Rais Samia, kuna mtu mmoja tu hapa Tanzania anaweza kukusaidia kuuvuka huu mtihani wa DP World na TEC - muite, ongea nae, msikilize, ufanye atachosema

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Raisi Samia, kwa sababu ya mambo fulani yaliyojitokeza hupa JF Forums, niliahidi kutotoa post tena. Lakini kwa ajili yako nimeamua kuvunja mwiko huo.

Nimefuatilia kwa makini sana yanayoendelea juu ya suala la DP World, jinsi lilivyoshughulikiwa Bungeni, na sasa kufikia hatua ya tamko la TEC. NI kweli kwamba suala hili linazidi kuweka taswira mbaya sana nchini, na huenda linakukosesha usingizi kwa kuwa hukutarajia litafika huku. Nahisi pia kuna mambo ambayo hatujui, labda upande wa UAE-Dubai, yanayolifanya liwe gumu hata zaidi. Na usipoangalia mambo yatazidi kuharibika.

Sasa maraisi wa kabla yako wamewahi kupitia vipindi vigumu kama vyako. Raisi Mkapa kuna wakati kulikuwa na suala na rada ya BAE. Serikali ya Uingereza ikamsumbua sana. Akaomba huyu mtu nitakaekutajia mwishoni amsaidie kulitatua. Na matokeo ni kwamba huyu mtu alilitatua kwa namna ambayo ilimfanya Raisi Mkapa amheshimu sana, kwa kuwa alilitatua kwa namna ya hekima, na ufahamu wa hali ya juu, hata Uingereza wakamsifia kwa hekima zake kwa jinsi alivyolitatua.

Kisha wakati fulani uhusiano kati ya Raisi Kikwete na Raisi Kagame uliharibika sana, hata Raisi Kagame akatishia kumpiga Raisi Kikwete. Kuona hivyo, Raisi Kikwete ikabidi amuombe huyu mtu asaidie kulimaliza hili suala, na kwa mara nyingine akalimaliza kwa namna ya busara sana iliyorejesha uhusiano kati ya Tanzania na Rwanda kwenye hali ya kawaida. Kutoka hapo Raisi Kikwete aliamua huyu mtu akae karibu yake katika ofisi ya Raisi ili azidi kumsaidia mambo mengine mengi.

Na labda nikuambie pia wakati fulani kulikuwa na suala la kupeleka boti za abiria kwenye ziwa Victoria, na mtangulizi wako Raisi Magufuli akagoma katakata kuzipeleka boti hizi kupitia barabara zetu. Hii ilileta mtafaruku sana kati ya mfanyabiashara maarufu nchini na serikali. Huyo huyo mtu ninaekuambia akaamua kuingilia kati na kuwasiliana na serikali ya Kenya. Kwa diplomasia yake serikali ya Kenya ilikubali kutatua tatizo hili. Jinsi alivyotatua tatizo hili ilimletea heshima sana kwa baraza la mawaziri Kenya na Tanzania, japo ilimfadhaisha sana Magufuli, wakati huo akiwa waziri katika serikali ya Kikwete, na kufanya awe na chuki nae, chuki aliyoiendeleza hata alipochaguliwa kuwa raisi.

Na labda utakuwa unajua kwamba huyu mtu aliingizwa katika serikali kutokana na ushauri wa Raisi Clinton kwa Mkapa. Raisi Clinton alishangaa sana kwamba kwa nini serikali ilikuwa haimtumii mtu huyu ambae Raisi Bill Clinton na Makamu wake Al Gore walimsifia sana kwa jinsi alivyoshughulikia kwa umakini mkubwa na busara za hali ya juu negotiations za climate change akiwa msemaji wa Group of 77 and China. Mkapa akawasikiliza.

Japo si mwanasheria, kuna wakati, Tanzania na nchi nyingine za mto Nile wakiwa katika mkutano wa kusign makubaliano ya Mto Nile, alizuia utiaji sahihi wa makubaliano hayo baada ya kugundua vipengele katika mkataba huo ambavyo mawaziri wa nchi nyingine hawakuviona. Vilikuwa vipengele ambavyo vilitoa faida kubwa kwa nchi moja ya mto Nile na kuondoa haki ya matumizi ya maji kwa nchi nyingine, vikiwa vimeandikwa kimaficho. Hizi nchi nyingine zikamsifia sana kwa umakini wake hadi kugundua hilo.

Kuna mambo mengi sana amefanya ambayo watu walimsifia kwa busara na hekima zake, ndani na nje ya Tanzania, siwezi kuyaweka yote hapa.

