Hizi taarifa zinatisha sana. Kwa kweli mleta maada kama taarifa zako ni kweli basi umeamua kujilipua kabisa na unafanya kazi iliyotukuka na ya kizalendo hasa. Ni wakati sasa wa vyombo vya serikali kulifanyia uchunguzi hili suala kwa kina na kufikisha kunapohusika ili kama kuna watu wanahujumu wachukuliwe hatua za kisheria haraka. Kila siku najiuliza hivi Tanzania hatuna waandishi wa habari za kiuchunguzi maana ndio eneo la hili lakini utakuta wanahangaika na mambo ambayo hayana tija kwa taifa hili.
Nilikuwa nafika hapo Chibuku kwa shughuki fulani wakati huo meneja anaitwa Kazonda kama sikosei. Baadaye nilibadili upepo nikaingia kwenye shughuli nyingine sasa siku ya siku napita hapo kuulizia naambiwa kiwanda kimefungwa. Nilishangaa kwani Chibuku kilikuwa kiwanda kinafanya kazi vizuri sikutegemea kingekufa kifo cha ghafla kiasi kile. Malighafi zake ni nafaka zinazlimwa hapa hapa Tanzania na pombe yake ni nzuri kwa sababu ni lishe pia. Na wafugaji walikuwa wanajipatia mabaki kwa ajili ya kulishia mifugo yao.