Rais Samia Kiwanda cha Chibuku/ Darbrew LTD kilifungwa tangu mwaka 2018. Muwekezaji yupo lakini Watendaji wa Jiji la Ilala wanakwamisha

Autodidacts

JF-Expert Member
Jun 9, 2021
1,165
1,803
DARBREW LTD ni kiwanda cha kutengeneza pombe aina ya chibuku,kilianzishwa tangu mwaka 1967 na kampuni binafsi LONRHO corporation. Serikali ilikitaifisha kiwanda hicho mwaka 1978 na kukiendesha kwa mafanikio.Kilianza kuwa na ubia mwaka 1997 ambapo serikali ilikuwa na hisa ya 40% na sekta binafsi 60% chini ya Tanzania Breweries Limited(TBL).

Kiwanda leo hii kina uwezo wa kuajiri ajira za moja kwa moja zaidi ya watu 150 na zisizo za moja kwa moja zaidi ya laki mbili(200,000). Kina uwezo wa kupokea nafaka tani zaidi ya milioni moja(1,000,000) kwa mwaka.Thamani ya kiwanda ni zaidi ya fedha za kitanzania bilioni 40! Ni kati ya viwanda vichache sana vilivyobaki kama legacy ya awamu ya kwanza.

Kiwanda cha DARBREW LTD hakikuwahi kufungwa tangu kuanzishwa kwake,hadi ilipofika mwaka 2006 kwa ajili ya uendeshaji mbovu wa TBL,kilisimama kwa siku chache,ata ivyo mwaka huo huo alipatikana muwekezaji mwingine kutoka Malawi na kununua hisa za 60% kutoka TBL. Muwekezaji huyu alipata mafanikio makubwa kiasi kuwa mmoja wa walipa kodi wakubwa kuzidi ata kampuni za kuchimba madini.

Ilipofika mwaka 2013,TBL walitamani kuwekeza tena katika kiwanda hiki baada ya kuona ufanisi wake na kumlazimisha muwekezaji huyo kutoka Malawi awauzie hisa 60% . TBL walifanikiwa kununua hizo hisa tena ivyo kuanza kuendesha kiwanda hicho kuanzia mwaka 2013. Kwa ajili ya uongozi mbaya na hasa uongozi wa aliekuwa meneja mauzo wakati huo ndg.Fred Kazindogo alietokea TBL na sasa ni muajiriwa wizara ya kilimo na mifugo,kiwanda kilisitisha tena uzalishaji mwaka 2018(Kwa sababu tu ya uongozi mbovu/poor management chini ya TBL)hadi leo hii bado hakijaanza uzalishaji.

Muwekezaji aliyekuwepo kati ya mwaka 2006-2013 na kuendesha kiwanda kwa mafanikio,amejitokeza kuomba tena tangu mwaka 2019 aruhusiwe kuendesha hicho kiwanda lakini kuna ukiritimba ufuatao hadi leo hii;

1.TBL kwa makusudi hawataki kiwanda kifunguliwe kwa kuwa kuna hujuma imefanyika kwa upande wa lililokuwa jiji la Dar Es Salaam na hawataki ijulikane. Hujuma yenyewe ni TBL kuuziwa sehemu ya ardhi kilipo kiwanda cha chibuku kinyume na sheria za mali za umma,pia wanalihitaji eneo hilo ambalo kimsingi ni mali ya serikali,eneo lina ukubwa wa zaidi ya 15,000 sqm. linapatikana Ubungo mkabala na stendi ya mabasi ya mwendokasi Ubungo,upande wa kushoto kama unaelekea Ubungo njia panda au mataa. Pia tuna taarifa ya kipande cha ardhi ya DarBrew kukodishwa bure kwa TBL kuanzia mwaka 2019 eti ili kufidia hasara ya tshs bilioni 29 waliyopata TBL wakiwa DarBrew. Huu ni wizi wa kumulikwa.

2. Kutokana na hujuma ya hapo juu, watendaji wa lililokuwa jiji la Dsm,hasa mwanasheria wa jiji aitwae Mtinange(alishirikiana na kulindwa sana na aliekuwa katibu mkuu TAMISEMI eng. Joseph Nyamhanga) ambae sasa huyu mwanasheria kahamishiwa mkoa wa Pwani,na aliekuwa mkurugenzi wa jiji la Dsm ndugu Spora ambae sasa kahamishiwa Kinondoni,pamoja na baadhi ya watendaji wa lililokuwa jiji la Dsm, kwa kushirikiana na watendaji wa TBL hasa mwanasheria Huruma Ntahena,walihusika kuhujumu kiwanda kisifunguliwe kuficha kashfa hii.