Mtu huyu anaitwa Prof. Mark Mwandosya. Muite, kaa nae, mwache akushauri kwenye hili jambo, na tekeleza atakachokuambia. Umekuwa ukiwasikiliza watu ambao wanakuambia nguo yako isiyoonekana inakupendeza sana - wanakudanganya na wanakupotosha wakidhani wanakuambia kile unachotaka kusikia ili uendelee kuwa nao. Mwite Prof. Mwandosya mkae nyie wawili tu kutafuta way forward juu ya jambo hili - na nakuambia utanitafuta kunishukuru kwa huu ushauri wa bure ninaokupa hapa. Kila la kheri.
 
Sasa wewe umemjuaje huyu mtu?

Jamaa umetumia kigezo gani cha kisayansi kujua, he is the one and only One can do that??

Tunahitaji muafaka ila walau njia tunazopendekeza walau ziwe scientifically hata kwa 75% tu inatosha

Sijabisha ila nataka kujua hiyo randomized sampling technique yako umefanyaje??
 
Sisi tayari tuna maagizo ya baraza la maaskofu wa kikatoliki na jukumu letu ni kuyatii bila kigugumizi chochote kile.
 
Attachments

  • IMG-20230820-WA0008.jpg
    IMG-20230820-WA0008.jpg
    58.5 KB · Views: 2
Tunajua uwezo mkubwa sana wa Prof Mwandosya ....ikibidi na kumpendeza Rais SSH basi afanye na aliponye Taifa tunakoenda si kuzuri kabisa ....ataingia kwenye historia mbaya kabisa......malumbano ya kidini sio afya kwa Taifa .....tutakuchukua na kukuchoka hutakuwa jinsi .....bali kutupisha !:lwa maslahi mapana Tanzania
 
Raisi Samia alipaswa kuteua timu yake ya kumshauri masuala yake yeye mwenyewe binafsi yaani "Personally".

Hivi ndivyo wafanyavyo viongozi wengi wenye nia njema na nchi zao.

Kuna watu hadi wanasaikolojia ambao humshauri kiongozi pale penye matatizo yanohitaji akili kuchambua kwa makini masuala mazito kabla ya kuja na uamuzi.

Timu ya washauri binafsi ambao si lazima wawe kwenye payroll ya serikali.

Hivyo, badala ya kumteua profesa Mwandosya kwenda EWURA kula pensheni ni bora awe mshauri wako wa karibu umlipe kama "private consultant or adviser" kuliko kwenda EWURA kuzuia nafasi kwa vijana.

NB
Naomba nitofautishe wasaidizi na washauri wa raisi ni watu tofauti.
 
Sasa wewe umemjuaje huyu mtu?

Jamaa umetumia kigezo gani cha kisayansi kujua, he is the one and only One can do that??

Tunahitaji muafaka ila walau njia tunazopendekeza walau ziwe scientifically hata kwa 75% tu inatosha

Sijabisha ila nataka kujua hiyo randomized sampling technique yako umefanyaje??
Kuna wakati akili zetu sisi waafrika ni za aina ya pekee.

Yaani pamoja na jamaa kuelekeza masuala kadhaa ambayo profesa Mwandosya ameyafanya hapo juu weye bado hujaelewa.

Kweli tuna safari ndefu sana.
 
Raisi Samia, kwa sababu ya mambo fulani yaliyojitokeza hupa JF Forums, niliahidi kutotoa post tena. Lakini kwa ajili yako nimeamua kuvunja mwiko huo.

Nimefuatilia kwa makini sana yanayoendelea juu ya suala la DP World, jinsi lilivyoshughulikiwa Bungeni, na sasa kufikia hatua ya tamko la TEC. NI kweli kwamba suala hili linazidi kuweka taswira mbaya sana nchini, na huenda linakukosesha usingizi kwa kuwa hukutarajia litafika huku. Nahisi pia kuna mambo ambayo hatujui, labda upande wa UAE-Dubai, yanayolifanya liwe gumu hata zaidi. Na usipoangalia mambo yatazidi kuharibika.

Sasa maraisi wa kabla yako wamewahi kupitia vipindi vigumu kama vyako. Raisi Mkapa kuna wakati kulikuwa na suala na rada ya BAE. Serikali ya Uingereza ikamsumbua sana. Akaomba huyu mtu nitakaekutajia mwishoni amsaidie kulitatua. Na matokeo ni kwamba huyu mtu alilitatua kwa namna ambayo ilimfanya Raisi Mkapa amheshimu sana, kwa kuwa alilitatua kwa namna ya hekima, na ufahamu wa hali ya juu, hata Uingereza wakamsifia kwa hekima zake kwa jinsi alivyolitatua.

