanzania wanatakiwa kuwa wamoja na mazungumzo yanatakiwa kuendelea licha ya vikwazo mbalimbali.

Ameongeza “Lakini wakiona matunda ya yanayotokea utamaduni utakubalika. Hakuna mwanadamu kaumbwa anapenda ugomvi tu, kila mwanadamu anapenda amani yar oh yake, tujenge amani ya moyo wetu.”

Chadema kushika dola mwaka 2025, Rais Samia amesema "Ndugu zangu siasa ni mchezo wa kulumbana kwa hoja Wote tukiwa na lengo la kushika dola kama alivyosema Mwenyekiti wa BAWACHA na Freeman Mbowe. Kwa sura nazoziona hapo hamna nia ya kushika dola 2025 mnajua Mama yupo dhamira hiyo haipo."

"Lakini niseme yes wote tuna lengo hilo lakini tukafanye kistaarabu kama Wanaadamu kama watu. Tuheshimiane, tuheshimike duniani."

Aidha Rais Samia ameongeza "Nataka niwaambie kitu kwa kipindi hiki kifupi nchi yetu inaheshimika sana duniani. Kwahiyo tusiirudishe chini, tusiirudishe nyuma. Twendeni na mwendo huu tuweke heshima ya nchi yetu pale inapostahiki. Tanzania ni taifa kubwa tusilitolee sifa yake."

Suala la Katiba Mpya, Rais Samia amesema kuwa yeye na chama chake wapo tayari kulifanyia kazi na muda si mrefu kamati maalum itaundwa kwa kushirikiana na vyama vyote vya siasa.

Suala la mmomonyoko wa maadili kwa jamii yetu hakuna mtu wa kumlaumu, dunia na nchi ilitetereka kwenye malezi, dini kwani sehemu paliposhikwa dini mambo haya hayawezi kutokea. Amewataka watanzania kuwaza ni wapi tulikosea ili tujisahihishe na kulinda heshima yetu kama nchi. Yale ya kuletewa tubapaswa kuyakataa kwani yakiingia hayaumizi mtu mmoja bali taifa zima.

Akimalizia kuhusu suala la wabunge 19, amesema kuwa Mahakama iachwe ifanye kazi yake kwa kuwa hata kama yeye ni Rais bado hana mamlaka ya kugusa huko.

Amewashukuru BAWACHA kwa mkutano huu, amefarijika kwa zawadi aliyoandaliwa na amewatakia kila lakheri katika kuendeleza mshikamano na umoja wa nchi.
 
Dah, mwamba ni jiniazi sana na anaijua shilingi kama ada ya mchagga.
Hapo ataonekana anatoa maneno ya busara kama zote huku akilamba lamba mdomo kuashiria utamu wa asali.

Kuna mtu anapiga kelele uviko-19+1 wafukuzwe chamani, wafukuzwe wakati kuna harufu ya asali? Tuache kuota ndoto za mchana labda siyo DJ.
 
Back
Top Bottom