3. Pia TBL wana hofu ya uwepo wa chibuku sokoni unapunguza wateja wao,ivyo wameamua kusimamisha kiwanda ili kulinda bidhaa zao. Ingawa dhana hii haina nguvu ya uhalisia ila ipo.

HALI ILIVYO SASA
Mpaka leo hii kiwanda hakijafunguliwa licha ya jiji la Ilala kuwa na taarifa za kuwepo kwa muwekezaji wa Malawi kutaka kuwekeza na amewapa proposal tangu mwaka 2019 na yuko tayari kukiendesha kwa bei inayotaka serikali,mkurugenzi wa Ilala ana taarifa,Meya ana taarifa.

Lakini wote wanaendeleza ule ule uozo wenye kila dalili za rushwa uliofanywa na watendaji wa lililokuwa jiji la Dsm. Mwanasheria wa jiji la Ilala Flora Luhala ni mmoja wa wahusika wakuu kwa sasa na anashirikiana na mwanasheria wa TBL Huruma(mastermind) kuendelea kuhujumu sera za viwanda,hoja wanayosingizia kuwa kiwanda kina deni la sh.milioni themanini(80,000,000) ,muwekezaji wa Malawi yuko tayari kulipa(na wanalijua hili) ili aendeleze uzalishaji lakini bado anasumbuliwa kwa hoja kuwa inasubiriwa tax clearance kutoka TRA(na hoja hii ni tangu mwaka 2019).

Mbunge wa Ubungo Prof. Kitila yupo na ana taarifa lakini kaingia ubaridi, waziri Jaffo aliekuwa TAMISEMI nae aliingia ubaridi. Kuna taarifa za uhakika kuwa TBL wanalipa pesa nyingi uko jiji kwa baadhi ya watendaji ili hatimae waendelee kumiliki kipande cha ardhi walichouziwa kinyemela,na lengo ni kutaka kuuziwa eneo lote endapo mkakati wao wa eneo kutangazwa kufilisika kwa kuitumia TRA kwa kigezo cha kodi kutokulipwa kama utafanikiwa. Ni mkakati uliopangwa kwa ustadi mkubwa kwa ushirika wa TBL na watendaji wa lililokuwa jiji la Dsm,na hawa wa sasa ,yaani jiji la Ilala ya sasa, wamehusishwa.

WITO KWA SERIKALI
Sisi tuliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha DARBREW LTD tunaomba serikali yako mh. Rais iingilie kati ili kiwanda kifunguliwe kwa haraka maana mitambo ni salama,muwekezaji yupo na malighafi zipo.

Pia waliochelewesha uwekezaji wawajibishwe hasa watendaji wenye kutanguliza maslahi binafsi kwenye jambo lenye maslahi ya umma,hawa ni wahujumu uchumi maana wameipotezea serikali kodi nyingi kwa muda wote tangu mwaka 2018 hadi leo hii,wamesababisha lawama kwa serikali kwa ukosefu wa ajira na wamepoteza sehemu ya soko la mazao ya kilimo, lakini pia wanasababisha mitambo kuweza kupata kutu na kufanya uwekezaji uwe wa gharama kubwa. Mwisho,tunaomba muwekezaji huyu wa Malawi apewe kipaumbele maana ndie aliendesha kiwanda hiki kwa mafanikio makubwa na kwa faida ya serikali kati ya mwaka 2006-2013 na kumbu kumbu zipo.

Tunawasilisha.

Tuliokuwa wafanyakazi wa DARBREW LTD(Dar Es Salaam Breweries Limited),kiwanda cha kutengeza chibuku.


image005.jpg
 
Sisi tuliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha DARBREW LTD tunaomba serikali iingilie kati kuwawajibisha watendaji hao waovu wenye kutanguliza maslahi binafsi kwenye jambo lrnye maslahi ya umma, hawa ni wahujumu uchumi maana wameipotezea serikali kodi nyingi kwa muda wote tangu mwaka 2018 hadi leo hii. Pia tunaomba muwekezaji huyu wa Malawi apewe kipaumbele maana ndie aliendesha kiwanda hiki kwa mafanikio na kwa faida ya serikali mwaka 2006-2013.

Tunawasilosha.

Ni sisi tuliokuwa wafanyakazi wa DARBREW LTD-Dar Es Salaam Breweries Limited kiwanda cha kutengeza chibuku.
 
Kiwanda kimefungwa tangu mwaka 2018 hadi leo,mitambo ipo na inafanya kazi,muwekezaji yupo na anataka sana kuwekeza hapo lakini watendaji wa jiji la Ilala wanatanguliza maslahi binafsi mbele. Sababu wanayoitoa haina mashiko,wanasema kodi ya sh mil.80 bado haujalipwa na TBL na wanasubiri tax clearance kutoka TRA na hii ni tangu mwaka 2019!