Kisha wakati fulani uhusiano kati ya Raisi Kikwete na Raisi Kagame uliharibika sana, hata Raisi Kagame akatishia kumpiga Raisi Kikwete. Kuona hivyo, Raisi Kikwete ikabidi amuombe huyu mtu asaidie kulimaliza hili suala, na kwa mara nyingine akalimaliza kwa namna ya busara sana iliyorejesha uhusiano kati ya Tanzania na Rwanda kwenye hali ya kawaida. Kutoka hapo Raisi Kikwete aliamua huyu mtu akae karibu yake katika ofisi ya Raisi ili azidi kumsaidia mambo mengine mengi.

Na labda nikuambie pia wakati fulani kulikuwa na suala la kupeleka boti za abiria kwenye ziwa Victoria, na mtangulizi wako Raisi Magufuli akagoma katakata kuzipeleka boti hizi kupitia barabara zetu. Hii ilileta mtafaruku sana kati ya mfanyabiashara maarufu nchini na serikali. Huyo huyo mtu niaekuambia akaamua kuingilia kati na kuwasiliana na serikali ya Kenya. Kwa diplomasia yake serikali ya Kenya ilikubali kutatua tatizo hili. Jinsi alivyotatua tatizo hili ilimletea heshima sana kwa baraza la mawaziri Kenya na Tanzania, japo ilimfadhaisha sana Magufuli, wakati huo akiwa waziri katika serikali ya Kikwete, na kufanya awe na chuki nae, chuki aliyoiendeleza hata alipochaguliwa kuwa raisi.

Na labda utakuwa unajua kwamba huyu mtu aliingizwa katika serikali kutokana na ushauri wa Raisi Clinton kwa Mkapa. Raisi Clinton alishangaa sana kwamba kwa nini serikali ilikuwa haimtumii mtu huyu ambae Raisi Bill Clinton na Makamu wake Al Gore walimsifia sana kwa jinsi alivyoshughulikia kwa umakini mkubwa na busara za hali ya juu negotiations za climate change akiwa msemaji wa Group of 77 and China. Mkapa akawasikiliza.

Kuna mambo mengi sana amefanya ambayo watu walimsifia kwa busara na hekima zake, ndani na nje ya Tanzania, siwezi kuyaweka yote hapa.

Mtu huyu anaitwa Prof. Mark Mwandosya. Muite, kaa nae, mwache akushauri kwenye hili jambo, na tekeleza atakachokuambia. Umekuwa ukiwasikiliza watu ambao wanakuambia nguo yako isiyoonekana inakupendeza sana - wanakudanganya na wanakupotosha wakidhani wanakuambia kile unachotaka kusikia ili uendelee kuwa nao. Mwite Prof. Mwandosya mkae nyie wawili tu kutafuta way forward juu ya jambo hili - na nakuambia utanitafuta kunishukuru kwa huu ushauri wa bure ninaokupa hapa. Kila la kheri.
Umeongeza utumbo we mwandosya. Acha kujipigia debe huna lolote
 
Kwani yeye hawezi kuchukua maamuzi mazuri hadi apate ushauri kutoka kwa mtu.Jibu lililobaki ni kurekebisha vile vipengele vya kilofa na kijuha ambavyo vimeelezwa haihitaji tena kurudiwa au aachane nao kabisa mkataba.kama hawezi kuchukua maamuzi ambayo hata mtoto wa miaka kumi angeweza basi itakuwa hatoshi kuwaongoza watanzania
 
Raisi Samia alipaswa kuteua timu yake ya kumshauri masuala yake yeye mwenyewe binafsi yaani "Personally".

Hivi ndivyo wafanyavyo viongozi wengi wenye nia njema na nchi zao.

Kuna watu hadi wanasaikolojia ambao humshauri kiongozi pale penye matatizo yanohitaji akili kuchambua kwa makini masuala mazito kabla ya kuja na uamuzi.

Timu ya washauri binafsi ambao si lazima wawe kwenye payroll ya serikali.

Hivyo, badala ya kumetua profesa Mwandosya kwenda EWURA kula pensheni ni bora awe mshauri wako wa karibu umlipe kama "private consultant or adviser" kuliko kwenda EWURA kuzuia nafasi kwa vijana.

NB
Naomba nitofautishe wasaidizi na washauri wa raisi ni watu tofauti.
anasikiliza kina nape
 
Back
Top Bottom