Muwekezaji kawaambia yuko tayari kulipa hiyo kodi lakini anaambiwa asubiri. Ajira zinapotea, kodi inapotea, mitambo inapata kutu. Tumechunguza na kugundua kuwa watu wa jiji wamewauzia TBL kipande cha ardhi ambayo ni sehemu ya DARBREW LTD na hawataki hili lijulikane, maana akija muwekezaji mwingine siri hii itajulikana, mheshimiwa Rais Samia na serikali yako tunaomba sana muwashughulikie hao wala rushwa tafadhali.
 
Sisi tuliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha DARBREW LTD tunaomba serikali iingilie kati kuwawajibisha watendaji hao waovu wenye kutanguliza maslahi binafsi kwenye jambo lrnye maslahi ya umma,hawa ni wahujumu uchumi maana wameipotezea serikali kodi nyingi kwa muda wote tangu mwaka 2018 hadi leo hii.Pia tunaomba muwekezaji huyu wa Malawi apewe kipaumbele maana ndie aliendesha kiwanda hiki kwa mafanikio na kwa faida ya serikali mwaka 2006-2013.
Tunawasilosha.
Ni sisi tuliokuwa wafanyakazi wa DARBREW LTD-Dar Es Salaam Breweries Limited kiwanda cha kutengeza chibuku.
Mama akiisikia hii na kuishughulikia,wadau jiandaeni na ajira za ukweli maana sisi tunaijua DARBREW na imetulea sana hapa mjini,halafu wanajitokeza waharibifu wachache wanaharibu
 
Tanzania breweries kabla ya ubinafshaji ilikuwa inatengeneza vinywaji bora sana,vilivyogunduliwa na wazalendo wasomi waliosemeaga ukemia Kule ujerumani.

Alivyopewa m south akabadilisha formula yote,tulikuwa tunalima ngano barley kwa ajili ya kuuzia TBL msouth akasema ngano yetu haina ubora kwa hyo tukapigwa pin ngano ikawa inatoka south tu.

Ile safari lager ya zamani ilikuwa noma ukipiga tatu we kidume,ya sasa hivi ni utopolo tu kama maji.

Konyagi ya zamani ya Tanzania distilleries ilikuwa nzuri sana mpaka wakenya waliijua Ila ya sa hivii WWII inapigwa na kvant.
 
Dah kumbe ndio mana mlipotea, nakumbuka yale mabuyu yalikua yanauzwa buku, tulikua tunanunua carton hata 100 au 70 zinaisha ndani ya siku..
Fight mkuu mrudi sokoni tupige pesa, japo soko wanaweza anza kwa shida kidogo.
Soko bado liko vizuri sana, wateja wanaulizia sana chibuku...tena hili la wateja wetu market share ya chibuku ni kubwa sana upande wa traditional beverages. TBL wanafikiri chibuku inawachukulia wateja wao. Hii tabia ya TBL kutumia ubia wake na serikali kuumiza kampuni zingine hawajaanza leo,TBL wana kitengo cha cooperate ambacho kazi yake ni kulinda maslahi ya TBL,kampuni ambazo wanaona ni tishio kwao eg. ilivyotokea kwa Kibo Breweries,wanahakikisha hazisimami
 
Mkirudi mtakuta kizazi cha wanywa chibuku wamehamia kwenye double kick wanatetemeka tu mikono na midomo kama wagonjwa wa matenguchi.
Chibuku ni lishe pia,na ilisaidia sana watu kuepuka aina ya vinywaji unavyozungumzia, sokoni tunaingia very soon mkuu. Tusaidiane tu kusambaza taarifa hizi za hujuma zifike kwa wakubwa kwa maamuzi
 
Ndio nzuri zaidi, ukizingatia Wananchi waliowengi wamepata Malnutrition kutokana na Awamu ya Magufuli.
😁
Wadau tupambane kwa pamoja kupiga kelele turudishe kiwanda hiki ili sisi,watoto wetu,jamaa na marafiki wapate ajira,200,000 zisizo za moja kwa moja na ajira 150 za moja kwa moja. Tumsaidie mama Samia kuleta sulubu,karibuni CCM,CHADEMA, na vyama vyote na wadau wote tuungane kwenye hili angalau
 
😂😂
Wadau tupambane kwa pamoja kupiga kelele turudishe kiwanda hiki ili sisi,watoto wetu,jamaa na marafiki wapate ajira,200,000 zisizo za moja kwa moja na ajira 150 za moja kwa moja. Tumsaidie mama Samia kuleta sulubu,karibuni CCM,CHADEMA, na vyama vyote na wadau wote tuungane kwenye hili angalau
Swadakta! Tanzania yetu Chibuku yetu.
 
Back
Top Bottom